Wanaokwenda jela si wote wana hatia, hata wewe kesho unaweza kuwa mfungwa

Wanaokwenda jela si wote wana hatia, hata wewe kesho unaweza kuwa mfungwa

Hivi mtu uzingatie mambo gani! Ili kuepukana na makosa yanayoweza kukupeleka jera?

Kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kuzingatia ili kuepukana na makosa ya jinai na kujiepusha na hatari ya kufungwa gerezani:​

  1. Kuzingatia sheria: Kuheshimu sheria na kuzingatia kanuni na taratibu zinazotolewa na serikali na taasisi nyingine ni muhimu sana. Kwa kufanya hivyo, unaweza kuepuka kufanya vitendo ambavyo vinaweza kukuletea matatizo na hatari ya kufungwa gerezani.
  2. Kutotenda makosa: Kuepuka kufanya makosa ya aina yoyote, iwe ni makosa madogo au makubwa, ni muhimu sana. Kwa kufanya hivyo, utapunguza hatari ya kuhukumiwa kwa makosa ya jinai na kufungwa gerezani.
  3. Kuepuka kutumia madawa ya kulevya: Kutumia au kuuza madawa ya kulevya ni kosa la jinai ambalo linaweza kukuletea matatizo makubwa na hatari ya kufungwa gerezani. Kuepuka kutumia madawa ya kulevya ni muhimu sana kwa afya yako na pia kwa usalama wako.
  4. Kutotenda vitendo vya udanganyifu: Kutenda vitendo vya udanganyifu, ikiwa ni pamoja na kughushi, kutoa taarifa za uwongo, na kuficha ukweli ni kosa la jinai. Kuepuka kutenda vitendo hivi ni muhimu sana ili kuepuka hatari ya kufungwa gerezani.
  5. Kufuata maadili na kanuni: Kufuata maadili na kanuni katika maisha yako ya kila siku ni muhimu sana. Kwa kufanya hivyo, utakuwa na uwezo wa kuepuka hatari ya kufanya vitendo ambavyo vinaweza kukuletea matatizo na hatari ya kufungwa gerezani.
Kwa ujumla, kuepuka makosa ya jinai ni suala muhimu sana katika maisha ya kila siku. Kwa kuzingatia sheria, kutotenda makosa, kuepuka kutumia madawa ya kulevya, kutotenda vitendo vya udanganyifu, na kufuata maadili na kanuni, utapunguza hatari ya kufungwa gerezani na kuishi maisha huru na salama.
 
Unaongelea 2020 wakati kuna watu wana kesi za 2010 Mahakama haina bajeti ya kukaa vikao
 
Chakula wanacholima(ga) kinakwenda(ga) wapi? Au hakitoshi?

Na Sheria unataka wafungwa wale kwa tabu au ni uchumi wetu mdogo?
Mkuu chochote kinachozalishwa na serikali hakiliwi kwa mtindo wa kaya!

Yaani ukalime uvunje hindi na kulichoma bila process!

Hawawezi kukila wanachokizalisha mpaka kiingizwe kwenye mfumo wa manunuzi ama tenda(zabuni).

Kwa mtindo huo, wawezakuta unachokizalisha wewe, usipate kukitumia maisha yako yote na ukaendelea kutumia usivyovizalisha!

Kuna sehemu sijaeleweka mkuu?
 
Hakuna anaejua siku yake ya kesho itakuwa vipi, lolote laweza kutokea uwe muhalifu ama sio mhalifu waweza kujikuta umeingia rasmi 18 za kwenda gerezani.

Wiki iliyopita nilienda mtembelea rafiki gerezani, yupo kwa takribani mwezi sasa kosa likiwa kununua simu kwenye magroup haya ya whatsapp, iliyoibiwa, simu aliyonunua kumbe ilikuwa ya wizi, kapewa kesi ya unyang'anyi kwa kutumia silaha, nilivyomkuta machozi yalinilenga. Ni mwezi kakaa lakini hali niliyomkuta nayo inasikitisha.

Mlo mmoja kwa siku tena ugal mkubwa ila mboga sasa unakuta majan yakunde yalokomaa maharage manne mchuzi pipa

Kuoga kwa folen

Kujisaidia kwa folen tena waziwazi kabsa wenzio wanakuona

Kulala sa kumi jioni,

Godoro kuu kuu zimeoza kwa jasho

Chumba kimoja wafungwa 50 mpk 60

Hakuna simu wala mawasliano ya aina yoyote

Kazi ni amri ni lazima kufanya

Ukiugua dawa za shida yan

Kwa upande wa mahabusu wanapoingizwa pale kwa mara ya kwanza huamini kuwa watatoka soon ila siku huwa wiki, wiki huwa mwezi, mwezi huwa miaka, wapo mahabusu kibao tangu 2020 kesi hazijasikilizwa

Epuka sana mambo ya madawa ya kulevya , wizi (ikiwemo kununua vya wizi), ujangili, kutembea na wanafunzi wa shule kike, n.k, hizi kesi ndio zina sotesha sana watu gerezani

Kama unadhani jela ni shule mpeleke mwanao, sio kuzuri hata kidogo
Amina
 
Mkuu chochote kinachozalishwa na serikali hakiliwi kwa mtindo wa kaya!

Yaani ukalime uvunje hindi na kulichoma bila process!

Hawawezi kukila wanachokizalisha mpaka kiingizwe kwenye mfumo wa manunuzi ama tenda(zabuni).

Kwa mtindo huo, wawezakuta unachokizalisha wewe, usipate kukitumia maisha yako yote na ukaendelea kutumia usivyovizalisha!

Kuna sehemu sijaeleweka mkuu?
Hiyo para ya 3. Kwamba magereza ya Kihoma yasile chakula chenye mawese bali alizeti na wa Singida wale mawese?

Pia inaingizwaje katika mfumo wa tenda?
 
Back
Top Bottom