Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Wakatoliki wao wanatumia Kristu na sio kristo, nilishawahi kuona waneandika kwenye janisa lao nikahisi ni typing error kumbe ndio uhalisia

Sent using Jamii Forums mobile app

Aliyekufundisha hivyo, alisoma Biblia kwa kurukaruka. Maneno "Kristo" na "Kristu" ni maneno yenye maana sawa tu.La kwanza limetoholewa kutoka Kigriki na la pili limetoholewa kutoka Kilatini.
 
Aliyekufundisha hivyo, alisoma Biblia kwa kurukaruka. Maneno "Kristo" na "Kristu" ni maneno yenye maana sawa tu.La kwanza limetoholewa kutoka Kigriki na la pili limetoholewa kutoka Kilatini.
Aliyenifundisha biblia nae kaisoma biblia hiyo hiyo na hakuona sehemu imeandikwa kristu ndio maana nikafuata mafundisho yake ya kufahamu kristo na si kristu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyenifundisha biblia nae kaisoma biblia hiyo hiyo na hakuona sehemu imeandikwa kristu ndio maana nikafuata mafundisho yake ya kufahamu kristo na si kristu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Basi, komaa naye huyo huyo maana anafahamu zaidi.Nina imani kuna siku atakufundisha kwamba Jua huzama kwenye matope meusi.
 
Mbona hawakatai kubatizwa na wachungaji?si wajibatize wenyewe mbona hawakatai kufungishwa ndoa zao na wachungaji?mbona wanakwenda kuombewa na wachungaji?mbona wanapewa ubarikio/kipaimara na maaskofu/wachungaji?

Sent using Jamii Forums mobile app

1. Ndio kule kule tunakokusema kwamba waprotestanti wanasoma maandiko Matakatifu kwa kurukaruka na ni wapinga Kristo.

2. Mtu anakataa nyama ya Nguruwe ikiwa imekaangwa lakini anakubali ikiwa katika mfumo wa Unga kwenye kopo.Au mtu anakataa Pombe kwenye Chupa ya Serengeti lakini anakubali kuwekewa kwenye mwili wake na daktari akiwa anachukuliwa damu au baada ya. Au mtu anaikataa Pombe lakini anaikubali awekewe ndugu marehemu wake Mochwari ili mwili wake usioze. Kama Padri hana uwezo wa kuwaondolea dhambi kwa sababu sio Mungu basi, vile vile hana uwezo uwezo wa kuwaondolea dhambi kwa njia ya ubatizo. Na kuanzia sasa wapange foleni wamusubirie Mungu awabatize au wawe wanajibatiza wenyewe vyumbani kwao.
 
Waoga wa kusoma biblia

1. Kama ni waoga wa kusoma basi, wasiwasumbue wanaosoma.

2. Kama "madishi" yao ya ufunuo wa Biblia yaliyumbishwa na viongozi wao, waliowaaanzishia madhehebu, basi wakae kimya. Kukaa kimya nako ni njia ya kuonyesha kwamba upo na sio lazima ubweke ubweke wakati unachokibwekea ni utumbo mtupu.
 
I agree with u..Asiekubaliana na ulichokiandika ana lake jambo..Tunakimbilia ulinzi wako?
 
Mimi naona wote mpo sahihi, kuungama kwa padri kupo, lakini siyo lazima.

Unajua, kuungama kwa padri ilikuwa hivi, unaenda kwa padri na kutaja dhambi zako zote ukimaliza yeye huingia mahali patakatifu yaani nyuma ya pazia na kusali kwa niaba yako na kukuombea.

Yesu alipokata roho, pazia lilipasuka katikati, ikimaanisha, swala la kusema lazima uende kutubu na kuombewa na padri nyuma ya pazia hakuna ulazima huo tena.

Yeye atakusikia popote ulipo. Ukitaka kwenda kwa padri nenda hujakatazwa, lakini siyo lazima kama ilivyokuwa kabla ya yeye kusulubiwa, kufa na kufufuka kwa ajili yetu.

Hizo kelele nyingine mnazopiga ni kutokujua tu.
 
MANTIKI YA WAKATOLIKI KUUNGAMA DHAMBI KWA PADRI

Kanisa Katoliki, linaazima maelekezo ya kuungama dhambi kwa Padri kutoka maneno ya Yesu mwenyewe. Yesu angalimaanisha mtu kuungama dhambi zake bila kuzieleza basi, kusingalikuwa na uwezekano wa kushindwa watu wengine kusamehewa dhambi zao. Kwa mantiki ya kawaida, huwezi kumkatalia mtu jambo au ombi ambalo hulijui ni nini? Mantiki Ya pili, ya kulazimika wadhambi kusema au kutaja dhambi zao mbele ya Mitume,ni kwa sababu Mitume kama binadamu hawakuwa uwezo wa kusoma mioyo ya waungamaji na kuona humo dhambi zao ili waweze kusamehewa.

Kumbe, kwa maneno “…msipowasamehe, hawasamehewi”, Yesu anawaelekeza Mitume kwamba baada ya kusikiliza dhambi za waungama, kuna mazingira dhambi husika zinaweza zisiondolewe na mara watakapofanya hivyo, basi Mungu naye anakuwa ameridhia maamuzi hayo.
.



