Sooth
JF-Expert Member
- Apr 27, 2009
- 3,922
- 5,620
jamani hichi kitu kinanishangaza sana kwa anayejua sheria za mitala ni sahii mwalimu mwenye master kuwa lecturer wa masters?na kusisimamia thesis.yani jamaa ni wabaishaji hata kufundisha hawawezi kozi zote za master wanalalamikia walimu waswahili wenye masters wao ni ubishoo tu
- Sio sahihi kwa mhadhiri mwenye masters kuwa lecturer wa wanafunzi wa uzamili (masters). Vigezo hivi vinatumika dunia nzima. Mhadhiri wa wanafunzi wa uzamili anatakiwa angalau awe na PhD. Sababu kubwa ni kwamba, ktk ngazi ya uzamili, wanafunzi wanafundishwa misingi ya kuwa watafiti. Kwa hiyo mtu ambaye anajua misingi tu ya utafiti hawez kumfundisha mtu mwingine kuhusu utafiti. Anahitajika mtu ambaye amebobea ktk utafiti.
- Kwa mwenye masters kumsimamia mwanafunzi wa uzamili ktk tasnifu (thesis), hii ndio haikubaliki kabisa. Labda kama msimamizi msaidizi-yaan anakuwepo msimamiz mwenye PhD, halafu huyu mwenye masters anakuwa msaidizi.
- Mtu mwenye masters ni msaidizi tu wa mhadhiri (mwenye PhD), tena ktk kozi za shahada ya kwanza.
Ni kweli kwamba vyuo vyetu ni vichanga sana na hivyo kulamizika kuvipotezea baadhi ya vigezo. Lakini, tusifike mahali tukaharibu hata maana ya shahada za uzamili. Hakuna sababu ya kuanzisha programu wakati huna resources. After all, hatuzihitaji kivile hizo shahada za uzamili kiasi cha kila chuo kuanzisha MBA, MPA, M.Sc. etc.