benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Siku chache baada ya Taasisi ya Al Hikma kutangaza uamuzi wa kuwalipia mahari vijana 50 ili waoe, zaidi ya vijana 1,000 wametuma maombi wakiwamo wanawake watatu wanaowaombea wachumba zao.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo
Shehe Nurdin Kishki amesema Dar es Salaam jana kuwa saa chache baada ya kutangazwa kwa ofa hivo taasisi hiyo ilianza kupokea maombi.
"Tulipotangaza tu siku ile ya Aprili 9 pale Uwanja wa Uhuru tulianza kupokea simu, kwenye kurasa zetu za kijami, barua pepe maombi ya vijana zaidi ya 1,000 wanaoomba kuozeshwa," alisema Shehe Kishki.
Alisema dirisha la kuchukua fomu za maombi limefunguliwa jana hadi Mei 5 mwaka huu na watakaochaguliwa baada ya kufungishwa ndoa pia watapatiwa semina ya ndoa ndipo watakabidhiwa wake zao.
"Hatutaki ndoa hizi ziishie baada ya fungate kwenye talaka. Ndio maana hatutaki vijana wa kukurupuka tu baada ya kusikia tangazo hili, tumelenga wale wenye nia na shida kweli ya mahari. Tunaamini talaka za vijana zikiongezeka ndio na mmomonyoko wa maadili unaongezeka," alisema Shehe Kishki.
Alisema baada ya taratibu zamaombi na mchujo kukamilika ndoa hizo zinatarajiwa kufanyika baada ya miezi mitatu hadi minne kuanzia sasa.
Ametangaza masharti manane kwa waombaji ili kupata sifa ya kulipiwa mahari na kuozeshwa ikiwemo waombaji kuwa tayari wa-metoa posa na kupangiwa mahari.
Alitaja masharti ya vijana wanaotaka kuingizwa kwenye programu hiyo kuwa ni lazima kijana mwombaji awe Muislamu kwa kuwa ndoa hizo zitafungwa na kusimamiwa na Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi Bin Ally.
Aidha, alisema sharti lingine ni lazima kijana mwombaji asiwe na mke, awe amejaza fomu maalumu ya maombi, lazima afanyiwe usaili, awe tayari kufunga ndoa ya pamoja Dar es Salaam, awe Mtanzania na lazima athibitishwe na imamu wa eneo lake.
"Hivi ninavyoongea tayari tumeshapokea maombi kutoka nje ya nchi wakiomba kuozeshwa akiwemo kijana Mtanzania anayeishi Misri. Lakini sisi tumewalenga vijana wa hapa nchini na lazima wakidhi vigezo hapo ili fedha isitumike kwa watu wasio na uhitaji," alisema Shehe Kishki na kuongeza:
"Tutalipa mahari, ukumbi, chakula, vifaa vidogo vidogo vya hapa nchini na lazima wakidhi vigezo hapo ili fedha isitumike kwa watu wasio na uhitaji," alisema Shehe Kishki na kuongeza:
"Tutalipa mahari, ukumbi, chakula, vifaa vidogo vidogo vya chumbani na bwana harusi atapewa kadi 20,10 kutoka upande wake na 10 upande wa mkewe kuja kushuhudia ndoa yake hiyo.