Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

EBR. :10:25
wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Ukiwa na lingine utaniquote tena
 
Nipe kifungu cha biblia kinachosema ubatizo ni function ya quantity badala ya quality.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi umelewa au umekula maharagwe ya kutoka Afghanistani? Mimi nimekuambia kwamba ubatizo ni function ya "Quality" na sio "Quantity". Na nikasema kama unadhani ubatizo ni function ya Quantity kawahini kuweka order za sabuni za kufulia na kuogea za OMO na Mshindi viwandani.Upo?
 
Mi mifano yako yote Hanna padri naona yesu ndo anaefanya na kusamehe sasa apo sijui padre ye anaingiaje kuchukua nafasi ya yesu
 
Unataka aseme uongo wewe ulishaona kwenye biblia neno padre?

Kapingane na Waraka wa Yakobo 5:14:

“14 Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.”

Neno “Wazee wa Kanisa” linamaanisha Kasisi.Biblia ya Kiswahili imejipatia neno “Wazee wa Kanisa” kutokana na neno la Kigriki (Lugha ya Agano Jipya) Presbyter lenye kumaanisha Kasisi au Baba au Padri.

Padri maana yake ni baba. Kumbe Yakobo anapowausia watu kuungama dhambi zao, anamaanisha wafanye hivyo mbele ya Mapadri ambao wao ndio wanapatiwa uwezo huo na Kristu.Kumbe, Kristu anauhisha mahusiano kati ya Mungu na mwanadamu kupitia kwa padri.

Huwezi kuwa umedandia maandiko matakatifu kwa mbele na ukafanikiwa kuyaelewa haya mambo.Basi, Imekula kwenu mazima.
 

Kwani lini ulienda kuungama kwa Padri akakuondolea dhambi zako kwa jina lake badala ya lile la "Kwa Jina la Baba,Mwana na Roho Mtakatifu"? Hivi tunajadiliana na "msukule"?

Haya ndiyo madhara ya watu wanaokaa muda wote wanaang'aza macho angani kuona kama Yesu anarudi upesi.Akili zako hazipo kabisa kwenye mjadala bali ziko zinasikilizia sasa huko nje kama kuna vishindo vya Yesu kurudi.
 
Naomba uthibitisho wa maaandiko palipo andikwa kuungama dhambi kwa padre.
 

1. Hivi Lugha ya kiingereza uliipatia wapi? Kwa Rasi Simba au kwa nani? How could the Deciples be able to pronounce the sins that are forgiven if they are in advance not aware of the particular sins?

2. Yaani umeenda kukopi ready made answers kutoka mitandao ya Ellen White bila hata kufanya editing na hivi ukashindwa kuona phrase ya kukunyongea? Angalia sasa unavyoumbuka.Unachokisema kwa majibu yako hayo ya kukariri "It is saying that Christian disciples have the authority to pronounce what sins "have been forgiven " yana tofauti gani na wanachofundisha wakatoliki?
 
imeandikwa wapi aliwapa mapadre mamlaka ya kusamehe dhambi
21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.
Yohana 20 :21

22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
Yohana 20 :22

23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
Yohana 20 :23



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubatizo huondoa dhambi na maungamo huondoa dhambi.Kwani hujawahi kujibatiza mwenyewe kwa maana si unajua maji ndiyo yanaondoa dhambi na unafahamu fika yanapatika kwenye mito na maziwa au baharini?
Kama unaamini kwamba ubatizo unaondoa dhambi ni kwanini mnawabatiza watoto wadogo??? Huwa wana dhambi gani hasa???

NB:
UBATIZO HAUONDOI DHAMBI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…