Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Waweza nionesha alipokatazwa....
unazurula ktkt ya poli ww anaesamehe Dhambi ni YESU pekee hakuna mwanadamu mwenye uwezo huo TANGU kuumbwa kwa Dunia mpaka leo

kuhani wetu alie baki ni yesu kristo tu anaetuombea kila wakati

ukinanmbia mapadiri ni makuhani unajidanganya mwenyewe ................husamehe dhambi basi jua kama ulienda kuwapigia magoti wakusamehe umebugi nenda piga mwenyewe magoti omba toba kwa MUNGU peke yako
 
Mimi naona wote mpo sahihi, kuungama kwa padri kupo, lakini siyo lazima.

Unajua, kuungama kwa padri ilikuwa hivi, unaenda kwa padri na kutaja dhambi zako zote ukimaliza yeye huingia mahali patakatifu yaani nyuma ya pazia na kusali kwa niaba yako na kukuombea.

Yesu alipokata roho, pazia lilipasuka katikati, ikimaanisha, swala la kusema lazima uende kutubu na kuombewa na padri nyuma ya pazia hakuna ulazima huo tena.

Yeye atakusikia popote ulipo. Ukitaka kwenda kwa padri nenda hujakatazwa, lakini siyo lazima kama ilivyokuwa kabla ya yeye kusulubiwa, kufa na kufufuka kwa ajili yetu.

Hizo kelele nyingine mnazopiga ni kutokujua tu.

1. Mtizamo wako huo ungalikuwa sahihi iwapo maneno ya "Endeni mkawaondolee watu dhambi...na wowote mtakaowafungia dhambi wamefungiwa na wowote ambao mngaliwafungia dhambi wamefungiwa" yangalitamkwa kabla ya kifo chake Yesu Kristu(kabla ya hilo pazia la Hekalu halijapasuka).

2. Na nimeeleza katika uzi mama ni kwa nini Yesu alitoa mamlaka hayo ya kuondoa dhambi kwa Mitume baada ya kifo chake na si kabla ya hapo.Mantiki ni kwamba Yesu asingaliweza kuwapa watu uwezo huo wa kuondoa dhambi wakati yeye anayeondoa dhambi angalipo hapa duniani.Kumbe, Yesu kutoa mamlaka ya kuondoa dhambi baada ya yeye kuondoka ilikuwa ni kukasimisha mamlaka hayo kwa Mitume.Kwamba Mitume na Mahalifa wao wawaondolee watu dhambi kwa niaba yake.
 
Mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, naye ni Yesu kristo si mtume wala nabii. Hivyo mwanadamu ukimkosea Mungu mwenye uwezo wa kukupatanisha wewe na Mungu ni mmoja tu.
1tim 2:5

Nimekuuliza waweza nionesha palipokatazwa...??? Au lugha inakuwa ngumu....??
 
Ukishapinga kikamilifu kimantiki uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote, aliyeumba ulimwengu, hizi habari za uongo mdogomdogo haziwezi kukusumbua.
 
Mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, naye ni Yesu kristo si mtume wala nabii. Hivyo mwanadamu ukimkosea Mungu mwenye uwezo wa kukupatanisha wewe na Mungu ni mmoja tu.
1tim 2:5

Nimekuuliza waweza nionesha palipokatazwa...??? Au lugha inakuwa ngumu....??
 
unazurula ktkt ya poli ww anaesamehe Dhambi ni YESU pekee hakuna mwanadamu mwenye uwezo huo TANGU kuumbwa kwa Dunia mpaka leo

kuhani wetu alie baki ni yesu kristo tu anaetuombea kila wakati

ukinanmbia mapadiri ni makuhani unajidanganya mwenyewe ................husamehe dhambi basi jua kama ulienda kuwapigia magoti wakusamehe umebugi nenda piga mwenyewe magoti omba toba kwa MUNGU peke yako
Bado hujajibu swali nililokuuliza...

Ukipata jibu nitaku-quote post yako...
 
Nimekuuliza waweza nionesha palipokatazwa...??? Au lugha inakuwa ngumu....??
Sasa unataka andiko gani tena au huelewi? Anayepatanisha wanadamu na Mungu ni mmoja tu naye ni Yesu kristo na andiko nimekuwekea hapo. Hakuna mwingine anayepaswa kupatanisha wanadamu na Mungu zaidi ya huyo mmoja aliyetajwa hapo.
Toa andiko linalosema padre anatupatanisha sisi wanadamu na Mungu pale tunapokosea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pitia hapa

Yohana 20:22-23
Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.
 
Nataka andiko la kukanusha kwamba ni marufuku mapadre(Makuhani) kuwaondokea watu dhambi ..
Naona unakaza ubongo mda wote unajinasibu kwamba hatutumii elimu zetu na wewe umeshindwa kuelewa hapo? Neno hilo limekua gumu kwako kulielewa? Neno kusema kwamba anayepatanisha kati ya mwanadamu na Mungu ni mmoja naye ni Yesu, huelewi kwamba akijitokea kiumbe mwingine kupatanisha huo upatanisho utakua ni batili? Au bado huelewi. Ukibeba imani tumia akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitaipinga hoja yako mkuu kupitia kipengele chako cha mada chenye maneno "Historia ya maungamo ya dhambi katika agano la kale"

Nianze kwa kukupa history kidogo. Mara baada ya anguko la Adamu na Hawa pale Eden Mungu alikuwa ameshaanda mpango wa wokovu wa Mwanadamu ndiyo maana utaona kuna mnyama alichinjwa pale ili wapate nguo za kuficha uchi wao lkn halikuwa lengo hasa Ila alichinjwa ili awe mbadala wao kwa dhambi walizotenda ndiyo maana hawakufa kama sheria isemavyo ya mshahara wa dhambi ni mauti.

