LGE2024 Wanaoharibu uchaguzi wanamwamini Mungu au wanaamini chama tawala?

LGE2024 Wanaoharibu uchaguzi wanamwamini Mungu au wanaamini chama tawala?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kinachoendelea nchini aibu kubwa sana ndani na machoni pa mataifa mengine.

Tumefikaje hatua ya watendaji wa serikali kuua mwananchi na mwanasiasa kwa sababu ya uchaguzi wa ujumbe wa serikali za mitaa?

Kama uchu wa madaraka umekuwa mkubwa kiasi cha kuua mjumbe wa shina je nini kitatokea kwa Diwani, Mbunge na Rais?

Tunategemea Mungu au tumeamua kumwacha na kujiamulia tunavyojisikia wenyewe? Tunaivuruga Tanzania kwa kuondoa haki miyoyoni wa wananchi kwa manufaa ya nani?

Tukubali tukatae kwa miaka kumi sasa nchi yetu inazidi kumegwa vipande na umoja na utu unaondolewa kupitia viongozi wa kisiasa na unafiki wa viongozi wa dini.

Viongozi wa dini waliopoacha kukemea mabaya ya viongozi na kujiona wao wanamwabudu watawala kuliko Mungu ndipo hali hii yakuuana ilipozaliwa.

Natambua hata waliopo ndani ya chama tawala wanaumizwa na haya yanayotendwa leo ila dola imewafunga mdomo.

Huu uchaguzi umeonyesha nchi iliyoporomoka kimaadili na namna ambavyo uwanja wa siasa umefutwa kutokana na mifumo iliyowekwa
 
Upinzani si waachane na mambo ya chaguzi, CCM wafanye wenyewe...
 
Hivi ukiwa mwanaccm Mungu ana umuhimu tena? Maana alivyovikataza ndo vinavyofanywa.

Uzuri sirgod hakopeshi, anamchukua mmoja mmoja bila kuangalia status yake ndani ya chama!
 
Back
Top Bottom