Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

hilo
Mapadri hawahawa waosifika kwa kuwazibua watoto mitaro afu ndo haohao wanaondoa dhambi?

Kweli imani zá watu!

Sent using Jamii Forums mobile app
hilo tu waliona je la mashekhe wanaizibua watoto mitaroo.. yule ustadhi wa mwanza aliyeshikwa ugoni kwa kuharibu vitoto alivyokuwa anavifundisha chuo..vepee!!! Msipende kuhukumu watu angalia matendo yako kwanza ..... kila mtu asimamie imani yake kikamilifu...
 

Imepenya hiyo.Hayo ya Walutherani sijui walokole achana nayo.Timu yako Wewe ndiyo inajitia kichwa maji.
 
Kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu.
Namwungamia Mungu Mwenyezi nawe padre wangu.Sikuungama tangu..........Niliondolewa dhambi, nikatimiza malipizi. Dhambi zangu ni hizi......
Najuta dhambi zangu zote.
Ee Yesu unihurumie.
Huo hapo juu ndio utaratibu wa kuungama wakatoliki. Je kuna mahali panaonyesha kwamba wakatoliki huungama moja kwa moja kwa padre? Padre huwa ni msimamizi tu wakati muumini anamwungamia Mungu wake, na tena mwishoni ni yeye yule Yesu anayeombwa huruma yake.
Hebu tuache kushuhudia uwongo jamani, tutahukumiwa kwao.
Wakatoliki wenzangu naomba tufuatilie na kutetea imani yetu kwa nguvu zote na ushahidi usio na shaka.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanisa la roma halijawahi kuwa la kweli hata siku moja, lenyewe ndilo lililo waua wakina petro.

Kanisa la sabato lililoanzishwa kwa misingi ya "kisangoma" (na hadi leo linaendelea na muelekeo huo huo),ndio la kweli?

Ombeni labda nisiwe hai na JF ifungwe. Nina orodha mambo ya mama yenu, Ellen White na wapiga ramli wenzie kama 1000 hivi, tena ya hovyo sana. Nitayachambua moja baada ya jingine tena kwa uweledi unaostahili. Ni lazima mfike mahali muelewe kwamba kupiga kwenu kelele haimaanishi kwamba watu hawakuwa na majibu ya ujinga na upotoshaji wenu.
 
Hahaah sasa mkuu tupo kwenye uhalali wa mapadri kusamehe watu dhambi! Wewe unakimbilia kwa wasabato! Hii maada inawahusu hao wasabato?
 
Unajua kama padri nae huwa anaungama dhambi?
 
Yesu wangu...unamaanisha walionje ya ukatoriki au wasioungama kwa padri wote ni motoni kwakuwa hawajasamehewa?
 
Aliyekufundisha hivyo, alisoma Biblia kwa kurukaruka. Maneno "Kristo" na "Kristu" ni maneno yenye maana sawa tu.La kwanza limetoholewa kutoka Kigriki na la pili limetoholewa kutoka Kilatini.
Nafikri tutumie kiyunani ndicho ambacho kwa asilimia nyingi biblia imetoka ktk maneno ya kiyunani
 
Mbona bado uko hapa tu? Nilifikiria umeshafika Vatikani kwenda kumshinikiza ili ajiuzulu upesi kama anavyotakiwa.
Kuhusu makasisi ni kweli wanashida na hata yule aliyepita ni matatizo yalisababisha ajiuzuru si kama alipenda. Hata huyu wakimkomalia ataenda na maji. Na akijiuzuru huyu waafrika weusi mtapata papa wa kwanza.
 
Ktk vitu ambavyo watu hufunga ufahamu wao kwa yale tu waliyoyasikia mwanzo ni dini na kabila.
 
Ok ni sawa. Ndiyo maana wengi tumezoea Kristo kwasababu biblia iliandikwa ktk kigiriki na kiyunani ktk lugha ya mwanzo.
 
Ni kuhani...ndiye aliyepewa mamlaka ya kufundisha neno la Mungu ili watu waupate uzima wa milele...

Pia ndiye aliyepewa mamlaka ya Kusamehe dhambi kupitia kwa Yesu Kristo
Sijawai kwenda kwa padri kufanya hivyo. Je mimi ni mkosefu ?
 
Kuna mtu kathibitisha Mungu yupo? Au longolongo za kila siku tu?
 
Suala hapa sio kutubu dhambi kwa Padri au hadharani ..
Kilichoongelewa kwenye hiyo mada ni uhakika wa huyo padri kutunza hiyo siri, na kama hawezi kutunza siri basi ni bora nikatubu hadharani ili ulimwengu mzima usikie na kunisamehe kwa sababu kama nilikuwa jambazi sikuwa namkosea padri bali wale nilowapora zao mali.
Maajabu ni pale yule aliyekuwa mpinga kristo kijivisha ngozi ya kondoo ilihali anajulikana kwamba bado anaendelea na harakati zake za kupinga Kristo.
Yeye ndo mfadhili mkubwa wa vyama vya kisiri vinavyoendesha mambo yanayoenda kinyume na ukristo. Hapa tutasemana tu hadi kieleweke.
 
Mtoa mada najua umetumia muda mwingi kukaririshwa vitu vingi ili uwe kibaraka wao. Ila kwa kipindi hiki mnaelekea kukwama kabisa! Hakuna tena wa kudanganyika na vitabu vyenu vyenye tafsiri isiyo rasmi.
 
Mtoa mada najua umetumia muda mwingi kukaririshwa vitu vingi ili uwe kibaraka wao. Ila kwa kipindi hiki mnaelekea kukwama kabisa! Hakuna tena wa kudanganyika na vitabu vyenu vyenye tafsiri isiyo rasmi.
Kwani wewe unatumia nini...??


Hujui hata Biblia ni mali ya hao Wakatoliki...??

Wao ndio walivipa majina na verses vitabu vya Biblia...


Endendelea kushangaa feri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…