Wanaoomba kulipiwa mahari Al Hikma wafika 1,000, wapo wanawake, wanatakiwa 50 tu

Wanaoomba kulipiwa mahari Al Hikma wafika 1,000, wapo wanawake, wanatakiwa 50 tu

Jamani si kila anayenyoosha mkono darasani mwalimu anapouliza swali basi anajua jibu mwingine ni msindikizaji tu so interview Wanayotaka kuifanya ni kwa ajili ya kupata wale waelewa na wenye msingi bora wa dini ambao watakalishwa chini na kufundishwa namna ya kuwa na uadilifu pindi atakapoozeshwa. Tusiwakatishe tamaa huenda baina yao wakapatikana waongofu watakao saidia kutupatia vizazi bora vya baadaye
 
Elimu kwa wazazi itolewe wasiwe vikwazo kwa vijana wao wanapopata wenza, endapo mahari itatakiwa kuwa laki 2,basi kijana atakapokuwa hata japo na kianzio cha hamsini, ndoa ifungwe bila shida.
Hilo ipo wazi na hata mafundisho yanasema katika hadithi kuwa ndoa bora ni yenye mahali hafifu ,hata kwa ndizi kama mahari ndoa inapita ikiwa muolewaji ameridhia japo swala hilo limepewa uhuru kwa muhisaka kutaja.

Na ndoa ni moja kati ya majambo yanatakiwa yawahishwe katika uislamu maana bila hivyo maranyingi hakuna njia isipokuwa uzinzi kuenea kutokana na hilo wazazi na wahusika wenyewe wanashauriwa mara nyingi kutoweka ugumu katika swala la ndoa. Lakini tatizo miongoni mwa watu wapo ambao bado wabishi na wanafanya mambo yawe magumu.
 
Kwenye uislamu hakuna mkaja wa bibi wala babu, ni binti anaulizwa anahitaji mahari yake iwe nini atakayotaja mwanaume unatakiwa ulete. Apatiwe binti mahari yake sio ya wazazi wala walezi.
Ndio maana unapendwa ,una akili Sana umejibu kwa mnogo
 
Kuna watu hawana akili wana mentality za kuombea watu mabaya na kupenda wanzao wafeli tu ,kama una moyo safi na hauna maradhi kama hayo basi una kitu kikubwa sana moyoni kwako.
🙏🙏🙏
 
Huna akili na itakuwa ajabu kichwa kama chako kuwa na familia inayokutegemea,anza na serikali kwa nini inatoa mkopo vyuoni na kwa vijana wachache ikiwa waombaji ni wengi kwa nini wasitoe kwa wote ?
We mfia dini unafananisha serikali na mambo ya imani? Huoni kuwa dini haipaswi kuonesha ubaguzi? Serikali ina namna nyingi kuwahudumia wananchi wake. Wakikosa mikopo kuna sehemu nyingine watahudumiwa, fikiria kuna elimu bure wanasoma watoto wote. Mtu wa dini unaitisha kusaidia watu hamsini kwani hujui kuwa watajitokeza wengi na utaishia kufanya ubaguzi na upendeleo? Dhambi kubwa sana hii ya kujitakia
 
Swali langu ni kwa hao wanawake,wao si ndo wataja kiwango cha mahari ina maana wameshindwa kutaja msahafu au wametaja kisha wanaume zao wamekosa pesa za kununulia?
 
we mfia dini unafananisha serikali na mambo ya imani? Huoni kuwa dini haipaswi kuonesha ubaguzi? Serikali ina namna nyingi kuwahudumia wananchi wake. Wakikosa mikopo kuna sehemu nyingine watahudumiwa, fikiria kuna elimu bure wanasoma watoto wote. Mtu wa dini unaitisha kusaidia watu hamsini kwani hujui kuwa watajitokeza wengi na utaishia kufanya ubaguzi na upendeleo? Dhambi kubwa sana hii ya kujitakia
Bado nasisitiza kuwa akili huna ,unadahani kuna mtu anaweza kuwasaidia watu wote wenye uhitaji ? hakuna hata mtu awe tajiri vipi.Dini inataka kila mtu afanye kile kilichopo ndani ya uwezo wake mfano mimi ninamfuturisha mtu mmoja kila siku kwa sababu huo ndio uwezo wangu na hakuna sheria ya kunilazimisha .

