Wanaokandia ongezeko la Wachina hawajui dunia inakoelekea. Hiyo ndio Globalization, ni mafuriko

Hili swala naona kama lina ongerewa kishabiki na chuki. Nafikiria watalaamu waangalia athari za kiuchumi kwa nchi.
Maana hawa watu wa nchi zingine wanaweza kuondoka na mzungoko wa fedha zetu watakapo amua kuondoka.
 
1.mchina atumii loophole sana, mchina anajua how goverment officials are so corrupt, even wakivunja hizo laws ni wazito kufuatilia. Results: mtanzania mpaka apate shida , ndio wazinduke kutoka usingizini

2 Kulingana na ufahamu wangu (si expert sana) but hizii ni baadhi ya restricted bussiness for foreigners hapa tz :

-Uzaji mdogo na biashara ndogo: Hii inajumuisha kuendesha maduka madogo, vibanda, na kujihusisha na biashara ndogondogo. Lengo ni kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wa Kitanzania.
-Uzaji wa bidhaa kwa kupita mitaani na kuuza kwenye vibanda vya barabarani: Shughuli hizi kwa ujumla zimehifadhiwa kwa raia wa Tanzania.
-Saluni za kinyozi na urembo za jadi: Uendeshaji mdogo katika sekta hii mara nyingi umehifadhiwa.
-Machinjio yanayohudumia jamii za mitaani: Maduka madogo ya nyama yanayohudumia mitaa ya karibu yanaweza kuwa na vizuizi.
-Kuendesha taxi na huduma za usafiri wa ndani: Sekta hii mara nyingi ina vizuizi kwa ushiriki wa watu binafsi kutoka nchi za nje ili kusaidia madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri wa ndani.
-Ukulima mdogo na shughuli za kilimo: Baadhi ya sehemu za uzalishaji wa msingi wa kilimo, hasa kwa kiwango kidogo, zinaweza kuwa zimehifadhiwa kwa raia wa Tanzania.
-Uchimbaji mdogo wa madini: Shughuli ndogo za uchimbaji madini mara nyingi zimezuiliwa kwa raia wa nje.
-Biashara zinazohusika na uuzaji wa moja kwa moja wa sanaa na kazi za mikono za kitamaduni: Ili kusaidia wasanii na mafundi wa ndani, sekta hii inaweza kuwa na vizuizi.

But kuna exception
Mfano : Watu binafsi kutoka nchi za nje mara nyingi wanaweza kushiriki katika sekta hizi kupitia ubia au ushirikiano na raia au kampuni za Tanzania, ambapo mshirika wa Tanzania anamiliki hisa
Vizuizi mara nyingi hutumika kwa shughuli ndogo. Uwekezaji mkubwa zaidi kutoka nchi za nje unaweza kuruhusiwa katika baadhi ya sekta hizi, hasa ikiwa unaleta mtaji mkubwa, uhamishaji wa teknolojia, na fursa za ajira.


3. Ni mfano an ni actual thing umeelezea?
 
Hii ni new case aisee, dar wanalalamika watu wa kaskazini ni wageni? 🤣🤣🤣
 
Umemshambulia jamaa bure kumbe wewe ndo huna kabisa exposure. Kuna wabongo kibao wana biashara China hasa hiyo ya migahawa. Achana na stori za vijiweni. Uhalisia hauko hivyo. Tuache uoga
 
Pwenti!
Hata watz wapo ambao wanafanya kazi za ovyo kwenye nchi nyingine, kazi ambazo pengine ni za wazawa wa hizo nchi.
 
Wewe ni kiazi kweli, uliyeshiba magimbi.

TZ ina historia ya ujamaa na watu wamelelewa kwenye misingi hiyo.

TZ wala hawamiliki vitu, ndio maana hata ardhi bado ni mali ya umma.

Katika taifa la aina hiyo, ukiruhusu zig zag watu waje Watanzania watapoteza kila kitu.


Tanzania bado serikali inalipa mshahara wa laki 3 ( $150). Mafao mtu kafanya kazi miaka 30 hafikishi milioni 100.

Ulaya na China watu wanalipwa Tsh 40,000 kwa saa, na pension za zaidi ya billion.

Watu wa aina hii, wewe kiazi huwezi kushindana nao.

Watakuja na pesa zao ambazo wewe huna, watakuwa na uwezo wa kulipa bei za vitu, kwa bei kubwa (kwao ni pesa kidogo).

