Wanaolilia legacy ya Hayati Magufuli someni alichoandika Bollen Ngetti

Wanaolilia legacy ya Hayati Magufuli someni alichoandika Bollen Ngetti

Nawasalimu wanabodi. Hili andiko ameandika Mwandishi Bollen Ngetti katika ukurasa wake wa Facebook. Nami nalisukuma kwenu nzima nzima bila ku-edit.
______________________

KULILIA LEGACY YA MAGUFULI NI UJINGA

Na Bollen Ngetti

INACHEFUA sana na kutia kinyaa kuona, kusoma au kusikia watu wazima ndani na nje ya Bunge wakipiga mayowe eti Watanzania wanapaswa kuenzi "legacy" ya Hayati John Magufuli. Inafedhehesha sana.

Baadhi ya hao wanaoigiza "kidali poo" mchezo wa watoto wanalalamika eti kuna watu wanasifia utawala mpya wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa shabaha ya kuzika na kufuta "legacy" ya Magufuli. Utopia.

Kinachotoa matumaini ni kwamba wengi wao ni kina Mulaga ambao kwao elimu Darasa la Saba ndio PhD katika kijiji kizima. Aibu ilioje!

Ndugu zangu, HAKUNA "legacy" YOYOTE aliyoacha John Magufuli, Jakaya Kikwete, Benjamin Mkapa, Alli Hassan Mwinyi na nina mashaka hata Samia Hassan asipojifunza kwa watangulizi wake naye hatoacha "legacy" yoyote. Naye atapita tu kama upepo pamoja na kwamba mimi ni miongoni mwa wanaomuunga mkono 100% kwa gia aliyoanza nayo.

Tusitumie vibaya neno "legacy" na kuichanganya na kumbukumbu "memory". Tunakosea.

Legacy haijengwi kwenye vitu na matendo (actions). Kujenga daraja la Mfugale na Busisi si "legacy". Hizo ni kumbukumbu tu. Legacy hujengwa katika mawazo (ideas).

Mbunge wa Temeke Masumbuko Lamwai alipojenga daraja la Manzese linalopita juu, Dar ilizizima kuona watu wanaweza kuvuka barabara kwa kupita juu!? Ulikuwa ni "Utalii". Lamwai hakuacha "legacy" bali "memory" maana Ubungo Interchange imeifuta. Kesho kutwa tutajenga barabara ya juu kutoka Ubungo hadi Kibaha. Hutolikumbuka Ubungo Interchange tena.

Magufuli kusimamia ujenzi wà SGR, Bwawa la Nyerere, Elimu "bure", ununuzi wa ndege nakadhalika. Yote hayo ni "memories".

Mwalimu Nyerere alipoanzisha siasa ya Ujamaa, Azimio la Arusha. Alijenga "idea" ndani ya vichwa vya Watanzania. Mwl ameacha "legacy" inayoishi. Wapo viongozi wengi duniani walioacha "legacy" kwa kuasisi "ideas" ambayo inaishi. Yesu na Mtume SAW waliacha "legacy" si "memory".

Tatizo la viongozi wetu (sitegemea SSH naye ataangukia humo) huongozwa kwa kauli mbiu zisizo na falsafa. Uwezo wao wa kuona na kufikiri ufikia ukomo na umbali wa miaka mitano hadi kumi. Ukisikia kiongozi anasema, "sitoi chakula cha bure utawala wangu subirini nitoke" huyo hana maono, hawezi kuacha legacy but memory.

Laiti tungezijengea falsafa kauli mbiu hizi kwa kuona Tanzania ya miaka 50, 100 hadi 200 tungepiga hatua kubwa. Labda Samia atakaribu lakini naye hatujui falsafa ya kauli mbiu "Kazii iendelee" .

Jakaya alikuja na Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya pamoja na Maisha Bora kwa Kila Mtanzania. Hakuna maono, hipita kama upepo.

Mkapa "uwazi na ukweli" ikageuka "uficho na uongo". Mwinyi "ruksa na fagio la chuma" ikawa fagio la pamba. Ni kana kwamba wanashindana kuwafukarisha wananchi wenzao.

Tunapolinganishwa na baadhi ya nchi tuliokuwa nao pamoja miaka ya 60 na leo wamepiga hatua utakuta walikuwa na visheni kali iliyojengwa na falsafa.

Kwa Marekani mfano: huwezi kuwa Raia bila kwanza kuandika kitabu au makala kadhaa kuonesha watu nini falsafa yako kasoro Donald Trump. Sisi tunaandika vitabu baada ya kustaafu isiyotusaidia kitu.

