Ibrahim K. Chiki
JF-Expert Member
- Apr 5, 2011
- 594
- 163
Duh, naona hoja ambayo ni intellectual argument ni mbili
1. inayohusiana na gharama za kuendesha kesi katika mahakama ya kadhi!
2. Waanzishe waislamu pekee
Majibu:
1. Gharama za kuendesha kesi hizo ni vema zitoke serikalini kwakuwa kadhi courts itakuwa pia imepunguza kwa kiasi kikubwa kesi za waislamu zinazofanywa na mahakama za serikali (inabidi tufanye calculation ili tupate kiasi hasa ni kesi ngapi za waislamu kwa sasa zipo mahakamani ambazo zinatakiwa kupelekwa kadhi courts na gharam yake ni shilingi ngapi each case..tukipata tuna transfer kiasi hicho kadhi courts
2. Ni muhimu kuanzishwa kisheria ili watu walioamua kufuata sheria hiyo wakubaliane na hukumu ya kadhi, kama itakuwa haitambuliki kisheria itakuwa haina maana kwasababu itakuwa hakuna tofauti ni kutokuwa na mahakama..kutambulika ni jambo la lazima ili iweze kuitwa mahakama..lakini kuhukumiwa huko ni optional siyo lazima..lakini unapokubali mahakama hiyo lazima ukubali hukumu zake..ok
tuache jazba nataka intellectual arguments ok
J
na hapo ndo kwenye tatizo. Point yako ya 2. Ikianzishwa kisheria tayari itakua imeingiliana na sheria za nchi yetu..nikimaanisha kua nchi yetu haina dini na hivyo haifungamani na umoja wowote wa kidini, ila kinchi-kimataifa inafungana na umoja wowote ule ambao hauna misingi ya kidini. Ndo maana ikasema wananchi na jumuiya zao za kidini ruksa kujiunga na jumuiya za kimataifa zenye misingi ya dini. Hope U get my point.