Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Kuungama dhambi kwa Padre iko wazi sana kimaandiko. Tatizo ni walokole wengi kufikiri ukishaokoka hutendi dhambi tena. Wanajipa moyo kwa utakatifu wa kutotenda dhambi ambazo wao wanafikiri ndio dhambi ikiwemo uzinzi, kunywa pombe ( hata kama si mlevi) n.k lakini upo uovu mwingi tu wanatenda wakati mwingine kutokana na mafundisho hafifu juu ya dhambi.

Yapo mazingira unaweza kutubu mwenyewe kama upo katika sehemu ambayo hakuna padre na upo kwenye hatari.

Kingine ifahamike kitubio kinaanzia mbali kuanzia kujutia na kukusudia kuacha dhambi then unapoungama kwa Padre ni ukamilisho wa kitubio na kupokea msamaha wa Mungu na hasa inatia nguvu na faraja unaposikia Padre akitamka kwa niaba ya Kristo "umesamehewa dhambi zako usitende dhambi tena".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye dhambi hawezi ondoa dhambi zá mwenzake.

Ukatoliki comedi zaidi.

Nilizaliwa na kukulia humo. Mjadala wa comedi zá wakatoliki JF hawezi tosha

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamuelewi maana ya mtu kupewa mamlaka. Mamlaka ya kusamehe dhambi hayafutwi na dhambi ya mhusika.

Padre anapokuwa katika dhambi hiyo inabakia yeye na nafsi yake lakini wewe unayekwenda kwake unapata neema ile ile ya kimamlaka.

Mfano mzuri ni Rais wa nchi, akifumaniwa akizini hakuondoi mamlaka yake ya kuamuru jeshi kuingia vitani au amri yoyote ya kisheria.

Kama Mapadre wangekuwa wanafanya hayo kwa mamlaka yao basi tungeweza kwanza kuhesabu maovu yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu hawapaswi kuungama kwa padri. Watu wanapaswa kuungama dhambi zao kwa Mungu.
Baada ya Yesu kufa msalabani Mungu alifungua njia ya watu kumwendea yeye kwa sala na toba.

Baada ya mtu kumkiri Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wake anakuwa amesha okolewa.sasa anakuwa na namba ya simu kupiga kwa Mungu moja kwa moja. Haitaji tena kupiga customer care au operator amuunganishe.

wali: "Ni nini ilikuwa umuhimu wa hekalu pazia kuwa vipande viwili wakati Yesu alikufa?"

Jibu: Wakati wa uhai wa Yesu, hekalu takatifu katika Yerusalemu lilikuwa ndilo nguzo muhimu katika maisha ya kidini ya Kiyahudi. Hekalu ilikuwa mahali ambapo dhabihu za wanyama zilikuwa zinafanyiwa na ibada kwa mujibu wa sheria ya Musa iliyofuatwa kwa uaminifu. Waebrania 9: 1-9 inatuambia kwamba katika hekalu pazia ilitenganisha pahali takatifu zaidi ya patakatifu – mahali ambapo uwepo wa mungu uishi ulimwenguni- kutoka kwa mahali pengine Hekaluni ambapo watu waliishi. Hii iliashiria kuwa binadamu alitenganishwa kutoka Mungu na dhambi (Isaya 59: 1-2). Ni kuhani mkuu tu aliyeruhusiwa kupita zaidi ya hii pazia mara moja kila mwaka (Kutoka 30:10, Waebrania 9: 7) aingie katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya waisraeli wote na kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zao (Mambo ya Walawi 16).

Hekalu la Sulemani lilikuwa dhiraa 30 kuelekea juu (1 Wafalme 6: 2), lakini Herode alikuwa amezidisha urefu hadi dhiraa 40, kulingana na maandiko ya Josephus,mhisitoria Myahudi wa karne ya kwanza. Hakuna uhakika kwa kipimo halisi cha dhiraa moja, lakini ni salama kudhani kwamba pazia hili lilikuwa mahali fulani karibu futi 60 juu. Josephus pia anatuambia kwamba pazia hili lilikuwa na upana wa inchi nne na kwamba farasi hata wafungwe kwa kila upande hawangeweza kuirarua dhiraa hii . Kitabu cha Kutoka kinafundisha kwamba pazia hii pana iliundwa kwa mtindo kutoka samawati( buluu), zambarau, na nyekundu, na kitani kizuri cha kusokotwa.

