Wanaoishambulia ACT-Wazalendo kujiunga SUK wajiulize kama CHADEMA hawajapokea ruzuku ya Novemba 2020

Wanaoishambulia ACT-Wazalendo kujiunga SUK wajiulize kama CHADEMA hawajapokea ruzuku ya Novemba 2020

Ruzuku sasa hivi yote mabillioni yanakwenda CCM.. ni muendelezo tu ya kuviminya vilivyo vyama hivi kisha kuviringishia mifupa..

Hao ACT yatari washaukimhilia mfupa tiari..njaa haina baunsa, Maalim sasa ni mwendo wa mateka.
 
Sasa mtu anakwambia Ruzuku haihusiani na uchaguzi ila wakati huo huo kuna vyama vinapata ruzuku na vyengine havipati,kama ruzuku haihusiani na huu uchaguzi ambao chadema hawautambui inakuaje sasa wao wapate ruzuku na vyama vyengine wasipate?
 
Kwenye post yako hii umetumia neno "MAMA" kwa namna ya udhalilishaji na kejeli. Labda nikushauri usirudie kutumia neno hilo kwa namna hiyo tena. Usitumie neno hilo katika mtazamo wa kudhalilisha na kutweza. Binafsi, na nina uhakika na wengine wengi wanawaheshimu sana akina MAMA kwa kuwa wao ni nguzo katika familia na jamii kwa ujumla. Hivyo wape akina mama heshima yao wanayostahili.
Achana nae huyo yeye hakuzaliwa na mwanamke na huenda wazazi wake wote ni wanaume
 
Mkuu inaoneokana kwenu hakuna wakubwa.
NB;sio kila kitu utakipata jf au Google..tafadhali keti chini na mzee wako akupe msingi wa maisha ,kulikoni kujibu jibu tu hoja ilimradi uonekane umechangia.
Google na JF inahusiana vipi na suala la kuwa Chadema ni chama cha wavuta bangi? Unatakiwa kuwa mwangalifu na lugha unayotumia katika majukwaa kama haya. Kama huna la maana la kusema jikalie kimya badala ya kuharibu jamvi kwa kurusha matusi na tuhuma ambazo huwezi kuzithibitisha.

Hilo la wazee ni kati yangu na wazee wangu, wewe halikuhusu. Na haulazimishwi kusoma kila ninachoandika.Kama unaona ninavyoandika havifai basi una uhuru wa ku report kwa moderators ili nifungiwe.

Mwisho, uwe na heshima kidogo kwa waliokuzidi umri. Nimejiunga Jambo Forum miaka 13 kabla yako. Kuna uwezekano mkubwa wakati mimi najiunga ulikuwa bado chekekea, kwa hiyo uwe na adabu kidogo.

Amandla...
 
Google na JF inahusiana vipi na suala la kuwa Chadema ni chama cha wavuta bangi?
Hilo la wazee ni kati yangu na wazee wangu., wewe halikuhusu. Na haulazimishwi kusoma kila ninachoandika.Kama unaona ninavyoandika havifai basi una uhuru wa ku report kwa moderators ili nifungiwe.

Amandla...
Hamna wa kukufungia kwa hoja zako binafsi mkuu. (Hujakiuka taratibu).
Lakni kusema kwamba hujanilazimisha kusoma hapo umekosea.. Nani aliye ni qoute kama sio wewe?? Uki qoute maanake unataka ni replay. So kama umelowa anguka miguuni nikusamehe😂😂😂😂😂😂
 
Ruzuku sasa hivi yote mabillioni yanakwenda CCM.. ni muendelezo tu ya kuviminya vilivyo vyama hivi kisha kuviringishia mifupa..

Hao ACT yatari washaukimhilia mfupa tiari..njaa haina baunsa, Maalim sasa ni mwendo wa mateka.
Kwani umewasikia Mbowe na Mnyika wakiongea ongea tena bwashee?

Huu ni wakati wa kula!
 
Hamna wa kukufungia kwa hoja zako binafsi mkuu. (Hujakiuka taratibu).
Lakni kusema kwamba hujanilazimisha kusoma hapo umekosea.. Nani aliye ni qoute kama sio wewe?? Uki qoute maanake unataka ni replay. So kama umelowa anguka miguuni nikusamehe😂😂😂😂😂😂
Na ku "quote" kwa sababu najibu hoja uliyoileta ambayo haina mashiko. Sio kwamba nataka unijibu. Unaweza kukaa kimya. Kama ambavyo mimi nitakavyokaa kimya kama uta"quote" nilichoandika maana sitakuwa na jipya la kukuelimisha.

Amandla....
 
Sasa mtu anakwambia Ruzuku haihusiani na uchaguzi ila wakati huo huo kuna vyama vinapata ruzuku na vyengine havipati,kama ruzuku haihusiani na huu uchaguzi ambao chadema hawautambui inakuaje sasa wao wapate ruzuku na vyama vyengine wasipate?
Swali zuri sana!
 
Nakuibia siri tu.

Hapa JF inaendeshwa kura ya siri ya kutafuta ni nani anaongoza kuanzisha thread za kipumbavu.

Mpaka sasa UNAONGOZA Mama.
Halafu moods wa jf wanazipenda sana mada za mapimbi hawa wa Lumumba Etwege , Yehodaya , Pascal Njaa , mada hazina kichwa wala miguu zinaachwa kwa Sababu Ni za kusifu na kuabudu ccm , weka mada critical inafutwa immediately , moods mpaka aibu mnachofanya , yamejaa ma nyuzi ya kiendawazimu kutoka lumumba kwa watajwa hapo juu kutwakucha Kama vile watu wengine wenye mawazo mbadala hawawezi kuanzisha nyuzi .
 
Nimeshuhudia humu mitandaoni makamanda wakimshambulia sana Zitto Kabwe kufuatia chama chake kujiunga na SUK huko visiwani Zanzibar.

Kigezo ni kwamba Chadema na ACT wazalendo hawayatambui matokeo ya uchaguzi mkuu na wao wanaita "uchafuzi"

Wanachosahau makamanda wa Chadema ni kuwahoji viongozi wao kama hawajapokea ruzuku ya mwezi November kutoka serikalini.

Ikumbukwe kuwa ruzuku ni zao la kura na idadi ya wabunge na madiwani ambao chama kimepata kwenye uchaguzi mkuu.

Natumai Matola na Salary slip mtauhoji uongozi kwa niaba yetu.

Maendeleo hayana vyama!
Bila kuathiri msimamo wangu wa kutoshabikia vyama vya siasa, naomba kukukumbusha kuwa Ruzuku wanayopokea vyama vya siasa sio hisani ya chama tawala, ni takwa la kisheria, lakini kubwa zaidi ruzuku ni kodi ya watanzania sio fedha inayotokana na michango ya chama tawala. PERIOD.
 
Nimesoma comments zote kutoka page 1 hadi hii ya 6 ajabu sijaona yeyote aliye kuja kujibu hoja zaidi ya matusi na kejeli tu.

Hii inatoa dalili kwamba hii hoja ni ngumu sana kujibika ndio mana matusi yanatawala.
 
Bila kuathiri msimamo wangu wa kutoshabikia vyama vya siasa, naomba kukukumbusha kuwa Ruzuku wanayopokea vyama vya siasa sio hisani ya chama tawala, ni takwa la kisheria, lakini kubwa zaidi ruzuku ni kodi ya watanzania sio fedha inayotokana na michango ya chama tawala. PERIOD.
Sasa mbona Chadema wanapewa ruzuku na Nccr mageuzi haipati?!!
 
Back
Top Bottom