#COVID19 Wanaoipinga chanjo ya Covid-19 ipo siku watapanga foleni kuchanjwa

Kuna tofauti kati ya kuamini sayansi na kuamini wanasayansi,tafiti za kisayansi zinafadhiliwa na wasio wanasayansi na hawafanyi hivyo kwa sababu ya kuamini sayansi.
 
Corona ni ugonjwa wa wazee kwahiyo inabidi tuwaweke lockdown wazee na sie vijana tuendelee na maisha kama kawaida,kwa kufanya hivyo tutaondoa hivi vifo vya wazee na kupunguza wingi wa wagonjwa huko hospitali.

Nasema uongo ndugu zangu?
 
Swali ni kwamba chanjo ya COVID 19 ni ipi? Kila nchi ina chanjo yake nyingine hadi 2 ambazo wanasema "zinaonyesha matokeo mazuri" chanjo zilizopo bado hazijajaribiwa Afrika kujua km hayo matokeo mazuri yatapatikana kwa hiyo viongozi wetu wapo makini hawataki tuwe sehemu ya majaribio. Mara WHO itakapokuwa na chanjo halisi kwa virusi hivyo hakuna nchi itaacha kuchanja wananchi wake, tuwe na subra.
 
Elon Musk huyu ni tajiri yeye kashasema hawezi kupata chanjo hayupo kwenye hatari ya kupata Corona

Ndugu wewe kwenye ukoo na Family yenu mmezika wangapi waliopata Corona.
Kwa nini tukilimbie chanjo wakati hatupo kwenye hatari ya kupata Corona
 
Wewe tafuta chanjo, chanjwa endelea na maisha, wasiotaka waache, HUJAKATAZWA MKUU, NENDA KACHANJWE..
 
Ndugu zetu wengi wanakufa. Taaarifa ya daki inaonyesha chanzo cha kifo ni pneumonia.
 
Wewe tafuta chanjo, chanjwa endelea na maisha, wasiotaka waache, HUJAKATAZWA MKUU, NENDA KACHANJWE..
Niende nikachanjwe wapi wakati mzee meko kakataa kuipokea? Hata nikienda Kenya bado mm simo katika bajeti
 
Hajakataa Ila alisema tujipe muda

Maneno matupu hayavunji mfupa. Kweli hajakataa?

Hivi anajua kuwa tuna janga? Janga hili linamhusu? Katamka hataki kusikia hadithi za Corona. Yeye anataka kazi tu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Corona ni ugonjwa wa wazee kwahiyo inabidi tuwaweke lockdown wazee na sie vijana tuendelee na maisha kama kawaida,kwa kufanya hivyo tutaondoa hivi vifo vya wazee na kupunguza wingi wa wagonjwa huko hospitali.

Nasema uongo ndugu zangu?
 
Wenzako walienda nje kuchanjwa na badala yake wakatuletea korona ya ajabu ajabu, hizo zinazoitwa chanjo hazina life-long immunity, itabidi uchanje kila baada ya miezi 6. Yaani makampuni ya kutengeza hiyo dawa inayoitwa chanjo yatapiga hela balaa, na watu wataendesha maisha kwa ncha ya sindano.....maisha ya kitumwa yaani.
 
"...... nimechorwa ....." πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hicho ulichoquote sijaelewa, unachocheka hakieleweki, conclusion yangu ni kwamba siwezi kujadiliana na taahira.
 
Hivi kuna mtu anapinga chanjo?, Au anashauri ipatikane iliyothibitishwa ni bora zaidi, kuliko sasa ni nyingi hata nyungu zetu tunaweza sema ni kundi la chanjo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…