Nimesoma andiko lako lote na nakubaliana na sehemu moja tu: kulea mtoto peke yako ni jambo gumu sana na linaweza kuleta msongo mkubwa wa mawazo. Lakini hapo ndipo ninapoona hoja yako inaanza kupoteza mwelekeo.
Unasema single mothers ni tatizo katika jamii, lakini katika andiko lote umeeleza madhara ya kulea mtoto peke yako bila msaada wa baba. Swali la msingi ni: kwa nini lawama nyingi ziende kwa anayebaki kubeba jukumu, na si kwa anayeliacha?
Kama single motherhood inaleta uchungu, msongo, hasira na changamoto za malezi kama ulivyoeleza, basi wanaume wanaokwepa wajibu wa malezi ni sehemu ya tatizo hilo pia. Haiwezekani kuzungumzia matokeo huku ukipuuza chanzo chake.
Mtoto hutokana na watu wawili. Hivyo kuwepo kwa single mother si ushahidi wa kushindwa kwa mwanamke peke yake, bali mara nyingi ni matokeo ya maamuzi, makosa au mazingira yanayowahusisha watu wawili.
Kwa mantiki hiyo, mjadala haupaswi kuwa "kwa nini kuna single mothers?" bali pia "kwa nini kuna wanaume wengi wanaowaacha wanawake walee watoto peke yao?"
Ukijibu swali la pili kwa uaminifu, utaona kuwa tatizo ni kubwa kuliko kundi la single mothers pekee.