Katika Jiji la Mwanza eneo la Mkuyuni karibu na Nyegezi Kona, kuna kundi la Watu wanajitambulisha kuwa ni Askari Polisi wakiwa hawana sare wala vitambulisho wanakamata Pikipiki (bodaboda) zisizokuwa na Namba (plate Number) na kuwapeleka wahusika ofisini kwao.
Wanazifunga kwa cheni na kufuli, wanawatoza faini waendesha pikipiki (Sh 5000 hadi 30,000), pesa ambazo haifahamiki wanafikisha Serikalini au wanazitumia vipi. Hili linaweza kuwa mwanya wa masuala ya utekaji yanayoendelea hapa nchini au rushwa.
Swali, ni mamlaka ipi imewapa hawa watu leseni/kibali cha kuendesha shughuli hizo, je ni kweli kwamba Jeshi la Polisi limeshindwa kudeal na Bodaboda wasiokuwa na namba, kiasi kwamba hawa watu wameona gape au ni njia za utapeli mpya?