Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Katika paragraph ya mwisho hapo umesema wamepewa mamlaka ya kuamua kwamba wasamehe dhambi au wasisamehe na wasiposamehe basi hizo dhambi hazitasamehewa, ambatanisha ni kifungu cha maandiko ili usiongee maneno matupu kudhibitisha hoja yako. Toa kifungu katika biblia kinachosema msipowasamehe hawasamehewi.

1. Umesoma mada nzima na hujaona hicho kifungu husika?

2. Kuyaelewa maandiko matakatifu hakuko katika kunukuliwa kwake tu.Ingalikuwa mambo yako hivyo, basi William Miller asingaliiletea Dunia maangamizi kwa kunukuu kifungu toka aya ya Ufunuo wa Yohana na kuitafisri kwamba siku 2300 zilimaanisha miaka 2300 ambayo ingaliishia mwaka 1843/1844 ambapo yeye wafuasi wake wangalimshuhudia Yesu akishuka duniani.
 
Nataka fungu lolote kutoka kwenye maandiko matakatifu yanayo ruhusu hicho unachokitetea na mimi nitakupa verse zinazopingana mnachokiamini ni sahihi
Sasa pitia mada yote tena kisha rudi hapa kuniuliza swali.....


Ungesoma mada yote usingeniuliza swali la kipuuzi kama hilo
 
Samahani mkuu Am a theologian by the way Siku zote naamini katika maandiko
Tangu lini mdhambi akasamehe wadhambi? Tangu lini kipofu akamwongoza kipofu mwenzake give me a biblical verse that a proves that theory ya Padre kusamehe

1. Kwani wewe ulibatiwa na "Mtakatifu" Ellen White? Watakatifu (Wachungaji Ellen White, William Miller, Hiram Edson,James White), ndio walioshuka kutoka Mbinguni kuja kukubatiza?

2. Je,Yesu ndiye alikufungisha ndoa au ndiye atakayefungisha ndoa yako? Kama wachungaji wako hawajawahi kukanyaga Mbinguni na bado walikubatiza ili kukuondolea dhambi ya asili na dhambi zingine, inashindikana nini kwa Padri kumuondolea mkatoliki dhambi?

3. Je,kuna Timu ya Malaika imepiga kambi pale Magomeni, Mwembechai au Chang'ombe, ambayo inafanya kazi ya kuwapunga pepo waprotestanti?
 
Mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, naye ni Yesu kristo si mtume wala nabii. Hivyo mwanadamu ukimkosea Mungu mwenye uwezo wa kukupatanisha wewe na Mungu ni mmoja tu.
1tim 2:5

Sent using Jamii Forums mobile app

Yesu alimbatiza nani alipokuwapo hapa duniani?Je,kwa kutofanya hivyo ina maana si yeye anayewaondolea watu dhambi zao kwa njia ya ubatizo? Hivi ndio kwanza unajifunza reasoning?
 
Biblia ndio katiba yetu Wakristo....

Nipe Mstari unaosema ni Marufuku mapadre kuondolea dhambi ...mbona ni rahisi tuu.....

Usinipotezee muda

Komaa naye huyo asitake kutuletea habari za Bibi yake, mganga wa kidini na ushirikina wa kiimani,Ellen White, hapa.
 
1. Kwani wewe ulibatiwa na "Mtakatifu" Ellen White? Watakatifu (Wachungaji Ellen White, William Miller, Hiram Edson,James White), ndio walioshuka kuja kukubatiza?

2. Je,Yesu ndiye alikufungisha ndoa au ndiye atakayefungisha ndoa yako? Kama wachungaji wako hawajawahi kukanyaga duniani na bado walikubatiza ili kukuondolea dhambi ya asili na dhambi zingine wewe,inashindikana nini kwa Padri kumuondolea mkatoliki dhambi?

3. Je,kuna Timu ya Malaika imepiga kambi pale Magomeni, Mwembechai au Chang'ombe, ambayo inafanya kazi ya kuwapunga pepo waprotestanti?
Acha kuchanganya mambo mkuu kubatiza kwenye maandiko wapo mitume waliobatiza wanafunzi wa Yesu na kina Filipo hao tunasoma habari zao kuwa waliobatiza
Kuhusu kuombea mapepo hayo ni mamlaka Yesu mwenye aliyatoa kwa mitume tunasoma katika maandiko je habari ya kutubu dhambi kwa binadamu tunazisoma kitabu gani
Give me the verse
 
Mimi sio mkatoliki na hata ningekuwa mkatoliki kamwe nisingekwenda kwa binadamu/Padri mwenye mwili wa nyama kama wangu kuungama dhambi.

Dhambi yako uliyoirithi toka kwa Adamu na Eva iliondolewa kwa njia gani? Yesu ndiye aliyeshuka na kukubatiza?
 
