Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 441
- 1,065
Yanayoendelea sasa kwa baadhi ya askari wa jeshi la polisi ni matokeo ya watu kufanya kazi wasiyoipenda. Hawawezi kuifanya kwa ufanisi.
Hapo zamani za kale kimbilio la waliokosa ajira ilikuwa fani ya ualimu. Kilichotokea ni kushuka kwa kiwango cha elimu nchini kwasababu ya kukosa morali ya kufanya kazi kwa walimu.
Siku za hivi karibuni kwenye elimu hakuna ajira mpeto mpeto tena na wanaotakiwa kusoma fani hiyo wanatakiwa wawe na ufaulu mzuri tofauti na ilivyokuwa awali.
Pia soma: Simiyu: Mkuu wa Mkoa athibitisha kifo cha Mtu mmoja katika Maandamano ya Busega
Toka zamani za kale kwenye majeshi yetu wamekuwa wakipokea vijana wenye ufaulu tofauti tofauti kuanzia wenye ufaulu wa juu, wa kati, wa chini na hata waliofeli.
Hata hivyo, tofauti na zamani za kale ambapo walioomba kujiunga na majeshi yetu walikuwa wale "wanaopenda" /wenye hobby ya kazi hiyo awe amefaulu au amefeli, siku hizi huko kwenye majeshi imekuwa kimbilio la waliokosa ajira.
Ukiangalia vijana wanaojiunga na majeshi yetu hata wale ambao ni wahitimu wa chuo kikuu, kwa asilimia kubwa halikuwa chaguo lao la kwanza. Wengi wanaenda ilimradi ni ajira itakayompa kipato na mbaya zaidi hata wanaoingia huko baadhi yao wanavutwa na "wajomba".
Matokeo yake ndio hiki kinachoendelea kwasasa kwenye baadhi ya maeneo hasa upande wa jeshi la polisi.
Weledi umeporomoka kwa kiasi kikubwa kwasababu walioko huko hawana furaha na kazi yao kwasababu halikuwa chaguo lao.
Sehemu ya kutumia maneno, wanatumia risasi za moto. Kwasababu wanajua kukoki silaha tu na kurusha risasi, hawana muda wa kutumia akili zao kwasababu hata mafunzo hawakuyazingatia kwani haikuwa hobby yao.
Tabia ya wazazi kuwalazimisha vijana kwenda kufanya kazi sehemu ambayo sio chaguo lao kwasababu za kujipatia kipato ni kudidimiza maendeleo ya nchi na ustawi wa jamii.
Daktari anayefanya kazi hiyo bila kuipenda hatawaheshimu wagonjwa kwasababu hakujiandaa kuwa daktari. Matokeo yake wagonjwa wengi watakufa mikononi mwake, wengine wataongeza usugu wa magonjwa kwa kupewa dozi isiyo sahihi. Hali kadhalika kwa askari anayefanya kazi hiyo ambayo haikuwa chaguo lake.
Ili ufanikiwe na ufanye kazi kwa weledi lazima ufanye kile unachokipenda na unakiweza na unajivunia kukifanya. Kazi yako ukiipenda utaifanya kwa weledi na hautopenda ichafuke.