Katika paragraph ya mwisho hapo umesema wamepewa mamlaka ya kuamua kwamba wasamehe dhambi au wasisamehe na wasiposamehe basi hizo dhambi hazitasamehewa, ambatanisha ni kifungu cha maandiko ili usiongee maneno matupu kudhibitisha hoja yako. Toa kifungu katika biblia kinachosema msipowasamehe hawasamehewi.
 
Kuna mtu akinambia wenye biblia mi binafsi sijaona neno padre, kupitia hapo tu padre simtambui. Au padre ndo mchungaji??

Nikakosa jibu.


OK Nije kwenye mada ya kuungama kwa padre,swali langu ni hili, nikiungama kwa padre Mwenye dhambi nasamehewa??

PILI, Niliwahi kuungama kwa padre,huku padre akiwa anasinzia,,niligundua baada ya kumaliza ye akiwa kasinzia badae akashtuka akanipa sala za kusali,,je pale nilisamehewa?? Mana msameheji alilala

TATU, padre akiwa kanitongoza naweza kwenda kuungama kwake??
Kama ulimkatalia lazima ukaungame la sivyo unampatia ili mmalizane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu hawapaswi kuungama kwa padri. Watu wanapaswa kuungama dhambi zao kwa Mungu.
Baada ya Yesu kufa msalabani Mungu alifungua njia ya watu kumwendea yeye kwa sala na toba.

Baada ya mtu kumkiri Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wake anakuwa amesha okolewa.sasa anakuwa na namba ya simu kupiga kwa Mungu moja kwa moja. Haitaji tena kupiga customer care au operator amuunganishe.

wali: "Ni nini ilikuwa umuhimu wa hekalu pazia kuwa vipande viwili wakati Yesu alikufa?"

Jibu: Wakati wa uhai wa Yesu, hekalu takatifu katika Yerusalemu lilikuwa ndilo nguzo muhimu katika maisha ya kidini ya Kiyahudi. Hekalu ilikuwa mahali ambapo dhabihu za wanyama zilikuwa zinafanyiwa na ibada kwa mujibu wa sheria ya Musa iliyofuatwa kwa uaminifu. Waebrania 9: 1-9 inatuambia kwamba katika hekalu pazia ilitenganisha pahali takatifu zaidi ya patakatifu – mahali ambapo uwepo wa mungu uishi ulimwenguni- kutoka kwa mahali pengine Hekaluni ambapo watu waliishi. Hii iliashiria kuwa binadamu alitenganishwa kutoka Mungu na dhambi (Isaya 59: 1-2). Ni kuhani mkuu tu aliyeruhusiwa kupita zaidi ya hii pazia mara moja kila mwaka (Kutoka 30:10, Waebrania 9: 7) aingie katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya waisraeli wote na kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zao (Mambo ya Walawi 16).

Hekalu la Sulemani lilikuwa dhiraa 30 kuelekea juu (1 Wafalme 6: 2), lakini Herode alikuwa amezidisha urefu hadi dhiraa 40, kulingana na maandiko ya Josephus,mhisitoria Myahudi wa karne ya kwanza. Hakuna uhakika kwa kipimo halisi cha dhiraa moja, lakini ni salama kudhani kwamba pazia hili lilikuwa mahali fulani karibu futi 60 juu. Josephus pia anatuambia kwamba pazia hili lilikuwa na upana wa inchi nne na kwamba farasi hata wafungwe kwa kila upande hawangeweza kuirarua dhiraa hii . Kitabu cha Kutoka kinafundisha kwamba pazia hii pana iliundwa kwa mtindo kutoka samawati( buluu), zambarau, na nyekundu, na kitani kizuri cha kusokotwa.

Ukubwa na unene wa pazia unafanya matukio yanayotokea wakati wa kifo cha Yesu juu ya msalaba kuwa wa maana sana. "Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka."(Mathayo 27: 50-51a).

Hivyo, je,tunafanya nini kwa hili? Ni umuhimu gani dhiraa hii ilyopasuka inayo kwetu siku hizi? Zaidi ya yote, kuraruriwa kwa dhiraa wakati wa kifo cha Yesu kuliashiria kidrama kwamba kafara yake, kumwaga damu yake mwenyewe,kulikuwa upatanisho wa kutosha kwa ajili ya dhambi.Kuliashiria kwamba sasa njia ya kuingia Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa wazi kwa watu wote, kwa wakati wote, Wayahudi na Mataifa.

Wakati Yesu alikufa, dhiraa iliraruka, na Mungu akatoka mahali pale kwamba kamwe hangeishi tenai katika hekalu zilizojengwa na binadamu (Matendo 17:24). Mungu alikuwa amemalizana na hekalu hilo na mfumo wake wa kidini, na hekalu na Yerusalemu ziliachwa "zikiuzunika kwa ukiwa" (kuharibiwa na Warumi) katika mwaka 70 A.D., tu kama Yesu alitabiri katika Luka 13:35. Bora tu Hekalu lilisimama, liliashiria kuendelea kwa Agano la Kale. Waebrania 9: 8-9 inarejelea umri uliokuwa unapita mara tu agano jipya liliimarishwa (Waebrania 8:13).