Mfano: Kiwanja ambacho wewe ungeweza kununua kwa milioni 5 ukajenga kibanda chako na wanao, wao watakuwa na uweso wa kugoa milionin 30 bila shida, na wewe huwezi kununua.

Nenxeni hata hapo Kenya mkajifunze maisha ya kibepari.

Msione Nyerere alikuwa mjinga.


Ndani ya miaka 5, mtajikuta Wazungu, Wachina, Waarabu na wahindi wanamiliki nchi yote, halafu mmepangishwa mnazeekea kwenye apartments mnalimishwa kwenye mashamba yao makubwa ya Cocoa, Kahawa, Mbaazi, Ifuta, na Parachichi kwa ujira wa kula na kodi.

Nchi ulizotolea mifano, zilikuwa za kibepari kama Kenya, walishagawana kila kitu, kwahiyo leo wakiruhusu watu kuja, ukiuza ardhi ni mali yako.

TZ hakuna kitu cha mtu.

Ni sawa na mtu asiye na mazoezi kumweka ukumbi wa mapigano na Bondia Kiduku.
 
Nakubaliana na hoja kuwa tunaishi katika dunia ya utandawazi, na kwamba watu kutoka mataifa mbalimbali wanapambana kutafuta riziki popote wanapoweza. Lakini pia ni muhimu kuelewa kuwa hoja ya watu kuhofia wachina sio tu kuhusu uwepo wao, bali ni athari zao kwenye biashara za wazawa na ushindani usio wa haki kutokana na mitaji yao mikubwa na fursa wanazopata.


Kuhusu suluhisho:
✅ Elimu bora ni jambo la msingi kabisa, kwani itawezesha Watanzania kushindana kwa ujuzi na ubunifu.
✅ Serikali pia inapaswa kuhakikisha kuwa kuna mazingira mazuri ya biashara kwa wazawa ili waweze kushindana kwa haki.
✅ Watanzania wanapaswa kubadilika kiakili na kimtazamo – dunia imebadilika, na wenye akili za kizamani wataachwa nyuma.


Kwa kifupi, badala ya kulalamika tu, ni vyema tukawekeza katika kujifunza, kubadilika na kushindana kwa kutumia maarifa badala ya kulalamikia hali iliyopo. 💪🔥
 
Vipi mkuu huko china na sisi tunaruhusiwa ?
 
Mlivyo mazuzu baada ya miaka 5.

Wacjina, Wahindi, Waarabu, Wazungu watakuwa wanakaa Masaki, Mikocheni na sehemu nyingine zote.

Halafu watawapangisha nyie mtakuwa kama mazuzu mnawalimia kwenye mashamba makubwa ya Chai, Kahawa, Mkonge, Cocoa etc


Narudia tena, hata kushindana na Wakenya hamna uwezo kwasababu miakili yenu imejaa giza ila wakenya wameshajeruhiwa.



View: https://youtube.com/shorts/mY2A2dpDHqM?si=b1-Ed481yAPe8RB9
 
Kuna pande mbili moja nadhani hao wengi wanaofanya hizo kazi kosa lao sio kufanya hizo kazi bali huenda hawana kibali cha kuwepo nchini na kufanya hizo kazi unless ni raia ambao huenda wazazi wao walikuja na sio wao kuja kufanya hizo kazi per se...

Mbili ni upuuzi kungangania hizi kazi za uchuuzi kwamba ndio zetu wakati tunawaachia watu uchumi wa nchi na commanding heights ili ndio watufanyie eti tugawane faida... (Kwahio badala ya kuhangaika na wachina kariakoo pia tuangalie kuna DP World Bandarini au Adani tunaotaka kuwapa Tanesco kutengeneza miundombinu ili tugawane jasho letu to infinity)

Tatu inabidi tuangalie mwisho wa siku tunataka nini na ili iweje je tunataka watu wapate faida kwa kufanya so called shughuli (hata kama mwisho wa siku ni for the detriment ya wengine) yaani gharama ya manunuzi kutokana na ulanguzi AU Tunataka mtu wa mwisho apate product as cheap as possible ?

Sababu kama issue ni gharama ya Kodi ambazo mchina halipi na ukizingatia sio kwamba tunalinda viwanda vya ndani (ambavyo havipo) basi huenda tujiulize hizo Kodi tunazolipa kubwa hata zinafanya nini....

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…