Nimeshuhudia humu mitandaoni makamanda wakimshambulia sana Zitto Kabwe kufuatia chama chake kujiunga na SUK huko visiwani Zanzibar.
Kigezo ni kwamba Chadema na ACT wazalendo hawayatambui matokeo ya uchaguzi mkuu na wao wanaita "uchafuzi"
Wanachosahau makamanda wa Chadema ni kuwahoji viongozi wao kama hawajapokea ruzuku ya mwezi November kutoka serikalini.
Ikumbukwe kuwa ruzuku ni zao la kura na idadi ya wabunge na madiwani ambao chama kimepata kwenye uchaguzi mkuu.
Natumai Matola na Salary slip mtauhoji uongozi kwa niaba yetu.
Maendeleo hayana vyama!
Ruzuku sio pesa ya CCM ni pesa ya Serikali! Ni ujinga kugomea pesa ambayo wakikataa itaenda kufanyiwa ufisadi ni bora watumie hiyo pesa kutoa mokopo kwa vijana na kujenga chama. Hii haina maana misamamo imebadilika mfano inawezekana kabisa wakapata njia ya kupeleka wabunge kwa muafaka maalumu bila wenyewe kukubali matokeo ya wizi