Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 471
- 1,217
Mara nyingi maadui zetu wakubwa hawaji na panga na bunduki. Wanakuja na tabasamu, na mikono ya kukumbatia.
Yule unayemwamini hadi unampa siri zako za moyoni ndiye anayeweza kukuchoma kisu mgongoni bila wewe kujua.
Kuamini ni kuzuri, lakini kuamini bila akili ni kujitengenezea kaburi lako mwenyewe.
Msemo huu unauma kwa sababu ni ukweli mtupu. Watu tunaowaruhusu karibu na mioyo yetu ndio wenye silaha kali zaidi za kutuumiza.
Kwa nini hasa?
1.Ukaribu hutoa ufunguo.
Adui wa nje hawezi kuingia ndani ya ngome yako. Lakini yule unayemwamini, unampa mwenyewe ramani ya kuingia anajua udhaifu wako, siri zako, na hofu zako. Ukigeuka, anajua pa kupiga ili paume zaidi.
2.Uaminifu kipofu ni hatari.
Kuamini ni jambo jema na msingi wa mahusiano yote Ila kuamini bila kujipa shaka yoyote ni kujifunga macho
3.Usaliti haunuki.
Maadui wa kweli hawakwambii "naja kukudhuru". Wanakuja na tabasamu, na maneno matamu, na ahadi. Wanakuwa bega la kulia mpaka siku moja utakaposhtuka umebaki peke yako na jeraha mgongoni.
Somo kuu.
Kuwa na macho mawili hata kwa wale unaowapenda. Penda, amini, jenga mahusiano - lakini usiuwe ubongo wako. Chunguza matendo, si maneno. Mpe mtu muda kuthibitisha uaminifu wake kabla hujampa funguo zote za moyo wako.
Kuwa mpole kama njiwa, lakini mwerevu kama nyoka.
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Malenga wa Kiha