Gari kuwa ya biashara haihalalishi wao kuvunja sheria. Unakuta mpo kwenye foleni anatanua kushoto na akiona askari ndio analazimisha kuchomekea. Kuna lanes za masaa kama zile za kuanzia Uwanja wa ndege hadi Gongo la Mboto, unakuta ni asubuhi hivyo lane 2 zinaenda mjini na moja inarudi Gomz ila maajabu yake unakuta daladala amekaa central lane ambayo kwa muda huo inaenda mjini na anakomaa kwa honi na mwendo hatarishi. Wameshasababisha ajali kibao kwa huo mtindo. Bado wanahitaji huruma hao watu?
Haya unakuta bodaboda na left overtake kwenye narrow roads, ikitokea dharura kwamba ujibane zaidi kushoto unamkuta yeye. Bado sisi ni wabinafsi??
Hao hao boda walishawahinisababishia ajali na haraka zao. Tulikuwa tunapishana na mara ghfla akakunja kona kuja upande wangu wa kulia lakini pia pikipiki ikatereza akaanguka. Ilikuwa ni high way maeneo ya Majumba sita Ukonga. Kitendo cha mie kufunga breki za ghafla kumnusuru gari lilokuwa nyuma yangu pamoja na jitihada zake za breki bado akaja kunigonga gari langu kwa nyuma.
Hapo Boda boda ingekuwa amri yangu ningewaondoa mjini.
Hapo hakuna ubinafsi mkuu ila ni ukweli mtupu. Sheria haina exemption na ni lazima kila mmoja afuate bila kuangalia mazingira