Ukubwa na unene wa pazia unafanya matukio yanayotokea wakati wa kifo cha Yesu juu ya msalaba kuwa wa maana sana. "Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka."(Mathayo 27: 50-51a).

Hivyo, je,tunafanya nini kwa hili? Ni umuhimu gani dhiraa hii ilyopasuka inayo kwetu siku hizi? Zaidi ya yote, kuraruriwa kwa dhiraa wakati wa kifo cha Yesu kuliashiria kidrama kwamba kafara yake, kumwaga damu yake mwenyewe,kulikuwa upatanisho wa kutosha kwa ajili ya dhambi.Kuliashiria kwamba sasa njia ya kuingia Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa wazi kwa watu wote, kwa wakati wote, Wayahudi na Mataifa.

Wakati Yesu alikufa, dhiraa iliraruka, na Mungu akatoka mahali pale kwamba kamwe hangeishi tenai katika hekalu zilizojengwa na binadamu (Matendo 17:24). Mungu alikuwa amemalizana na hekalu hilo na mfumo wake wa kidini, na hekalu na Yerusalemu ziliachwa "zikiuzunika kwa ukiwa" (kuharibiwa na Warumi) katika mwaka 70 A.D., tu kama Yesu alitabiri katika Luka 13:35. Bora tu Hekalu lilisimama, liliashiria kuendelea kwa Agano la Kale. Waebrania 9: 8-9 inarejelea umri uliokuwa unapita mara tu agano jipya liliimarishwa (Waebrania 8:13).

Kwa maana, dhiraa iliashiria Kristo mwenyewe kama njia ya pekee kwenda kwa Baba (Yohana 14: 6). Hii imeonyeshwa kwa ukweli kwamba kuhani mkuu alipaswa kuingia Patakatifu pa Patakatifu kupitia kwa dhiraa . Sasa Kristo ni Kuhani wetu mkuu zaidi, na kama waumini katika kazi yake iliyokamilika,tunashiriki katika Ukuhani wake bora.Tunaweza sasa kuingia Patakatifu pa Patakatifu kupitia kwake. Waebrania 10: 19-20 inasema kwamba “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia ilyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia , yaani, mwili wake."Tunaona mwili wa Yesu ukiraruriwa kwa ajili yetu tu kama alivyorarua pazia kwa ajili yetu.

Pazia kupasuliwa kutoka juu hadi chini ni ukweli wa hisitoria. Umuhimu mkubwa wa tukio hili umeelezewa kwa undani kwa utukufu katika Waebrania. Mambo ya hekalu yaliashiria mambo ambayo yangekuja, na yote yatuashiria kwa Yesu Kristo. Alikuwa pazia kwa Patakatifu pa Patakatifu, na kupitia kifo chake waaminifu sasa wanaweza kumpata Mungu bila gharama.

Pazia katika hekalu ilikuwa ukumbusho wa mara kwa mara kwamba dhambi ilimfanya binadamu kutofaa kwa uwepo wa Mungu. Ukweli kwamba sadaka ya dhambi ilitolewa kila mwaka na mara kwa mara dhabihu zingine zilirudiwa kila siku ilionyesha bayana kwamba dhambi kwa kweli haingeweza kupatanishwa kwa au kufutika na sadaka za wanyama tu. Yesu Kristo,kupitia kwa kifo chake,ameondoa vikwazo vilivyo kati ya Mungu na mwanadamu, na sasa tunaweza kumkaribia kwa kujiamini na ujasiri (Waebrania 4: 14-16).
Ndio maana Yesu alipokuwa akisamehe wayahudi waliona anakufuru. Sishangai hata nyie kuendelea kushangaa hata pale alipowapa mamlaka hayo mapadre.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza hili andiko wataosoma lote kwa umakini ni wachache na hasa Wakatoliki wanaotaka kujua imani yao ....wale wa "rohoni" hujipa majibu mapema kabisa ....ukisoma comments utaona hata reply zao zimejibiwa vizuri tu kwenye andiko lakini wanakuja na majibu ya maswali yao wanayoyajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu! Hivi unatubu kwa binadamu mwenzako kwani mungu hayupo? ndio hawa hawa wanaojiua kwa kujirusha gorofani kwa tuhuma za ubadhilifu wa pesa ndio tutubu kwao?!
Mwanadau hana uwezo wa kusamehe dhambi! Binadamu ni binadamu tu siku zote
 
Mkuu kwenye uzi wako nimeona neno "YESU KRISTU"
Usahihi ni "YESU KRISTO" siyo "YESU KRISTU"

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii nchi tunasafari ndefu..

