#COVID19 Wanaoipinga chanjo ya Covid-19 ipo siku watapanga foleni kuchanjwa

Abby Newton

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2017
Posts
1,252
Reaction score
2,253
Kuna watu wanaishi kwa kuamini kila taarifa.Kwa ujumla ulimwengu wa leo unaendeshwa na habari za uzushi na uongo.Unaposikia au kuambiwa jambo lolote lazima ulichekeche. Ndio maana tukaambiwa akili za kuambiwa changanya na za kwako.

Kuhusu chanjo ya Covid-19, kuna watu tena viongozi wakubwa wa nchi wanasema eti wazungu wanataka kutuangamiza sisi ngozi nyeusi hasa Wafrika eti kupitia hii chanjo.Hiki ni kichekesho kabisa.

Wazungu waliotengeneza chanjo ya Covid-19 ndio waliotengeneza chanjo ya Polio,Kansa ya shingo ya kizazi, hadi chanjo za magonjwa ya mifugo.
Ni hawa hawa ndio wanaotutengenezea vifaa tiba na madawa ya magonjwa mengine km Malaria,Kifua kikuu,STDs,UTI, n.k. Km kweli wangekuwa na ajenda ya kutuua na kutuangamiza si wangeshafanya hivyo "a long ago" kabla ya uwepo wa kizazi chetu cha kuhoji hoji na kudadisi mambo??? Sisi tumeshindwa kutengeneza hata "tooth pick" sembuse chanjo ya Covid-19? Jamani!! Tuache mzaha beee!

Ajenda pekee ya mzungu na mataifa yaliyoendelea ni kuona Wafrika tukiendelea kuwategemea wao kwa kila kitu ili tuendelee kuwa soko kwa bidhaa zao na hatimaye waendelee kututawala. Kama kweli hatutaki kutawaliwa kibiashara na kiuchumi basi tuanze kuchukua hatua za kimkakati na sio hizi za kukurupuka.

Afrika ndio bara lenye idadi kubwa ya vijana,na idadi hii itaendelea kuongezeka muongo kwa muongo. Idadi hii ya vijana inatengeneza soko kubwa kwa bidhaa za kisasa km smartphone,Tvs,nguo, nk. Hivyo wazo la kuangamiza Waafrika ni wazo la mtu asiyejua mifumo ya kibiashara ya dunia ya leo. Kumuangamiza Mwafrika ni kuangamiza biashara ya dunia nzima.

Dunia ya leo ni vigumu kuishi ukitegemea kile unachokiamini peke ako.Tuko katika zama za kuingiliana sana. Kukataa kabisa chanjo ya Covid-19 ni kukataa biashara na wenzako na mwishowe utajikuta umetengwa "and you will suffer the consequences".

Leo hii kitu pekee wanachojivunia Korea Kaskazini ni kumiliki mabomu ya Nyuklia basi. Lakini wananchi wake wanaendelea kuishi katika umasikini wa kutupwa kwa sababu ya kuchukua misimamo mikali isiyo na tija.

Ni kweli hatutakiwi kupokea kila kitu kama jalala lakini si vema kujifanya kichwa ngumu wakati hao tunaowaletea ukaidi ndio wanaotufanya tuwe hivi tulivyo.

Tupokee chanjo ya Covid-19 kiroho safi tu, huku tukiendelea kumuomba Mungu atuepushe na hili janga. Hamna namna wajameni.!
 
Mkuu hawa wanaoipinga hii chanjo usije kushangaa wakachanjwa kabla yetu.

Usizugwe na maneno yao.

Tusishangae kupigwa kumbo wachanjwe wao kwanza.

Wengine wapinga chanjo wanasemekana tayari walishapokea yao muda tu. Hivi wao wako safi.

Nani alishafanikiwa kuwadanganya watu wote siku zote?
 
Wewe chanjwa, wasiotaka kuchanjwa waache wafe. Wataisha mtabaki mliochanjwa.
... kwanini mnazuia hiyo chanjo kuingia nchini? Anyway, mtake msitake mtadhibitiwa tu; dunia haitawaacha mcheze na afya za binadamu wenzenu kisa mna madaraka.
 
Kuhusu chanjo ya Covid-19, kuna watu tena viongozi wakubwa wa nchi wanasema eti wazungu wanataka kutuangamiza sisi ngozi nyeusi hasa Wafrika eti kupitia hii chanjo.Hiki ni kichekesho kabisa.
Kauli zilishabadilika. Sasa wanasema kwa kuwa kuna chanjo 3-4 tofauti zinazopigiwa chapuo, wao watasubiri kwanza wachanjwe watu huko na mwisho wa siku ionekane ipi inafaa zaidi hasa kwa mazingira ya Africa. Then ndipo wanaweza kuamua Nchi ichague kuagiza chanjo ipi baada ya kuassess matokeo yake chanya.

