zaza1
Member
- Jun 28, 2018
- 60
- 50
Kauli ya Naibu Waziri Mhe. Regina Ndege Qwaray kwamba wanaojitolea wanapendelewa huku akisema kujitoa sio kigezo cha ajira, ni kauli inayokera na inayokosa uhalisia. Ukweli ni mmoja: hii ni tafsiri yake binafsi — akili yake — sio hali halisi inayowaumiza maelfu ya vijana.
Kama kweli wanaojitolea wanapendelewa, basi waelezwe hawa vijana waliokaa taasisi za umma miaka 3, 5, hadi 10 bila ajira, wakifanya kazi nzito bila mshahara wala hatima. Upendeleo uko wapi? Au upendeleo uko kwenye karatasi za ofisini tu?
Hii kauli inaonyesha wazi mtengano mkubwa kati ya viongozi na uhalisia wa wananchi. Walioko juu wanaongea kwa nadharia, walioko chini wanaishi maumivu. Ni rahisi kusema “wanapendelewa” ukiwa hujawahi kusota kwenye kujitolea bila uhakika wa kesho.
Na tusidanganyane:
Mfumo unaoitwa rasmi wa ajira nao umeoza. Vimemo, ndugu, marafiki, na hata ongo vimekuwa siri ya wazi. Kama mfumo huo ni safi na wa haki, kwa nini malalamiko haya hayakomi? Au haki ipo kwa wasiokuwa na sauti tu?
Swali gumu lakini la lazima kuuliza:
Kwa nini watoto wa vigogo na viongozi wakubwa hawapiti huo huo mfumo “rasmi” unaosifiwa?
Kwa nini wao hupenya bila jasho, wakati mtoto wa maskini anapimwa hadi pumzi ya mwisho?
Cha kushangaza zaidi, wengi wanaopitia mfumo huo rasmi hawatoi tija inayolingana na nafasi walizopewa. Hakuna uwajibikaji, hakuna moyo wa kazi, hakuna ufanisi. Lakini vijana waliokuwa wakijitolea kwa bidii na uzalendo wanaambiwa “kujitoa sio kigezo”. Huu ni uonevu wa kimfumo.
Na tukumbuke hili pia:
kuteuliwa kuwa naibu waziri hakumaanishi mtu ana akili au maono kuliko Watanzania wengine wote.
Ni uteuzi wa kisiasa, sio cheti cha hekima.
Kwa hali hii, ni wazi kwamba Rais ana kazi kubwa ya kufanya tathmini upya ya viongozi wake, na inapobidi kufanya mabadiliko kwa kuweka naibu waziri mwenye maono, anayesikiliza sauti za walioko chini, si yule anayepamba mfumo ulioshindikana.
Watanzania hawapigi kelele kwa sababu ya uvivu.
Wanapiga kelele kwa sababu wamechoka kudharauliwa kwa kauli za kufariji zisizo na ukweli.
Mfumo wa ajira una tatizo — na kulikana ndiko kunakofanya liendelee kuoza.