Na tatizo lingine ni lugha yetu kiswahili imekiwa ni lugha masikini..inakopa maneno huku na huko .


Ni hivi mpendwa(Uende ukawaelimishe na wengine)

Hakuna tofauti ya maneno Kristo na Kristu...maneno yote hayo mawili yametoholewa kwenye lugha mbili za Biblia...yaani Kilatini na Kigiriki..

Kristu.....ni kilatini..."Kristus"...sisi kwa kiswahili tukatohoa Kristu..

Kristo...ni Kigiriki..."Kristos".....sisi tukatohoa kwa kiswahili Kristo .


Ukifuatilia kwa makini maneno mengi ya Kilatini yanaishia ni ....us-
Mfano...Augustus, Cornelius, Titus, Anacketus, Thaddeus...

Vivyo hivyo kwa Kigiriki


Ahsante
 
Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu! Hivi unatubu kwa binadamu mwenzako kwani mungu hayupo? ndio hawa hawa wanaojiua kwa kujirusha gorofani kwa tuhuma za ubadhilifu wa pesa ndio tutubu kwao?!
Mwanadau hana uwezo wa kusamehe dhambi! Binadamu ni binadamu tu siku zote
Soma mada uelewe....ungejipa muda kusoma ungeelewa..
 
Kwanza hili andiko wataosoma lote kwa umakini ni wachache na hasa Wakatoliki wanaotaka kujua imani yao ....wale wa "rohoni" hujipa majibu mapema kabisa ....ukisoma comments utaona hata reply zao zimejibiwa vizuri tu kwenye andiko lakini wanakuja na majibu ya maswali yao wanayoyajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo kanisani/dhehebu unalosali kwa matakwa yako au kwa sababu umewakuta babu, bibi, baba, mama etc wanasali huko na wewe ukajiunga nao...think sio unapokea mapokea na kutiririka nayo tu kwa sababu huna choice...unafuata mkumbo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi tunasafari ndefu..

Na tatizo lingine ni lugha yetu kiswahili imekiwa ni lugha masikini..inakopa maneno huku na huko .


Ni hivi mpendwa(Uende ukawaelimishe na wengine)

Hakuna tofauti ya maneno Kristo na Kristu...maneno yote hayo mawili yametoholewa kwenye lugha mbili za Biblia...yaani Kilatini na Kigiriki..

Kristu.....ni kilatini..."Kristus"...sisi kwa kiswahili tukatohoa Kristu..

Kristo...ni Kigiriki..."Kristos".....sisi tukatohoa kwa kiswahili Kristo .


Ukifuatilia kwa makini maneno mengi ya Kilatini yanaishia ni ....us-
Mfano...Augustus, Cornelius, Titus, Anacketus, Thaddeus...

Vivyo hivyo kwa Kigiriki


Ahsante
Acha mbwembwe wewe biblia ya kiswahili ina neno "KRISTO" siyo "KRISTU"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni kawaida na mada zake siku zote, namjua, nenda jukwaa la dini ndio utakuta mada zake nyingi za kuwaponda wasabato,
Hizi ndio akili za Watanzania....na labda wewe ni Msabato hivyo unawakilisha akili za Wasabato ..


Hivyo yeye kuleta mada za kuonesha mapungufu wa Wasabato hivyo kuna kuzuia wewe kusoma maudhui ya mada...??

Huoni kutukosoma kwako mada kutafanya uharibu huu uzi..??
 
Acha mbwembwe wewe biblia ya kiswahili ina neno "KRISTO" siyo "KRISTU"

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuh ......Kwakweli tuna kazi .....pamoja na kuandika yote hayo bado hujanielewa....???



Labda ni kuambie kitu...Biblia ilikuwa Cimpilled na Kanisa Katoliki....Lugha ya Agano la Kale ilikuwa Kiebrani....

Wakati Agano jipya ilikuwa ni Kiyunani (Kigiriki)

Transalation ya kwanza yaani "Vulgate" aliyoifanya St. Jerome (Padre) alifanya kutoka lugha zote hizo na kwenda Kilatini...

Sijui kama tumeelewana
 
Back
Top Bottom