MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Hizi propaganda zisizo na maana zenye malengo ya kuvuruga soka la Tanzania linapaswa kupingwa na kukemewa vikali. Hakuna mzee wa Yanga mwenye akili timamu, akatoa pesa mfukoni, maana kufungua na kuendesha kesi inahitaji nguvu ya mwili na pesa, Ukiachilia mbali mafanikio yaliyopatikana ndani ya Yanga kutoka club namba 79 kwa ubora Afrika mpaka namba 9 ndani ya muda mfupi, mtu mwenye akili timamu atumie gharama zake, muda wake, nguvu zake kwenda kupingana na mafanikio hayo! Kichwani akijua kabisa kwamba hakuna asiyemtaka Hersi kusalia Yanga! Jeuri hii inatokea wapi? Nguvu hii inatokea wapi? Pesa hii inatokea wapi? Ni muda wa wanayanga kuwa Imara na kukemea ikibidi kuwafuta uanachama baadhi ya mamluki wanaoonyesha kupokea hongo ili kuhujumu timu.
#DaimaMbele #NyumaMwiko
#DaimaMbele #NyumaMwiko