Wanaoomba kulipiwa mahari Al Hikma wafika 1,000, wapo wanawake, wanatakiwa 50 tu

Swali langu ni kwa hao wanawake,wao si ndo wataja kiwango cha mahari ina maana wameshindwa kutaja msahafu au wametaja kisha wanaume zao wamekosa pesa za kununulia?
Jamani masahafu Ni kitabu kitakatifu lakini huwezi kwenda dukani kununulia unga ukapika ugari tujifunze kufanya reasoning, mwanamke akitaka msahafu sawa lakini yeye ndio ana haki ya kutaja nae ana mahitaji yake yanayotimizwa na pesa tukitumia masahafu nakesho tukikosa pesa ya kula tusomeane masahafu njaa iishe.....tuna manipulate dini Sana.
 
Hio taasisi imewaumbua wengi sana . Mkuu humu Jf tulikua tunaambiwa waislam hamshindwi kutoa mahari maana ni ndogo sana tena hata msahafu tu inatosha na harusi haina mahitaji sana. Sasa haya ya kulipiana mahari ni mageni kwa wengi wetu humu JF
 
Hizi mahari inaweza kuwa issue kabisa mpaka mtu kushindwa kuoa?.....

Mkishapendana, waomba mahari unawapiga sound tu kwa kutanguliza hata 10K na nyingine utaleta....ruhusa ya ndoa ikishapita tu imekula kwao.
 
Hio taasisi imewaumbua wengi sana . Mkuu humu Jf tulikua tunaambiwa waislam hamshindwi kutoa mahari maana ni ndogo sana tena hata msahafu tu inatosha na harusi haina mahitaji sana. Sasa haya ya kulipiana mahari ni mageni kwa wengi wetu humu JF
Mahari za waislama kwa ndoa nyingi Ni around 300K hio ni nyingi kwani ??

Simply, Kuna mahari za 400K au tuseme 300K hii still Ni ndogo the same time Kuna kijana anayefanya kazi kiwanda Cha sabuni au pale Pepsi kwa siku wanalipwa 5000/7000 kijana huyu kuweza kukusanya 400K ya pamoja sio jambo rahisi kamwe inaweza pita mwaka mzima, miaka 2 mpaka 3 na ajapata 400K ya pamoja....kwahio kulipiwa mahari hio HAIMAANISHI kuwa hio mahari sio ndogo.

Tukija kwenye mahari kuwa masahafu still Kuna maelfu ya ndoa ya afungwa kwa mahari ya msahafu kila mwaka.

Mbali na kuliangalia jambo hili kwwnyw mahari ila hili jambo la kijamii zaidi sehemu ya waislam kujamiiana pia
 
Hee.....maajabu haya.
 
Binadamu tunafanya maisha yanakuwa magumu sana, yaani unatoza mahali yakuolewa binti yako kiasi cha kumshinda muoaji matokeo yake anaghailisha na kuoa.
 
Mzini shoga basha kahaba hana haja ya ndoa
Sio kila mkataa ndoa shoga, mm muda huu nipo na WIFI yako lakin sina mpango wa kuoa na tunaishi huu mwaka wa pili, lkn ww unaishi kwa hisani ya viuno vya dadako. Hivi shule zmefungwa kwani?
 
Tuwaombee mema, ndoa zao zitadumu inshaAllah
 
Ila KIUME, ni bora uende ukweni na kitu kidogo, uwaambie hali tete wakuvumulie upambane kutafuta mahari ukipata utalipa kilichobaki. Hii ya kulipiwa mahari imekaa kiboya sana. Kama umeshindwa kupambana kupata mahari, utaweza kweli kupambana kulisha mke na mtoto? Hata kama mnapendana kiasi gani, mtoto wa kiume kama huna uwezo, huna hela zako, usikimbilie ndoa maana hamtakula penzi lenu.
Ukioa wakati huna uwezo ili utimize masharti ya imani kuna wasamaria wema watakusaidia kukulelea mkeo, na ndio hapo utapiga simu redioni kuomba wimbo wa kisa cha mpemba..
 
Hii kitu iliishaje? Vijana walifanikiwa kuozeshwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…