Acha kuchanganya mambo mkuu kubatiza kwenye maandiko wapo mitume waliobatiza wanafunzi wa Yesu na kina Filipo hao tunasoma habari zao kuwa waliobatiza
Kuhusu kuombea mapepo hayo ni mamlaka Yesu mwenye aliyatoa kwa mitume tunasoma katika maandiko je habari ya kutubu dhambi kwa binadamu tunazisoma kitabu gani
Give me the verse

Yesu alipoagiza hivi unafikiria alikuwa "amelewa"?

"19 Ilikuwa jioni ya siku hiyo ya Jumapili. Wanafunzi walikuwa wamekutana pamoja ndani ya nyumba, na milango ilikuwa imefungwa kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi. Basi, Yesu akaja, akasimama kati yao, akawaambia, “Amani kwenu!” 20 Alipokwisha sema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Basi, hao wanafunzi wakafurahi mno kumwona Bwana. 21 Yesu akawaambia tena, “Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma nyinyi.” 22 Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.” (Yohana 20:19-23)
 
Yesu alimbatiza nani alipokuwapo hapa duniani? Je,kwa kutofanya hivyo ina maana yeye anayewaondolea watu dhambi zao kwa njia ya ubatizo? Hivi ndio kwanza unajifunza reasoning?

Wewe ukibatizwa anayekuondolea dhambi ni aliyekubatiza au ni Yesu?
 
Wakatoliki mkinipa andiko lolote kwenye Biblia linalosema kwamba padri ana mamlaka ya kusamehe dhambi Nampa 1M cash
Huwezi kuniambia padri ambaye ni mdhambi kama mimi aje amsamehe dhambi zangu The Holy Bible says for all have sinned and fallen short of the glory of God.
Naona umeandika makala ndeeefu isiyo na Bible proof hata moja
Ndugu zangu RC ni wakati wa kuifanya Biblia andiko kuu kuliko hao mapadri wenu ambao wengine wana scandal za kubaka kulawiti na Kusapoti usho**
Nyie hamjasoma hilo bandiko...I'm sure 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitaipinga hoja yako mkuu kupitia kipengele chako cha mada chenye maneno "Historia ya maungamo ya dhambi katika agano la kale"

Nianze kwa kukupa history kidogo. Mara baada ya anguko la Adamu na Hawa pale Eden Mungu alikuwa ameshaanda mpango wa wokovu wa Mwanadamu ndiyo maana utaona kuna mnyama alichinjwa pale ili wapate nguo za kuficha uchi wao lkn halikuwa lengo hasa Ila alichinjwa ili awe mbadala wao kwa dhambi walizotenda ndiyo maana hawakufa kama sheria isemavyo ya mshahara wa dhambi ni mauti.

Kutokea hapo utaona ibada za kafara kupitia wanyama zikianza kwa kila aliyekuwa akitenda dhambi na hata habari ya ukuhani pia baadaye hema ya kukutania ilipoanzishwa katika kitabu cha kutoka 25 agizo la ujenzi wa hema hiyo lilipotolewa.

Katika ujenzi ule Mungu anamwambia musa kuwa hema ile itakuwa mfano wa ile ya mbinguni kwa hiyo note hata mbinguni kuna huduma ya upatanisho kupitia kuhani

Turudi kwa mada hema ya kukutania Ilikuwa na sehemu kuu tatu uwa wa nje, patakatifu na patakatifu pa patakatifu ambapo ktk uwa wa nje ndiyo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa ambapo mdhambi alitwaa kondoo kama mbadala wake na kwenda naye kwa kuhani ambaye aliact kama mpatanishi baina ya mwanadamu mdhambi na Mungu ambapo aliungama dhambi zake kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kondoo kama namna ya kuhamisha dhambi kutoka kwake kwenda kwa kondoo kisha alimchinja na kuhani kukinga damu na kuingia nayo kwenye chumba cha pili cha patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wakati kondoo akiteketezwa katika ua wa nje huu ndiyo ulikuwa utaratibu wa wokovu ulioandaliwa na Mungu kabla ya Kristo kuja duniani

Baada ya Kristo na kufa kama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu yohana 1:29 na kufa pale msalabani habari za kwenda kuungama kwa kuhani zilikoma au huduma za kikuhani na utoaji kafara ulikwisha maana huduma ile ilikuwa kivuli kumuwakilisha Kristo na sasa Kristo ameshakuja hakuna haja tena kwenda kwa mwanadamu kuungama wakati Kristo yupo

Kwa hiyo hoja yako ya kuungama kwa padri ni kutaka kuturudisha kwa huduma ya kikuhani ya mwanadamu ambayo ni hatari sana maana unapinga kwamba Kristo bado hajafa kwa ajili ya dhambi na wewe unageuka kuwa mpinga Kristo

Leo hatuna haja ya kuungama kwa mwanadamu tena maana tunaye Kristo mwombezi wetu kuhani asiyepatikana na mauti anayehudumu ktk hekalu lisilofanywa kwa mikono ya mwanadamu huyo pekee astahili kutuombea msamaha kwa Mungu Baba na si mwingine yoyote
Lete mistari ya biblia sio porojo za mawazo yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom