Wanaokula mnofu wa Tanzania

Tatizo hao ndio wenye maamuzi kwahiyo wakifanya amendment lazima wajiangalie wao ,ndio maana hata katiba mpya ilikwama kwasababu ingeenda kuwaumiza hadi wao ,ebu fikiria mbunge amekaa bungeni miaka 20 halafu aje apitishe kipengele cha ukomo wa ubunge vipindi vi3 ,je atapitisha?
 
kwa nini na hizo kada zingine wasipewe allowance ambazo ni non taxable kama hao wachumia tumbo? inavyoonekana watu muhimu kwa jamii wanadharaulika saaaana kuliko hao wachumia tumbo ambao wakichaguliwa wanabadilika na kujiona ni ma intellectual ambao wengi ni magumashi na wamefoji vyeti. Jaribu kuangalia mishahara na marupurupu kwa nchi wanaojitambua utaona wanalipana kutokana na umuhimu wa kada kwa jamii.
 
Daah hapo umesema kweli lazima wajipendelee wao
 
Usisahau kwamba hiyo fedha anagawana na wajumbe.....
ole wake aile pekeyake
 
Dawa yahaya yote CCM kuondolewa madarakani..
 
haya maisha bhana! mtu kasota kutafuta degree lakn anakuja kutungiwa sheria na mtu ambae et "anajua kusoma na kuandka"

hii ishu ya mbunge kujua kusoma na kuandka iliwekwa enz hzo wakat tanzania ikiwa haina wasomi wa kutosha lakn sasa nchi ina wasomi kila kona kwa nn vigezo vya mtu kuwa mbunge visibadilishwe? mm napendekeza mtu kuwa mbunge angalau awe na degree moja.
 
Mi naona sababu kubwa ya walimu kudharuliwa hata kwenye malipo inaanzia na mfumo wetu wa elimu...leo hii kusoma ualimu ambao ndo msingi wa taifa wala sio kazi ukiwa na ufaulu hata wa D 4 tu unaweza soma kuanzia vidudu kwrnda juu...sasa fikiria kama mwalimu ana elimu duni unadhani kuna mtu atawathamini?

Iweke sheria labda ualimu,udaktari,nurse,maabara na kada zote za afya na uhandisi,uchumi mtu anayetaka kusoma walau awe na Division one..hapo kila mtu ataheshimu.. na structure nzima ya jinsi wanavyopatikana kuanzia shuleni hadi kwenye ajira ibadilike nina amini muda mfupi tu nchi itapaa..tofauti na sasa ualimu imekua kama vile option ya mwisho kwa mtu aliyefeli
 
Madiwani pekee wangetosha kua wawakilishi wa wananchi na ingewekwa sheria mtu awe na angalau digrii ya fani flani ingesaidia pamoja na mengineyo kama historia yake ya nyuma kuhusu nidhamu nk..pia ukomo uwe 10yrs
 
Kuna wengine hawajagombea. Wameteuliwa, viti maalum na wamepitwa bila kupingwa.
Wamepita bila kupingwa au bila kupigiwa kura🤩?

Nilichojifunza katika haya maisha ya hapa town jitahidi sana kukaa jirani na ma bigfish. Ndio namna pekee na rahisi ya kufikia matobo!
 
Basi itasaidia kama Halmashauri itawanunulia furniture sawa na wafanyakazi wengine, itawalipa maderva na makatibu etc yeye akabaki na pesa zake ili basi hizo zingine zisaidie na jamii yake hiyo; pendekezo
 
Wamepita bila kupingwa au bila kupigiwa kura🤩?

Nilichojifunza katika haya maisha ya hapa town jitahidi sana kukaa jirani na ma bigfish. Ndio namna pekee na rahisi ya kufikia matobo!
Nadhani viti maalumu inaushindani sana kuliko hata ule wa jimbo...Usije dhani wameteuliwa
 
Daah! Bora niendelee na business zangu tu 🚶🚶🚶
 
Basi itasaidia kama Halmashauri itawanunulia furniture sawa na wafanyakazi wengine, itawalipa maderva na makatibu etc yeye akabaki na pesa zake ili basi hizo zingine zisaidie na jamii yake hiyo; pendekezo
Haitotokea iwezekane ,siasa zetu chafusana.Mimi mbunge serikali initaftie dereva?.katibu wangu jimbo, au ofisi ya bunge initaftie dereva,katibu!!!! Mbona sikumbili utaenda na maji
 
Haitotokea iwezekane ,siasa zetu chafusana.Mimi mbunge serikali initaftie dereva?.katibu wangu jimbo, au ofisi ya bunge initaftie dereva,katibu!!!! Mbona sikumbili utaenda na maji
Unatafuta wewe ila malipo yafuate scheme na mifumo ya serikali...Hii itasaidia sana kuondoa hizo biases na psychological problems wanazopata technochrats
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…