Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Status
Not open for further replies.

na hapo ndo kwenye tatizo. Point yako ya 2. Ikianzishwa kisheria tayari itakua imeingiliana na sheria za nchi yetu..nikimaanisha kua nchi yetu haina dini na hivyo haifungamani na umoja wowote wa kidini, ila kinchi-kimataifa inafungana na umoja wowote ule ambao hauna misingi ya kidini. Ndo maana ikasema wananchi na jumuiya zao za kidini ruksa kujiunga na jumuiya za kimataifa zenye misingi ya dini. Hope U get my point.
 
Sijui nieleze vipi ili nieleweke vema. Nitajaribu.
Sijakataa ndoa au mirathi kama ibada. Hoja inayotakiwa kujengwa ni kuweka taratibu za mirathi ziwiane na za ndoa ambayo tayari inakubalika kisheria. Taratibu hizo ni pamoja na kuwa na mtu au watu watakaoshughulikia. Hii ndio hoja inayotakiwa kuelezwa ili kila mmoja aelewe.

Kosa kubwa ni kuwa nguvu ya hoja inapotezwa na suala la uchangiaji. Na kwa bahati mbaya halielezwi kama uchangiaji tu bali linafungamanishwa na mambo mengine. Hapa hoja hugeuga na kuwa ' wao dhidi ya sisi'. Ni kutokana na kutoelewa ujenzi wa hoja jamii inachanganyikiwa kuwa waislam wanataka nini. Je wanataka mirathi katika mambo ya dini yao itambuliwe na ipewe nafasi au waislam wanataka kupata ruzuku kwasababu fulani anapata ruzuku. Ikifika hapo hoja inajiua yenyewe na watu wanaanza kuchangia mambo nje ya hoja.

Nitakupa mfano, lilipokuja suala la kadhi baadhi ya viongozi wa kiislam waisoelewa na wenye jazba wakaliongelea kama sharia ya dini.
Jamii nyingine ikaingiwa na hofu kuwa kwanini sharia itumike katika secular country. Zikazuka hoja za watu kukatwa mikono n.k. hali iliyopoteza kabisa hoja ya msingi.
Watu wakaelimishwa kuwa sio sharia in general bali sharia katika ndoa na mirathi na kuwa haitahusu makosa ya jinai.
Hapo wasio waislam wakaelewa na kusema hilo halina tabu kama watajitengenezea utaratibu wao. Na siku hizi hulisikii kwasababu limeelezwa kwa weledi na umma umelielewa.

Kosa lile lile linajirudia, badala ya watu kueleza umuhimu wa mirathi na ndoa kama vitu viwili katika kimoja, wamejikita katika kusema mbona ABC wanapata hiki. Sasa inaonekana suala si ibada bali kudai ruzuku. Ukiongelea mirathi na ndoa basi mweleshe asiyejua ufungamano wa vitu hivyo na sio kurukia mfumo kristo n.k. Hapa watu hawapambanishi simba na yanga.

Nasisitiza kuwa kama waislam wanaweza kufanya ibada zao bila msaada wa serikali sioni kwanini wasiombe suala la mirathi kama sehemu ya ibada likubaliwe kisheria kama sehemu ya ndoa tu na wajiwekee utaratibu wao wa kulisimamia wao wenyewe kama wanavosimamia ibada nyingine bila kuingiliwa na serikali.

Mwisho naomba unisome kama mchangiaji hilo la intellectual ni kubwa na inawezekana viatu hivyo siwezi kuvivaa, muhimu soma hoja
 

Hii "interllectuals" mi inaniacha hoi maana ukijaribu kuweka intellectual argument, kuna akina Anheuser wanaponda na kusema ni kimbelembele! Bora mleta mada aondoe hilo neno kwenye mada kuu!
 
Hii "interllectuals" mi inaniacha hoi maana ukijaribu kuweka intellectual argument, kuna akina Anheuse wanaponda na kusema ni kimbelembele! Bora mleta mada aondoe hilo neno kwenye mada kuu!

Wos ndio maana mchango wangu wa kwanza wenye hii mada niliadika hivi

Kwa point hiyo utaona mtu anadai kitu sababu yeye ni kundi fulani. Lakini huyo huyo hataiki kuchukua kuvua majoho ya dini na kuchukua postion ya serikali kujua kama angekwua yeye je ageruhusu mahakama kama hizo ngapi?

Anasema huwezi kulinganisha Wajaruo au na wahaya na uislam. Sababu yeye kwake uisam ni muhim zaidi. Anashindwa kutumia intellectual knowledge kuwa Tanzania kuna watu mila zao na desturi zao ni muhimu kama vile yeye kwake uislam ulivyo muhimu.

