Katiba na sheria zetu zimejengwa kwenye misingi ya tamuduni za mfumo kristo(judeo christian traditions , values and morals). Muslims demand for kadhi courts to address mirathi is surely not asking for too much. We must learn to give and take.
Sina uhakika kama atatoke mmoja wetu na kukuomba uthibitishe madai haya kwa kutumia katiba hii tulio nayo utaweza kuandika hata mstari mmoja. Kama utaweza basi nakuomba utupe ushahidi wa hizo values, traditions na morals ili nasi tufunguke.
Lakini pia jiulize wewe umefanya nini ili kupata katiba mpya isiyokuwa na mfumo wa kidini. Juzi tumeona uhuni bungeni na tumekaa kimya kwa kuaminishwa kuwa katiba italetwa na malaika wachache wanoishi kama wanadamu, halafu leo tunasema katiba imeandikwa kwa msingi wa dini fulani. Swali, unafanya nini ili kuhakikisha haindikwi na mfumo unaousema wewe.
Pili, kama suala la kadhi linahitaji serikali basi hakuna sababu ya kuunda chombo kingine. BAKWATA inatosha na labda ifanye utaratibu wa kumpata kadhi. Nina uhakika kwa maneno hayo wapo ambao nyongo zimewachemka matumboni na wengine wananiona
hayawani
Nina sababu za msingi, ya kwamba madai mengi ya waislam ni kuwa BAKWATA ni chombo cha serikali na kinafadhiliwa na serikali ili kuhujumu uislam.Kumbu kumbu zangu zinanionyesha kuwa Sheikh mkuu kwa nyakati hizo(sijui sasa) alikuwa anapewa nyumba na serikali ikiwa ni pamoja na usafiri. Hii labda ndio sababu inayopelekea wengi kuamini BAKWATA ni chombo cha serikali pamoja na madai mengine.
Unapoomba mahakama ya kadhi ihudumiwe na serikali, hapo tayari umeshaingia katika mfumo wa serikali. CAG itabidi akague fungu linafanyaje kazi na kama kuna ubadhirifu basi wahusika watafikishwa mbele ya sheria na wizara kama ya fedha zinatingia.
Ikifika hapo tutasikia madai kuwa serikali inainglia mambo ya dini na maandamano. Ikumbukwe kuwa serikali siku zote ni taasisi inayokuwa 'Regulated' na hivyo itaweka regulations kwa mujibu wa sheria. Hiyo mahakama inayodhaniwa itakuwa huru haitakuwa huru kwasababu mkono wa serikali umeingia kama ulivyoingia BAKWATA kwa makusudi au kwa uhalali na kisheria.
Tatu, kama ndoa inayofungwa na sheikh popote inakubalika na makubaliano ya jinsi gani ifanyike ni kati ya wana ndoa na sheikh wao, na kuwa serikali inatambua hivyo kwanini asiwepo kadhi ambaye kisheria anatambuliwa (labda jina la kadhi ndilo linahitajika) ashughulikie masuala hayo? Kama yupo anayekataa uwepo wa kadhi basi aniulize nimthibitishie.
Nne, kama waislam wanaweza kuhudumia misikiti na miradi yao kwanini iwe tabu kupata chanzo cha fedha kumhudumia kadhi.
Na ikumbukwe kuwa kama sheikh anavyofanya mazishi ya mtu kwa imani au kumfungisha ndoa au kusuluhisha mgogoro ndivyo kadhi anatakiwa aendeshe shuguli zake kwasababu ni sehemu ya ibada. Ima atawezaje kujikimu hilo linabaki suala la waumini husika kama wanavyoweza kumhudumia sheikh, kulipa bili za umeme na maji n.k. Ni kwa njia hiyo pekee waislam wataweza kuwa na vyombo vyao huru.
Tano, hoja na umuhimu wa kadhi ubaki kwa mantiki yake. Usifanywe kama simba na Yanga kwasababu hiyo ina 'adulterate' mamlaka na hadhi ya kadhi. Kazi ya kadhi sio mirathi ya kugawa mali. Kadhi anashugulikia mambo yote yanayohusu sheria ikiwa ni pamoja na mahusiano ya ndoa na kutafsiri sharia kama zilivyo. Ndiyo maana katika enzi za zamani ni makadhi waliokuwa na hadhi ya kuwashauri waumini wao juu ya tafsiri za ibada kama mfungo wa Ramadhani n.k.
Kufanya kazi ya kadhi ni kugawa mali(ambazo pengine hazipo) ni kutoelewa nini maana ya kadhi kunakochangiwa na kukariri maneno
Mwisho, suala la kadhi ni nyeti na lenye mantiki na hekima zake. Linatakiwa lishugulikiwe na watu wenye weledi wa hali ya juu. Kuliacha mitaani lizagae zagae na kila mmoja kuliandikia anachofikiri linapoteza mantiki kwasababu tu wapo waliokaririshwa kutoa hoja lakini hawawezi kuzitetea. Hoja ya kadhi inahusu imani na uhuru wa kuabudu na sio suala la fulani anapata hiki basi wale nao wapewe kile.
Sio suala la kugawana mali ni suala la kufuata sharia katika mambo ya kijamii ili kuleta utangamano katika ibada.