Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.


1. Umesoma mada nzima na hujaona hicho kifungu husika?

2. Kuyaelewa maandiko matakatifu hakuko katika kunukuliwa kwake tu.Ingalikuwa mambo yako hivyo, basi William Miller asingaliiletea Dunia maangamizi kwa kunukuu kifungu toka aya ya Ufunuo wa Yohana na kuitafisri kwamba siku 2300 zilimaanisha miaka 2300 ambayo ingaliishia mwaka 1843/1844 ambapo yeye wafuasi wake wangalimshuhudia Yesu akishuka duniani.
 
Nataka fungu lolote kutoka kwenye maandiko matakatifu yanayo ruhusu hicho unachokitetea na mimi nitakupa verse zinazopingana mnachokiamini ni sahihi
Sasa pitia mada yote tena kisha rudi hapa kuniuliza swali.....


Ungesoma mada yote usingeniuliza swali la kipuuzi kama hilo
 
Samahani mkuu Am a theologian by the way Siku zote naamini katika maandiko
Tangu lini mdhambi akasamehe wadhambi? Tangu lini kipofu akamwongoza kipofu mwenzake give me a biblical verse that a proves that theory ya Padre kusamehe

1. Kwani wewe ulibatiwa na "Mtakatifu" Ellen White? Watakatifu (Wachungaji Ellen White, William Miller, Hiram Edson,James White), ndio walioshuka kutoka Mbinguni kuja kukubatiza?

2. Je,Yesu ndiye alikufungisha ndoa au ndiye atakayefungisha ndoa yako? Kama wachungaji wako hawajawahi kukanyaga Mbinguni na bado walikubatiza ili kukuondolea dhambi ya asili na dhambi zingine, inashindikana nini kwa Padri kumuondolea mkatoliki dhambi?

3. Je,kuna Timu ya Malaika imepiga kambi pale Magomeni, Mwembechai au Chang'ombe, ambayo inafanya kazi ya kuwapunga pepo waprotestanti?
 
Mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, naye ni Yesu kristo si mtume wala nabii. Hivyo mwanadamu ukimkosea Mungu mwenye uwezo wa kukupatanisha wewe na Mungu ni mmoja tu.
1tim 2:5

Sent using Jamii Forums mobile app

Yesu alimbatiza nani alipokuwapo hapa duniani?Je,kwa kutofanya hivyo ina maana si yeye anayewaondolea watu dhambi zao kwa njia ya ubatizo? Hivi ndio kwanza unajifunza reasoning?
 
Biblia ndio katiba yetu Wakristo....

Nipe Mstari unaosema ni Marufuku mapadre kuondolea dhambi ...mbona ni rahisi tuu.....

Usinipotezee muda

Komaa naye huyo asitake kutuletea habari za Bibi yake, mganga wa kidini na ushirikina wa kiimani,Ellen White, hapa.
 
Acha kuchanganya mambo mkuu kubatiza kwenye maandiko wapo mitume waliobatiza wanafunzi wa Yesu na kina Filipo hao tunasoma habari zao kuwa waliobatiza
Kuhusu kuombea mapepo hayo ni mamlaka Yesu mwenye aliyatoa kwa mitume tunasoma katika maandiko je habari ya kutubu dhambi kwa binadamu tunazisoma kitabu gani
Give me the verse
 
Mimi sio mkatoliki na hata ningekuwa mkatoliki kamwe nisingekwenda kwa binadamu/Padri mwenye mwili wa nyama kama wangu kuungama dhambi.

Dhambi yako uliyoirithi toka kwa Adamu na Eva iliondolewa kwa njia gani? Yesu ndiye aliyeshuka na kukubatiza?
 

Yesu alipoagiza hivi unafikiria alikuwa "amelewa"?

"19 Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, “Amani kwenu!” 20 Alipokwisha sema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Basi, hao wanafunzi wakafurahi mno kumwona Bwana. 21 Yesu akawaambia tena, “Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma nyinyi.” 22 Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.” (Yohana 20:19-23)
 
Yesu alimbatiza nani alipokuwapo hapa duniani? Je,kwa kutofanya hivyo ina maana yeye anayewaondolea watu dhambi zao kwa njia ya ubatizo? Hivi ndio kwanza unajifunza reasoning?

Wewe ukibatizwa anayekuondolea dhambi ni aliyekubatiza au ni Yesu?
 
Nyie hamjasoma hilo bandiko...I'm sure 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lete mistari ya biblia sio porojo za mawazo yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…