Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Kuungama dhambi kwa Padre iko wazi sana kimaandiko. Tatizo ni walokole wengi kufikiri ukishaokoka hutendi dhambi tena. Wanajipa moyo kwa utakatifu wa kutotenda dhambi ambazo wao wanafikiri ndio dhambi ikiwemo uzinzi, kunywa pombe ( hata kama si mlevi) n.k lakini upo uovu mwingi tu wanatenda wakati mwingine kutokana na mafundisho hafifu juu ya dhambi.

Yapo mazingira unaweza kutubu mwenyewe kama upo katika sehemu ambayo hakuna padre na upo kwenye hatari.

Kingine ifahamike kitubio kinaanzia mbali kuanzia kujutia na kukusudia kuacha dhambi then unapoungama kwa Padre ni ukamilisho wa kitubio na kupokea msamaha wa Mungu na hasa inatia nguvu na faraja unaposikia Padre akitamka kwa niaba ya Kristo "umesamehewa dhambi zako usitende dhambi tena".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye dhambi hawezi ondoa dhambi zá mwenzake.

Ukatoliki comedi zaidi.

Nilizaliwa na kukulia humo. Mjadala wa comedi zá wakatoliki JF hawezi tosha

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamuelewi maana ya mtu kupewa mamlaka. Mamlaka ya kusamehe dhambi hayafutwi na dhambi ya mhusika.

Padre anapokuwa katika dhambi hiyo inabakia yeye na nafsi yake lakini wewe unayekwenda kwake unapata neema ile ile ya kimamlaka.

Mfano mzuri ni Rais wa nchi, akifumaniwa akizini hakuondoi mamlaka yake ya kuamuru jeshi kuingia vitani au amri yoyote ya kisheria.

Kama Mapadre wangekuwa wanafanya hayo kwa mamlaka yao basi tungeweza kwanza kuhesabu maovu yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana Yesu alipokuwa akisamehe wayahudi waliona anakufuru. Sishangai hata nyie kuendelea kushangaa hata pale alipowapa mamlaka hayo mapadre.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza hili andiko wataosoma lote kwa umakini ni wachache na hasa Wakatoliki wanaotaka kujua imani yao ....wale wa "rohoni" hujipa majibu mapema kabisa ....ukisoma comments utaona hata reply zao zimejibiwa vizuri tu kwenye andiko lakini wanakuja na majibu ya maswali yao wanayoyajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu! Hivi unatubu kwa binadamu mwenzako kwani mungu hayupo? ndio hawa hawa wanaojiua kwa kujirusha gorofani kwa tuhuma za ubadhilifu wa pesa ndio tutubu kwao?!
Mwanadau hana uwezo wa kusamehe dhambi! Binadamu ni binadamu tu siku zote
 
Mkuu kwenye uzi wako nimeona neno "YESU KRISTU"
Usahihi ni "YESU KRISTO" siyo "YESU KRISTU"

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii nchi tunasafari ndefu..

Na tatizo lingine ni lugha yetu kiswahili imekiwa ni lugha masikini..inakopa maneno huku na huko .


Ni hivi mpendwa(Uende ukawaelimishe na wengine)

Hakuna tofauti ya maneno Kristo na Kristu...maneno yote hayo mawili yametoholewa kwenye lugha mbili za Biblia...yaani Kilatini na Kigiriki..

Kristu.....ni kilatini..."Kristus"...sisi kwa kiswahili tukatohoa Kristu..

Kristo...ni Kigiriki..."Kristos".....sisi tukatohoa kwa kiswahili Kristo .


Ukifuatilia kwa makini maneno mengi ya Kilatini yanaishia ni ....us-
Mfano...Augustus, Cornelius, Titus, Anacketus, Thaddeus...

Vivyo hivyo kwa Kigiriki


Ahsante
 
Soma mada uelewe....ungejipa muda kusoma ungeelewa..
 
Upo kanisani/dhehebu unalosali kwa matakwa yako au kwa sababu umewakuta babu, bibi, baba, mama etc wanasali huko na wewe ukajiunga nao...think sio unapokea mapokea na kutiririka nayo tu kwa sababu huna choice...unafuata mkumbo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha mbwembwe wewe biblia ya kiswahili ina neno "KRISTO" siyo "KRISTU"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni kawaida na mada zake siku zote, namjua, nenda jukwaa la dini ndio utakuta mada zake nyingi za kuwaponda wasabato,
Hizi ndio akili za Watanzania....na labda wewe ni Msabato hivyo unawakilisha akili za Wasabato ..


Hivyo yeye kuleta mada za kuonesha mapungufu wa Wasabato hivyo kuna kuzuia wewe kusoma maudhui ya mada...??

Huoni kutukosoma kwako mada kutafanya uharibu huu uzi..??
 
Acha mbwembwe wewe biblia ya kiswahili ina neno "KRISTO" siyo "KRISTU"

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuh ......Kwakweli tuna kazi .....pamoja na kuandika yote hayo bado hujanielewa....???



Labda ni kuambie kitu...Biblia ilikuwa Cimpilled na Kanisa Katoliki....Lugha ya Agano la Kale ilikuwa Kiebrani....

Wakati Agano jipya ilikuwa ni Kiyunani (Kigiriki)

Transalation ya kwanza yaani "Vulgate" aliyoifanya St. Jerome (Padre) alifanya kutoka lugha zote hizo na kwenda Kilatini...

Sijui kama tumeelewana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…