Wanaolalamikia 'SINGO MAZA' wasipuuzwe. WANA HOJA

Andiko nzuri sana na lenye hoja za maana, hongera sana.

Ukweli malezi sio mepesi , garama za malezi si nyepesi haijalishi una kipato cha namna gani..
Kwetu wanaume hatujali tunagharamika kiasi gani kutoa mahitaji kwa watoto wetu kwani ndani yetu tunajihesabu kama sehemu ya uanaume wetu, kwa lugha rahisi tumejitoa sadaka bila kujali maisha yetu kwa ujumla kwa ajili ya famili, hii iko ndani mwetu .

Binafsi napata shida sana ninapo ona mwanamke anae itwa single mother akibezwa , tena akibezwa na mwanaume .

Naweza nisiwe sahihi lakini huwa naamini anguko lolote la mwanamke ni matokeo ya kufeli mwanaume .

Mwanaume anapo shindwa kusimama kama mwanaume athari zinajidhirisha kwa mwanamke na kisha kulaumiwa mwanamke!

Mapendekezo yako mleta mada ni mazri na yanayo paswa kuungwa mkono. Zinahitaka juhudi za lazima kupunguza hiki kinacho itwa single mother, ikibidi hata mamlaka .

nini kifanyike kwa mwaname kupunguza matokeo ya single mother?
kwanza kabisa ni mwanamke mwenyewe, mwanamke kwa sababu ana wajibu na mwili wake mwenyewe.
kwa sababu pia mwanamke hafanyi mapenzi bila sababu, hana msukumo wa kufanya mapenzi unaolingana mwanaume kwa hio ana uwezo mkubwa wa kupunguza kama si kuuondisha kabisa unao itwa usingle mother.

bahati mbaya pamoja na dharura tunarudi pale kwenye mapendekezo yako.

shukrani.
 
To yeye my love hope you gud.

Umesoma uzi wote kweli love?
SIjakuelewa vizuri ila nimeweka wazi kuwa sio singo maza wote na pia mimi mimi pia nilikua singo maza hivyo mateso nayajua na siwezi kunyooshea/hukumu anayeteseka na ulezi peke yake.
Mkuu
Sasa Hivi Umeongeza Mtoto Mwingine ?💘💞💕❣️
 
Ila kuna wanaume wapumbavu sana hii dunia. Kuna jamaa lilitelekeza meneja likakimbilia kwa mchepuko. Sasa naye anaitwa singo maza jamani, hovyo kabisa! Almanusura nimvagae!
Lilitelekeza meneja kivipi mkuu?
 
Umeongea point nyingi sana
 
Nimesoma andiko lako lote na nakubaliana na sehemu moja tu: kulea mtoto peke yako ni jambo gumu sana na linaweza kuleta msongo mkubwa wa mawazo. Lakini hapo ndipo ninapoona hoja yako inaanza kupoteza mwelekeo.

Unasema single mothers ni tatizo katika jamii, lakini katika andiko lote umeeleza madhara ya kulea mtoto peke yako bila msaada wa baba. Swali la msingi ni: kwa nini lawama nyingi ziende kwa anayebaki kubeba jukumu, na si kwa anayeliacha?

Kama single motherhood inaleta uchungu, msongo, hasira na changamoto za malezi kama ulivyoeleza, basi wanaume wanaokwepa wajibu wa malezi ni sehemu ya tatizo hilo pia. Haiwezekani kuzungumzia matokeo huku ukipuuza chanzo chake.

Mtoto hutokana na watu wawili. Hivyo kuwepo kwa single mother si ushahidi wa kushindwa kwa mwanamke peke yake, bali mara nyingi ni matokeo ya maamuzi, makosa au mazingira yanayowahusisha watu wawili.

Kwa mantiki hiyo, mjadala haupaswi kuwa "kwa nini kuna single mothers?" bali pia "kwa nini kuna wanaume wengi wanaowaacha wanawake walee watoto peke yao?"
Ukijibu swali la pili kwa uaminifu, utaona kuwa tatizo ni kubwa kuliko kundi la single mothers pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…