Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swali ni kwamba chanjo ya COVID 19 ni ipi? Kila nchi ina chanjo yake nyingine hadi 2 ambazo wanasema "zinaonyesha matokeo mazuri" chanjo zilizopo bado hazijajaribiwa Afrika kujua km hayo matokeo mazuri yatapatikana kwa hiyo viongozi wetu wapo makini hawataki tuwe sehemu ya majaribio. Mara WHO itakapokuwa na chanjo halisi kwa virusi hivyo hakuna nchi itaacha kuchanja wananchi wake, tuwe na subra.Kuna watu wanaishi kwa kuamini kila taarifa.Kwa ujumla ulimwengu wa leo unaendeshwa na habari za uzushi na uongo.Unaposikia au kuambiwa jambo lolote lazima ulichekeche. Ndio maana tukaambiwa akili za kuambiwa changanya na za kwako.
Kuhusu chanjo ya Covid-19, kuna watu tena viongozi wakubwa wa nchi wanasema eti wazungu wanataka kutuangamiza sisi ngozi nyeusi hasa Wafrika eti kupitia hii chanjo.Hiki ni kichekesho kabisa.
Wazungu waliotengeneza chanjo ya Covid-19 ndio waliotengeneza chanjo ya Polio,Kansa ya shingo ya kizazi, hadi chanjo za magonjwa ya mifugo.
Ni hawa hawa ndio wanaotutengenezea vifaa tiba na madawa ya magonjwa mengine km Malaria,Kifua kikuu,STDs,UTI, n.k. Km kweli wangekuwa na ajenda ya kutuua na kutuangamiza si wangeshafanya hivyo "a long ago" kabla ya uwepo wa kizazi chetu cha kuhoji hoji na kudadisi mambo??? Sisi tumeshindwa kutengeneza hata "tooth pick" sembuse chanjo ya Covid-19? Jamani!! Tuache mzaha beee!
Ajenda pekee ya mzungu na mataifa yaliyoendelea ni kuona Wafrika tukiendelea kuwategemea wao kwa kila kitu ili tuendelee kuwa soko kwa bidhaa zao na hatimaye waendelee kututawala. Kama kweli hatutaki kutawaliwa kibiashara na kiuchumi basi tuanze kuchukua hatua za kimkakati na sio hizi za kukurupuka.
Afrika ndio bara lenye idadi kubwa ya vijana,na idadi hii itaendelea kuongezeka muongo kwa muongo. Idadi hii ya vijana inatengeneza soko kubwa kwa bidhaa za kisasa km smartphone,Tvs,nguo, nk. Hivyo wazo la kuangamiza Waafrika ni wazo la mtu asiyejua mifumo ya kibiashara ya dunia ya leo. Kumuangamiza Mwafrika ni kuangamiza biashara ya dunia nzima.
Dunia ya leo ni vigumu kuishi ukitegemea kile unachokiamini peke ako.Tuko katika zama za kuingiliana sana. Kukataa kabisa chanjo ya Covid-19 ni kukataa biashara na wenzako na mwishowe utajikuta umetengwa "and you will suffer the consequences".
Leo hii kitu pekee wanachojivunia Korea Kaskazini ni kumiliki mabomu ya Nyuklia basi. Lakini wananchi wake wanaendelea kuishi katika umasikini wa kutupwa kwa sababu ya kuchukua misimamo mikali isiyo na tija.
Ni kweli hatutakiwi kupokea kila kitu kama jalala lakini si vema kujifanya kichwa ngumu wakati hao tunaowaletea ukaidi ndio wanaotufanya tuwe hivi tulivyo.
Tupokee chanjo ya Covid-19 kiroho safi tu, huku tukiendelea kumuomba Mungu atuepushe na hili janga. Hamna namna wajameni.!
Ndugu zetu wengi wanakufa. Taaarifa ya daki inaonyesha chanzo cha kifo ni pneumonia.Elon Musk huyu ni tajiri yeye kashasema hawezi kupata chanjo hayupo kwenye hatari ya kupata Corona
Ndugu wewe kwenye ukoo na Family yenu mmezika wangapi waliopata Corona.
Kwa nini tukilimbie chanjo wakati hatupo kwenye hatari ya kupata Corona
Niende nikachanjwe wapi wakati mzee meko kakataa kuipokea? Hata nikienda Kenya bado mm simo katika bajetiWewe tafuta chanjo, chanjwa endelea na maisha, wasiotaka waache, HUJAKATAZWA MKUU, NENDA KACHANJWE..
Hajakataa Ila alisema tujipe mudaNdugu zetu wengi wanakufa. Taaarifa ya daki inaonyesha chanzo cha kifo ni pneumonia.
Kamsikilize tena vizuri ndugu angu.Hajakataa Ila alisema tujipe muda
Kuna muda sayansi haisemi ukweli na hugeuka tatizo pia
Hajakataa Ila alisema tujipe muda
Waafrika weusi ni 15% tu ya idadi ya watu duniani, ni ushenzi kusema tuna overpopulation!
Juhudu kubwa zimekuwa zikifanywa na mataifa ya magharibi kuhakikisha idadi ya waAfrika weusi inabaki kuwa minority na hivyo oppressed zaidi duniani. Hili limefanyika kwa kusambaza magonjwa ya kuua watu wengi kwa mpigo kama 'Ebola', 'ARV na Ukimwi', Tuskegee syphilis experiment - Wikipedia...www.jamiiforums.com
Sasa kwani nimechora mimi?
Sasa kwani nimechora mimi?
Hicho ulichoquote sijaelewa, unachocheka hakieleweki, conclusion yangu ni kwamba siwezi kujadiliana na taahira."...... nimechorwa ....." 😂😂😂😂😂😂
Hii itakuja kuwa kama Yellow fever tuWewe chanjwa, wasiotaka kuchanjwa waache wafe. Wataisha mtabaki mliochanjwa.