Nilitegeamea majibu ya" intellectual" anayetetea mahakama ya kadhi ni kuwa sawa ni haki hata kwa wajaruo, wahaya, na makabila mengine mahakama zao kuingizwa kwenye mfumo wa mahakam za serikali. Na iiwezekana wazee wa kijaruo mara nyingi nimesikia wanasuluisha migororo ya mirathi zao waingizwe kweye payroll ya Justice
 
Mimi napenda kujibu swali lako hivi: suala la mahakama ya kadhi ni suala linalohusu jumuiya ya waislam. hivyo si jambo la kikatiba kwa kuwa halina maslahi kwa watanzania wote. ndiyo maana Rais aliamua kulishughulikia kwani liko kwenye mamlaka yake. kitu kilichobaki ni kuangalia jinsi sheria za nchi zitakavyoweza kuhuisha suala hilo bila kuathiri uhuru wa kuabudu na kuingilia hazina ya taifa. pia sheria hizo itabidi ziache fulsa ili kama kuna dini nyingine zinataka masuala yao ambayo hayahusiani na jin
 
Kama kweli uanzishwaji wa mahakama za kadhi ni kwa ajili ya mirathi tu, basi hapo hakuna haja ya kupigishana kelele, msisitizo uelekezwe katika mafundisho ya dini juu ya namna ya kujenga familia na kugawanya mirathi.
Hapo tutakuwa tumepiga hatua katika kuzuia tatizo, badala ya kung'ang'ania mfumo wa kusubiri matatizo
 

Kweli kabisa.
Lakini kwani umesahau utamaduni wa kuzuia ni kama haupo?
Inabidi tujifunze utamaduni huu badala ya kusubiri tatizo litokee ndio tutafute dawa hata kama inagharimu zaidi ya uwezo wetu.
 
Nchi hii ina mambo mengi sana ya kujadili na sio haya,kuoa uoe wewe halafu uumbufu ulete kwa watu wengine si vema hata kidogo;kwanza mjadala wa mahakama za kidini MH RAIS amekataa na mjadala umefungwa.TAFADHARI Usirudie kuandika masuala haya hapa yanachochea chuki katika nchi.Tafadhari ondoa hoja hii mara moja.Pia hakuna aliye wakataza anzisheni wenyewe.
 

Mwanakijiji
a. Wakristo wenyewe watataka mahakama sasa kwa vile waislamu wameomba?? au wanataka sidhani kama itakuwa ni mahitaji yao kwakuwa kutofauta hiyo hukumu za kikristo ni dhambi kwa wakristo..kama ni dhambi then wanaogopa nini kuomba kuanzishwa siku zote?? wala hatujaona huo mfano kwa nchi nyingi za kikristo duniani mbona sijaona hiyo sheria na hukumu zikitumika? kadhi courts ambazo zipo hata kwa nchi za kikristo kwa ajili ya waislamu kwasababu ni ibada...kwa hiyo hoja yako ni uwongo au uchoyo na chuki tu kwa waislam wa Tanzania

b. Waislamu wa Tanzania wanalipa kodi kama wananchi wengine kuna kuwa na shida gani kuhudumia na pesa za serikali kwakuwa hata sasa kuna kesi za kiislamu katika mahakama za kawaida ambapo hakimu analipwa lakini anahukumu kesi ambazo hana ujuzi nayo??..kazi ya serikali ni kuhudumia wananchi wote kwahiyo hawa waislamu wanaotaka mahakama ya kadhi pesa zao zinatakuwa hizo hizo zinazoenda katika mahakama zetu ..ndio maana nikasema serikali inatakiwa kupeleka kwenye kadhi funds pesa equivalent na kesi ambazo zingeenda mahakama za sasa not otherwise..

Sijaona mantiki ya waislamu kulipia huduma ambayo serikali inatakiwa kutoa kwa wananchi wake..
 

Umekasirika na umeandika kwa hasira..sijaona unataka kusema nini?? please andika tena ukiwa umetulia ..just intellectual arguments..
 
Kama unataka kazi nenda kasome usilazimize kuanzisha NGO ili kupata ajira nenda shule.Mahakama kwa ajili ya ndoa tu tena si kwa waislamu wote ila wachache tu waliotayari,narudia tena ondoa link hii hapa maramoja.
 
Kama hukubaliani na mahakama zilizopo tafadhari sana usitende makosa,pia si lazima kuoa wanawake wengi,gawa urithi wako kabra hujafa,epuka jkulazimisha jambo alisilowezekana,pesa za kumlipa kadhi ni kodi za wananchi wote hata ambao si waislamu,kama bado hujaelewa tafadhari jiulize ni nchi ngapi zenye sheria hii?jipange upwa kwa hili mjadala umefungwa
 

Mnataka mahakama ya qadi toka wapi? wakati imeshabainishwa kwenye ibada zenu! ushauri wa buree, Nyie wenyewe waislamu, sunni! shia! qadian!.... kaeni hata ukumbi wa diamond jubilee hall chagueni maqadi watoe hukumu za kiislamu kwa mujibu wa quran, anaewazuia kufanya ibada hiyo nani?
 
