Wanaoishambulia ACT-Wazalendo kujiunga SUK wajiulize kama CHADEMA hawajapokea ruzuku ya Novemba 2020

Wanaoishambulia ACT-Wazalendo kujiunga SUK wajiulize kama CHADEMA hawajapokea ruzuku ya Novemba 2020

Hakuna uhusiano kati ya kukubali matokeo na kuchukua ruzuku, matokeo feki ya uchaguzi yalitangazwa na NEC ya CCM, hayo hayatambuliki, pesa za ruzuku ni kodi halali wanazokatwa wananchi wa taifa hili na serikali, hivyo serikali kama wakusanyaji ni wajibu wao kuvipa ruzuku vyama vyote vinavyostahili, na hili ni takwa la sheria sio mapenzi ya CCM, narudia tena hakuna uhusiano kati ya kuyakubali matokeo na kuchukua ruzuku.
Mgao wa pesa za Ruzuku ni zao la hesabu za kura halali tulizopiga so je mnakubali matokeo na mchakato nzima kura au njaa tu inawaponza kupokea pesa haram?
 
Sawa kabisaa hujakosea, sasa hebu tueleze hilo takwa la kisheria jinsi linavyotoa haki kwa chama fulani kupata ruzuku na vingine kukosa sheria imetoa vigezo gani hapo?
Mana CUF wanapata ruzuku wakati TLP hawapati Ruzuku hili limekaaji kisheria?
Kasome hiyo sheria ndugu, hiyo sheria haijatungwa na ccm wala cdm, imetungwa na bunge ambalo mimi na wewe tunawakilishwa.
 
Umeelewa nilichoandika lakini.
Nimekuelewa vizuri tu ndio maana nikauliza hilo swali,kama ruzuku(ambayo inahusiana na uchaguzi na ndio maana vyama vyengine vinapata wengine hawapati) si hisani ya chama tawala basi na uchaguzi si hisani ya chama tawala. Sasa kama hauurambui uchaguzi na unasusia yale yanayohusiana na uchaguzi kama hizo nafasi za viti maalumu basi na ruzuku isuswe maana nayo inahusiana na uchaguzi.
 
Kwa kukusaidia tu ni kwamba ili upate ruzuku lazima ushiriki uchaguzi na upate kiasi flani cha kura ama uwe na idadi flani ya wabunge ama vyote. Cdm imekuwa second runner kwenye uchaguzi hivyo wanastahili kupata ruzuku kwa mujibu wa sheria. Na hiyo haidhinishwi na bunge, inatoka hazina moja kwa moja. Hivyo hakuna anayeulizwa kama unaitaka au hapana, ni haki inayolindwa na sheria. Kutambua matokeo ni hiyari, sio sheria. Jaribu kutumia walau 1/8 ya akili aliyokujaalia Mungu, acha kuwaza mihemko ya kisiasa muda wote.
 
Ina maana sisi wananchi ni Walevi?
Tatizo wameambukizwa uropokaji na Antipasi! Ambaye amewaacha kwenye mataa na kwenda kupokea elfu kama kumi na sita hivi kwa wiki huko Ubelgiji kisa kajisingizia ukimbizi!
 
Kwa kukusaidia tu ni kwamba ili upate ruzuku lazima ushiriki uchaguzi na upate kiasi flani cha kura ama uwe na idadi flani ya wabunge ama vyote. Cdm imekuwa second runner kwenye uchaguzi hivyo wanastahili kupata ruzuku kwa mujibu wa sheria. Na hiyo haidhinishwi na bunge, inatoka hazina moja kwa moja. Hivyo hakuna anayeulizwa kama unaitaka au hapana, ni haki inayolindwa na sheria. Kutambua matokeo ni hiyari, sio sheria. Jaribu kutumia walau 1/8 ya akili aliyokujaalia Mungu, acha kuwaza mihemko ya kisiasa muda wote.
Sasa wapi hujanielewa? Hata hizo nafasi za viti maalumu huko Bungeni ambazo zinahusiana na uchaguzi si hisani ya chama tawala, ila Chadema wamesusia ila ni haki yao kama ilivyo ruzuku. Sasa ruzuku ndio isemwe kuwa ni haki inayolindwa na sheria hivyo ni haki yao Chadema kuichukua sababu si hisani ya serikali ila ubunge pamoja na zile nafasi za viti maalumu ndio inaonekana ni hisani ya serikali si suala ambalo lipo kisheria.
 
Sasa wapi hujanielewa?hata hizo nafasi za viti maalumu huko bungeni ambazo zinahusiana na uchaguzi si hisani ya chama tawala,ila chadema wamesusia ila ni haki yao kama ilivyo ruzuku. Sasa ruzuku ndio isemwe kuwa ni haki inayolindwa na sheria hivyo ni haki yao chadema kuichukua sababu si hisani ya serikali ila ubunge pamoja na zile nafasi za viti maalumu ndio inaonekana ni hisani ya serikali si suala ambalo lipo kisheria.
Uchaguzi upi ambao unazungumzia bro! Hapakuwa na uchaguzi uhuni tu ulifanyika sasa hiyo second runner yakutokea wapi wakati hapakuwa na uchaguzi? Au ni second runner ya kupokelea Ruzuku. Tehe, tehe, CDM bana
 
Uchaguzi upi ambao unazungumzia bro! Hapakuwa na uchaguzi uhuni tu ulifanyika Sasa hiyo second runner yakutokea wapi wakati hapakuwa na uchaguzi! Au ni second runner ya kupokelea Ruzuku. Tehe, tehe, CDM bana
GAGL
 
Back
Top Bottom