Nimeomba kuonana na Raia Samia nimuulize nini falsafa yake inisaidie kuandika kitabu ninachoandika juu yake nimefukuzwa getini na "mitulinga". Nchi ya ajabu sana.

Nihitimishe kwa kusema Magufuli alizaliwa Chato, akaishi, akatuongoza, akafariki, akazikwa Chato, finito! Hana "legacy' yoyote. Chapeni kazi. No Legacy any more! Karibuni!
Kuacha legacy ni jambo moja, na watu waliaochiwa legacy kufanikiwa kuiendeleza legacy hiyo ni jambo jingine.

Ni kweli kabisa Mwalimu Nyerere ameacha legacy lakini je, tunafanikiwa kuifuata na kuendelea kuifuata kwa kiwango gani? Na kama hatufanikiwi, ni kwa nini, wakati legacy aliyoaicha tunaipenda?

Kwa Tanzania ya wakati huu, bora kiongozi akaacha kumbukumbu kama vile ya kujenga angalau darasa la moja tu shule ya msingi kuliko kuacha legacy

Legacy za viongozi wetu hatuwezi kwenda nazo na kuziendeleza kama tunavyopenda kutookana na ukweli kuwa kwa wakati huu tunao maadui wengi mno walitapakaa ndani na nje ya nchi, na wana nguvu kuliko sisi

Hata hivyo, maadui hawa wanaotuletea shida kufuata legacy za viongozi wengi hawawezi hata siku moja kuja na kubomoa Tanzanie Bridge iliyojengwa na Rais SSH

Kwa hali hiyo ni bora viongozi wetu wakaendeea na Magufulification style na si kujikita kwenye kuacha legacy ambazo waTanzania hawawezi tena kwenda nazo kama inavyotakiwa kwa sababu hawana uwezo wa kufanya hivyo.
Kama hoja yako nimeielewa lakini
 
Hivi kuanzisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 haitoshi kusema mwinyi aliacha legacy
Hapana; legacy ni kama model ya kitu au jambo ambayo kiongozi huwa anaacha halafu watu wake wanakuwa wanaitumia kila mara kama chombo cha kuwasaiidia kuendelea kutatua matatizo yao mbali mbali ya sasa na ya wakati ujao pia,

Legacy kwa maana nyingine, ni Falsafa sahihi na haifanyi kazi kwenye tukio la wakati mmoja tu kama vile lile la vyama vingi vya siasa
Legacy inafanya kazi kuanzia pale ilipoaznia na kuendelea hata milele
 
Hivi mtu mwenyewe alishakufa mbona bado watu wanaumia
Kulingana na mleta mada; huyu mtu Hayati JPM hajaacha legacy yoyote ila amefanikiwa kuacha matendo makuu ya ajabu ambayo hadi muda huu bado yapo kwenye Kumbukumbu za waTanaznia

Kulinagana na mwandishi ni kwamba Mwalimu Nyerere yeye alifanikiwa pia kuacha vyote, legacy na kumbukumbu za matendo makuu, kitu ambacho ni sahihi kabisa

hata hivyo, tahadhari pekee ninayopenda kutoa mimi hapa ni kwamba, legacy isipoambatana na matendo makuu inakuwa si lolote si chochote kwa sababu legacy ni FALSAFA tu, ambayo watu wakifanikiwa kuielewa vizuri na kutumia, wanaweza kufanikiwa. Hata hivyo ikitokea kwa bahati mbaya wakashindwa kuielewa au kuikubali, haiwezi kuwasaidia chochote na itakuwa haina faida yoyote kwao; kiasi kwamba wanaweza kumuona kiongozi bora kuwa ni yule aliyewahi kuwajjengea darasa moja tu la shule ya msingi, kuliko yule aliyewahi kuacha legacy ambayo haikuwahi kuambatana na matendo makuu au ambayo hawakuweza kuikubali

Mwalimu alifanikiwa kujenga viwanda nchi nzima na hicho ndicho wanachokikumbuka kwa akili zao zote hadi sasa kuzidi hata wanavyoweza kuwa wanaikumbuka FALSAFA yake ya Siasa ya Ujama na Kujitegema

Kwa hali waliyonayo kwa wakati huu, Watanzania wanahitaji kutendewa matendo makuu ya kuwapeleka kwenye maendelea na si kuaminishwa kwenye FALSAFA peke yake

Mungu aendelee na Mama SSH kwa kishindo kikuu
 
Ujamaa wa nyerere uko wapi? Hata iwe kawacha legacy hiyo?
 
Back
Top Bottom