Ni kwanini waislamu hawawezi ku enforce laws zao wenyewe za kiibada kwenye mahakama zao mpaka wasaidiwe na serikali lakini madhehebu mengine ya dini yanaweza?
Madhehebu mengine yanaweza vipi, how?

Mahakama ya kanisa ikiamuru, kwa mfano, mali ya mtaliki iende kulipia ada na malezi ya mtoto, na wewe ukakaidi wanakufanya nini, wanakufukuza kwenye fellowship ya maombi ya Jumatano? Padri, Shehe, Kadhi Mkuu, hana dola, ana enforce vipi amri yake?
 
Ninachosema mimi ni kwamba mambo ya ibada inabidi yabaki kuwa ya ibada bila kuihusisha serikali. Kama mtu(muislam) kaamua kutotii sheria za kiislam(ambazo ni ibada) hauwezi kumlazimisha kutii hizo amri kwa kutumia chombo cha serikali kwa sababu katiba yetu inatupa uhuru wa kuabudu au kutoabudu kitu chochote. Kwa hiyo kama muislam yeyote kaamua kutozifuata hizo amri ni uamuzi wake na hauwezi kumlazimisha kwa sababu huko ni kuvunja katiba. Mkuu kwa tanzania yetu, amri za dini zetu siyo mikataba ambayo ni lazima kuifuata...tunao uhuru wa kuzifuata hizo sheria kama wacha Mungu wa kweli au kutumia sheria za serikali kama tumeamua kumuweka Mungu pembeni...!
 

Nimependa hizo sehemu nilizo bold.

Mungu ni Imani ya mtu.Wapo wanaoamini, wapo wasioamini.Serikali ya Tanzania haina dini.Kwa msingi huo, serikali isiyo na dini, haiwezi kuwasaidia watu kufuata "amri za Mungu wao, au dini zao".

Kiserikali, kila mtu anao uhuru kuabudu atakacho na atakavyo.Ukiamua kuabudu Ng'ombe kama wanavyofanya baadhi ya watu ruksa! Ukiamua kuabudu nature, ruksa! Ukiamua kumuabudu Mungu wako unayemuamini wewe, ni wewe na Mungu wako.Haiwezi kuwa ni wewe, Mungu wako na serikali! Na hapa ndipo tunaposhindania ( bone of contention).Ni jukumu la kila mwenye dini yake kuabudu humohumo kwenye dini yake bila kuhusisha serikali isiyo na dini.

Kwa wakristo wakatoliki kwa mfano, kwenye masuala ya ndoa - wao wana sheria ya mke mmoja, na hakuna talaka hadi kifo kiwatenganishe! Hapo hapo, sheria za nchi zinaruhusu talaka.Wapo wakatoliki chungu mzima ambao wameenda mahakamani kudai talaka na hii ni kinyume kabisa na sheria za kikatoliki za ndoa. Kinachofanyika kwa mtu kama huyu, ni kwamba kanisa halitambui hiyo, na pia hawezi tena kufunga ndoa kanisani. Hatujawahi kusikia hata mara moja, wakatoliki wakiidai serikali ianzishe mahakama za kanisa ndani ya mfumo wa serikali.Wenyewe wanao utaratibu wao wa kufuata katika maswala yao, na hata kesi kama hizi, wanafuata hizo taratibu kivyao bila kuingiza dini nyingine maana kwa kufanya hivyo itakuwa kuingilia uhuru wa imani za wengine na hii ni kinyume na uhuru wa mtu binafsi chini ya katiba.Mara ngapi tunasikia pingamizi kanisani kwa mtu anayetaka kufunga ndoa na huku pale ambapo ametenda kinyume na matakwa ya sheria za kikristo katoliki? Ndio utaratibu, na wasioridhika wamepeleka rufaa hadi Vatican - MAKAO MAKUU YA KANISA KATOLIKI..Hii yote ni nje ya mfumo wa utoaji haki wa Serikali. mfumo unaotegemezwa na walipa kodi wote - wakristo, waislam na hata wasio na dini..Pale mhusika anapokaidi/kukiuka, basi hutengwa na kanisa.
 

hivi kazi ya serkali ni kuchonga Misalaba na kugaramia watu kwenda hija maka! Mbona unalazimisha mbuzi kula nyama?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…