Wanabodi.
Wanaohamia CCM Wasibezwe, Wanaona Mbali, Majimbo Yote Kurejeshwa?, Jee Tunarejea Kuwa Nchi Chama Kimoja?
Politics is a game of hide and seek and the changing variables, hivyo kwa mazingira ya sasa ya siasa za Tanzania ya Magufuli, wanasiasa karibu wote walioko upinzani, with very few exceptions, wenye uwezo wa kuona mbali kwa kusoma trends za kisiasa kwa kuangalia mwelekeo wa 2025, kwa matokeo haya, watakuwa wameishasoma mazingira yaliyopo na hali halisi ya siasa zetu za Tanzania na siasa za upinzani nchini katika kipindi hiki na their chances ya upinzani kushinda kata yoyote au jimbo lolote kuelekea 2025, hivyo, wenye kuona mbali, wameamua kufanya uamuz wa mapema kwa kuvihama vyama vyao sasa kwa kujiunga CCM!, ili ku secure their positions mapema badala ya kusubiri kifo hiyo 2025!