Sasa unatoa wapi mamlaka ya kulazimisha idadi ya watu mtu anaotaka kusaidia wakati mtu mwenyewe anajua fika uwezo wake upi ?

Nimetoa mfano wa mikopo serikalini kuonyesha kuwa sababu kubwa inayopelekea mtu kushindwa kuhudimia idadi kubwa ni uwezo na hata uwezo ukiwa nao lazima ugawe kwa ufanisi kwani hitajio sio moja .
 
Swali langu ni kwa hao wanawake,wao si ndo wataja kiwango cha mahari ina maana wameshindwa kutaja msahafu au wametaja kisha wanaume zao wamekosa pesa za kununulia?
Mahari mara nyingi mwanamke anatumia na yeye kufanya maandalizi binafsi ya ndoa ,jambo jipya kama hilo lazima afanye maandalizi ya ziada kwani kutakuwa na mambo ya ziada ambayo yanahitaji fedha hivyo katika haki nyingine inalazimu pesa zitumike hapo inakuwa ngumu kutaja msahafu au kiwango cha chini cha pesa.
 
Huna akili , kuna watu wanalipiwa ufadhili wa masomo na watu au serikali vyuoni mtu anaomba kwenye pesa ya mkopo alipiwe angalau ada ili aweze kusoma .

Udini unakusumbua na utakuua kwa kuteseka pasipo na sababu za msingi.
hiyo ni taasisi ya kidini haipaswi kutoa ufadhili kwa ubaguzi na upendeleo, hao wote waliojitokeza kulipiwa mahari wanahitaji huo msaada na wote wanastahili kusaidiwa bila hata kufanyiwa usaili. Ukifanya ubaguzi ni dhambi
 
Baada ya ndoa kufungwa, na baada ya miezi sita kupita, katika ndoa 50 zitakazo kuwa salama ni ndoa 10 pekee, nazo baada ya miaka miwili kutakuwa hakuna ndoa,
Why:
Nafsi ya muoaji ya dhati na upendo wa dhati huwa haifungwi na mahari,ukizingatia mahari huweza kulipwa kidogo kidogo au awamu kwa awamu.
Kwenye Uislamu mahari ndio ndoa yenyewe bila mahari hakuna ndoa na kwenye Uislamu mahari inatamkwa na mwolewaji na inakuwa mali yake binafsi sio kama kwenye ndoa nyingine tunasikia malipo wanayotoza wazazi nayo wanaita "mahari" utafikiri wao ndio wanaolewa!
 
Huna akili na itakuwa ajabu kichwa kama chako kuwa na familia inayokutegemea,anza na serikali kwa nini inatoa mkopo vyuoni na kwa vijana wachache ikiwa waombaji ni wengi kwa nini wasitoe kwa wote ?
naona kama umechanganyikiwa we mfia dini, kuna ambao wananipa nzuri we umekazana kunimwagia dislike kila uonapo comment zangu unakereka. Uwe na akili huru dini yako imekuharibu akili na umekuwa mtumwa wa fikra. Unajua kumlipia kijana mahari italeta dharau kwa mke wake na kwa jamii inayomzunguka? Huyu sheikh angetoa mitaji ya biashara au miradi ya kiuchumi kwa vijana hao inge make sense. Unamlipia mtu mahari apate mke ataenda kumlisha mawe huyo mke kama tu mahari hakuwa nayo?
 
Huoni wametangaza na vitu vingine kwenye habari kama semina ya ndoa au umekurupikia mada ?
Namaanisha, kinachokwamisha watu kufunga ndoa ni kukosa mahari tu? Kwamba wote wasio na ndoa ni ukosefu wa mahari?
 
Back
Top Bottom