Kutokea hapo utaona ibada za kafara kupitia wanyama zikianza kwa kila aliyekuwa akitenda dhambi na hata habari ya ukuhani pia baadaye hema ya kukutania ilipoanzishwa katika kitabu cha kutoka 25 agizo la ujenzi wa hema hiyo lilipotolewa.

Katika ujenzi ule Mungu anamwambia musa kuwa hema ile itakuwa mfano wa ile ya mbinguni kwa hiyo note hata mbinguni kuna huduma ya upatanisho kupitia kuhani

Turudi kwa mada hema ya kukutania Ilikuwa na sehemu kuu tatu uwa wa nje, patakatifu na patakatifu pa patakatifu ambapo ktk uwa wa nje ndiyo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa ambapo mdhambi alitwaa kondoo kama mbadala wake na kwenda naye kwa kuhani ambaye aliact kama mpatanishi baina ya mwanadamu mdhambi na Mungu ambapo aliungama dhambi zake kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kondoo kama namna ya kuhamisha dhambi kutoka kwake kwenda kwa kondoo kisha alimchinja na kuhani kukinga damu na kuingia nayo kwenye chumba cha pili cha patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wakati kondoo akiteketezwa katika ua wa nje huu ndiyo ulikuwa utaratibu wa wokovu ulioandaliwa na Mungu kabla ya Kristo kuja duniani

Baada ya Kristo na kufa kama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu yohana 1:29 na kufa pale msalabani habari za kwenda kuungama kwa kuhani zilikoma au huduma za kikuhani na utoaji kafara ulikwisha maana huduma ile ilikuwa kivuli kumuwakilisha Kristo na sasa Kristo ameshakuja hakuna haja tena kwenda kwa mwanadamu kuungama wakati Kristo yupo

Kwa hiyo hoja yako ya kuungama kwa padri ni kutaka kuturudisha kwa huduma ya kikuhani ya mwanadamu ambayo ni hatari sana maana unapinga kwamba Kristo bado hajafa kwa ajili ya dhambi na wewe unageuka kuwa mpinga Kristo

Leo hatuna haja ya kuungama kwa mwanadamu tena maana tunaye Kristo mwombezi wetu kuhani asiyepatikana na mauti anayehudumu ktk hekalu lisilofanywa kwa mikono ya mwanadamu huyo pekee astahili kutuombea msamaha kwa Mungu Baba na si mwingine yoyote
Unasema "Leo hatuna haja ya kuungama kwa Padre kwa sababu tunaye Yesu Kristo kuhani mkuu na mwombezi"

Sasa kwanini huwa unaenda kanisani na unasikiliza maubili na mafundisho ya watumishi hata usikae mwenyewe kwako ukaomba peke yako kama unajua na kuamni Yesu Kristo yupo na huitaji kuwategemea wanadamu au watumishi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakatoliki mkinipa andiko lolote kwenye Biblia linalosema kwamba padri ana mamlaka ya kusamehe dhambi Nampa 1M cash
Huwezi kuniambia padri ambaye ni mdhambi kama mimi aje amsamehe dhambi zangu The Holy Bible says for all have sinned and fallen short of the glory of God.
Naona umeandika makala ndeeefu isiyo na Bible proof hata moja
Ndugu zangu RC ni wakati wa kuifanya Biblia andiko kuu kuliko hao mapadri wenu ambao wengine wana scandal za kubaka kulawiti na Kusapoti usho**
 
Ukibeba imani tumia akili.
Kama wewe ulivyoshindwa kuitumia akili yako kuelewa mantiki ya mleta uzi sio...???

Hivyo wewe umebeba imani gani ilifunga akili yako kuelewa post wazi kabisa ilisheheni jadidi za biblia na kila aina ya vitamini na madini kwa ubongo..?
 
Wakatoliki mkinipa andiko lolote kwenye Biblia linalosema kwamba padri ana mamlaka ya kusamehe dhambi Nampa 1M cash
Ungesoma uzi wote ungeona majibu yapo....Swali alilouliza majibu yake yapo hapo mwanzo..

Au ndio unataka kututhibitishia msemo wetu pendea kuwa kuwa ukitaka kumificha mwafrika mwekee kitu kwenye maandishi...???

Kaa chini tulia soma Post yote kwa umakini
 
Huwezi kuniambia padri ambaye ni mdhambi kama mimi aje amsamehe dhambi zangu The Holy Bible says for all have sinned and fallen short of the glory of God.
Padre kuwa mdhambi hakumuondolei mamlaka yake ya kuondolea dhambi
..
 
Hakuna
Ungesoma uzi wote ungeona majibu yapo....Swali alilouliza majibu yake yapo hapo mwanzo..

Au ndio unataka kututhibitishia msemo wetu pendea kuwa kuwa ukitaka kumificha mwafrika mwekee kitu kwenye maandishi...???

Kaa chini tulia soma Post yote kwa umakini
Biblical verification yoyote that's what I demand nimesoma sijaona biblical proof
 
Naona umeandika makala ndeeefu isiyo na Bible proof hata moja
Kweli...??? Au umeamua kujitoa ufahamu ...

Mbona thread yote ina nukulu ya Biblia mwanzo mwisho .....tena tukipewa chanzo cha sakramenti ya upatanisho toka agano la Kale....
 
Padre kuwa mdhambi hakumuondolei mamlaka yake ya kuondolea dhambi
..
Samahani mkuu Am a theologian by the way Siku zote naamini katika maandiko
Tangu lini mdhambi akasamehe wadhambi? Tangu lini kipofu akamwongoza kipofu mwenzake give me a biblical verse that a proves that theory ya Padre kusamehe
 
Back
Top Bottom