Kwa maana, dhiraa iliashiria Kristo mwenyewe kama njia ya pekee kwenda kwa Baba (Yohana 14: 6). Hii imeonyeshwa kwa ukweli kwamba kuhani mkuu alipaswa kuingia Patakatifu pa Patakatifu kupitia kwa dhiraa . Sasa Kristo ni Kuhani wetu mkuu zaidi, na kama waumini katika kazi yake iliyokamilika,tunashiriki katika Ukuhani wake bora.Tunaweza sasa kuingia Patakatifu pa Patakatifu kupitia kwake. Waebrania 10: 19-20 inasema kwamba “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia ilyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia , yaani, mwili wake."Tunaona mwili wa Yesu ukiraruriwa kwa ajili yetu tu kama alivyorarua pazia kwa ajili yetu.

Pazia kupasuliwa kutoka juu hadi chini ni ukweli wa hisitoria. Umuhimu mkubwa wa tukio hili umeelezewa kwa undani kwa utukufu katika Waebrania. Mambo ya hekalu yaliashiria mambo ambayo yangekuja, na yote yatuashiria kwa Yesu Kristo. Alikuwa pazia kwa Patakatifu pa Patakatifu, na kupitia kifo chake waaminifu sasa wanaweza kumpata Mungu bila gharama.

Pazia katika hekalu ilikuwa ukumbusho wa mara kwa mara kwamba dhambi ilimfanya binadamu kutofaa kwa uwepo wa Mungu. Ukweli kwamba sadaka ya dhambi ilitolewa kila mwaka na mara kwa mara dhabihu zingine zilirudiwa kila siku ilionyesha bayana kwamba dhambi kwa kweli haingeweza kupatanishwa kwa au kufutika na sadaka za wanyama tu. Yesu Kristo,kupitia kwa kifo chake,ameondoa vikwazo vilivyo kati ya Mungu na mwanadamu, na sasa tunaweza kumkaribia kwa kujiamini na ujasiri (Waebrania 4: 14-16).
 
1.Kwani umeambiwa lazima uende kwa padri yule yule tu? Ndivyo kanisa Katoliki linavyofundisha?

2. Kwa nini unauona tu upungufu wa Mapadri katika kuungama dhambi ila kukubatiza bado unaendelea kwenda kwao na bado hata watoto wako bado unampelekea padri yule yule?

3. Mtu yeyote "anayemtunishia" Padri kuungama dhambi hana tofauti na Adamu na Eva kutokuwa tayari kukiri makosa yao na badala yake waliishia kutafuta visingizio.Ni dalili ya kukosa unyenyekevu.Ni dalili ya kujiona sisi tunafahamu zaidi kuliko wengine au kwamba sisin tuna hadhi sana kuliko wengine.
Mapadri hawahawa waosifika kwa kuwazibua watoto mitaro afu ndo haohao wanaondoa dhambi?

Kweli imani zá watu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Ndio kule kule tunakokusema kwamba waprotestanti wanasoma maandiko Matakatifu kwa kurukaruka na ni wapinga Kristo.

2. Mtu anakataa nyama ya Nguruwe ikiwa imekaangwa lakini anakubali ikiwa katika mfumo wa Unga kwenye kopo.Au mtu anakataa Pombe kwenye Chupa ya Serengeti lakini anakubali kuwekewa kwenye mwili wake na daktari akiwa anachukuliwa damu au baada ya. Au mtu anaikataa Pombe lakini anaikubali awekewe ndugu marehemu wake Mochwari ili mwili wake usioze. Kama Padri hana uwezo wa kuwaondolea dhambi kwa sababu sio Mungu basi, vile vile hana uwezo uwezo wa kuwaondolea dhambi kwa njia ya ubatizo. Na kuanzia sasa wapange foleni wamusubirie Mungu awabatize au wawe wanajibatiza wenyewe vyumbani kwao.
Mwenye dhambi hawezi ondoa dhambi zá mwenzake.

Ukatoliki comedi zaidi.

Nilizaliwa na kukulia humo. Mjadala wa comedi zá wakatoliki JF hawezi tosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani ndio nasema watu tuna matatizo ya kuchakata maudhui. Yesu kwa mfano huo alitaka kufundisha jinsi ya watu tunavyoweza kujiona wakamilifu na wengine wanaotambua kwamba ni wakosefu na hivi wanastahili msamaha.Ingalikuwa ni hivyo kwamba hakuna haja ya kuungama dhambi basi Yesu asingaliweza kuacha huo muundombinu wa kuwaondolea watu dhambi. Mungu hawezi kujipinga hata kidogo.
Kwa hiyo nikiwa sehemu ambako hakuna padri siwezi kuungama nikasamehewa?
halafu kwenye huo mfano nataka uniambie kwanini huyo jamaa alisamehewa bila uwepo wa padri?usiniletee ngonjera
 
Back
Top Bottom