In short, hawataki tuwe miongoni wa “panya wa majaribio”.

Lakini chanjo haitakwepeka, especially kwa wale wanaosafiri nje ya mipaka ya JMT. Ni kama ilivyo sasa Yellow Fever vaccine. Wengi mno hawajachanjwa kwa kuwa hawajawahi kuvuka kupitia terminal three.
 
Kuna watu wanaishi kwa kuamini kila taarifa.Kwa ujumla ulimwengu wa leo unaendeshwa na habari za uzushi na uongo.Unaposikia au kuambiwa jambo lolote lazima ulichekeche. Ndio maana tukaambiwa akili za kuambiwa changanya na za kwako.

Kuhusu chanjo ya Covid-19, kuna watu tena viongozi wakubwa wa nchi wanasema eti wazungu wanataka kutuangamiza sisi ngozi nyeusi hasa Wafrika eti kupitia hii chanjo.Hiki ni kichekesho kabisa.

Wazungu waliotengeneza chanjo ya Covid-19 ndio waliotengeneza chanjo ya Polio,Kansa ya shingo ya kizazi, hadi chanjo za magonjwa ya mifugo.
Ni hawa hawa ndio wanaotutengenezea vifaa tiba na madawa ya magonjwa mengine km Malaria,Kifua kikuu,STDs,UTI, n.k. Km kweli wangekuwa na ajenda ya kutuua na kutuangamiza si wangeshafanya hivyo "a long ago" kabla ya uwepo wa kizazi chetu cha kuhoji hoji na kudadisi mambo??? Sisi tumeshindwa kutengeneza hata "tooth pick" sembuse chanjo ya Covid-19? Jamani!! Tuache mzaha beee!

Ajenda pekee ya mzungu na mataifa yaliyoendelea ni kuona Wafrika tukiendelea kuwategemea wao kwa kila kitu ili tuendelee kuwa soko kwa bidhaa zao na hatimaye waendelee kututawala. Kama kweli hatutaki kutawaliwa kibiashara na kiuchumi basi tuanze kuchukua hatua za kimkakati na sio hizi za kukurupuka.

Afrika ndio bara lenye idadi kubwa ya vijana,na idadi hii itaendelea kuongezeka muongo kwa muongo. Idadi hii ya vijana inatengeneza soko kubwa kwa bidhaa za kisasa km smartphone,Tvs,nguo, nk. Hivyo wazo la kuangamiza Waafrika ni wazo la mtu asiyejua mifumo ya kibiashara ya dunia ya leo. Kumuangamiza Mwafrika ni kuangamiza biashara ya dunia nzima.

Dunia ya leo ni vigumu kuishi ukitegemea kile unachokiamini peke ako.Tuko katika zama za kuingiliana sana. Kukataa kabisa chanjo ya Covid-19 ni kukataa biashara na wenzako na mwishowe utajikuta umetengwa "and you will suffer the consequences".

Leo hii kitu pekee wanachojivunia Korea Kaskazini ni kumiliki mabomu ya Nyuklia basi. Lakini wananchi wake wanaendelea kuishi katika umasikini wa kutupwa kwa sababu ya kuchukua misimamo mikali isiyo na tija.

Ni kweli hatutakiwi kupokea kila kitu kama jalala lakini si vema kujifanya kichwa ngumu wakati hao tunaowaletea ukaidi ndio wanaotufanya tuwe hivi tulivyo.

Tupokee chanjo ya Covid-19 kiroho safi tu, huku tukiendelea kumuomba Mungu atuepushe na hili janga. Hamna namna wajameni.!
Bado sana
 
Kelele nyingi si muende hapo jirani tu wana chanjo. Wenzetu kibao wanaishi nchi zenye chanjo bado hawajapata lakini huku kwa wategemea misaada mnalialia sana
Ikibidi itabidi twende tu tukapate chanjo , hili gonjwa hatari maumivu yake acheni kbs.
 
Mkuu hawa wanaoipinga hii chanjo usije kushangaa wakachanjwa kabla yetu.

Usizugwe na maneno yao.

Tusishangae kupigwa kumbo wachanjwe wao kwanza.

Wengine wapinga chanjo wanasemekana tayari walishapokea yao muda tu. Hivi wao wako safi.

Nani alishafanikiwa kuwadanganya watu wote siku zote?
Kuna habari kuwa wachina wameshachanja wale wa gr1.
 
Safi kabisa mkuu. Maana kukaa na kusubiria kisichokuja ni upotevu wa muda. Mwenye uwezo anaweza kuifata popote inapotolewa

Back
Top Bottom