Kama umesoma uzi vizuri utabaini kwamba uwezekano huo ungalikuwapo basi Yesu Kristu asingaliweka miundo mbinu hiyo ya Upatanisho.Kwa kuwa Yesu ni Mungu alijua watu kwa kujiungamia wenyewe wangaliishia kufanya sarakasi tu.Kuungama dhambi kunahusisha kufanya malipizi,waaidha kurudisha ulivyochukua kama alivyofanya Zakayo.
Ni kwamba tunalazimika kuungama dhambi ili mahusiano yetu na Mungu yawe mazuri.Dhambi ina madhara yafuatayo:mosi,inaleta mahusiano mabaya kati ya mwanadamu na Mungu.Pili,kati ya mtu mmoja na mwingine na tatu, kwa mtu mwenyewe.
Kumbe tofauti na Wakristu wengine wanavyoelewa, dhambi haiharibu tu mahusiano kati ya mwanadamu na Mungu, bali pia kati ya wanadamu na wanadamu.Mt.Paulo anatueleza mara nyingi sana katika barua zake kuwa sisi ni viungo katika mwili wa Kristu na kwamba yeye (nafsi ya Pili) na Mungu baba ni wamoja Rejea Warumi 12:5):
“Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.”
Kwa hiyo, ni mantiki hiyo kwamba kwa sababu sisi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake,basi dhambi ya mtu mmoja haiishii katika kumuumiza mhusika pekee, bali madhara yake lazima yamguse na mwingine katika mnyororo ule ule unaotuunga kwa Kristu.(Rejea 1 Kor 12:26):
“26 Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.”
UNACHOONGELEA WEWE UNAMAANISHA KUTUBU
Injili ya Marko 1:1-5, nayo inatueleza kuwa watu walikuwa wanamwendea Yohana Mbatizaji wakishakutubu na wakishaungama dhambi zao, walibatizwa ili kupokea ondoleo la dhambi zao:
“4 Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao. 5 Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani”.
Katika ya aya 4 na 5 ya Injili hiyo ya Marko, tunapata maneno mawili “Kutubu” na “kuungama” ambayo yana maana tofauti.
Na mwinjili Marko, anapotuandikia hivyo anamaanisha kwamba kulikuwa na mambo mawili yanafanyika kwa mtaka ubatizo kabla hajabatizwa.Mosi, kutubu dhambi na pili,kuungama dhambi.
KUTUBU, kunatofuatiana na KUUNGAMA kwa sababu, kutubu ni hali ya kuugua moyoni.KUTUBU ni kitendo cha kujutia tendo fulani.Kutubu hufanyika moyoni, wakati kuungama kunafanyika nje ya nafsi ya mtu.
Kuungama ni kusema nje ya moyoni na mbele ya mtu mwingine kuwa umekosa.Kumbe, Marko anapotumia maneno hayo mawili sio kama anataka kutueleza maana ile ile moja ya kujutia dhambi moyoni bali kuweka wazi hizo dhambi zenyewe.
Yakobo naye katika 5:14-15, anatupatia picha halisi ya maana ya neno kuungama anapotumia neno “ungamianeni” dhambi zenu.Ikiwa Yakobo alitaka kumaanisha mtu kusema dhambi zake kimoyokimoyo, basi angalitumia neno jingine na wala sio ungamieneni:
“14 Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.15 Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.16 Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.”