shizukan
JF-Expert Member
- Jan 16, 2011
- 1,158
- 564
Duh, naona hoja ambayo ni intellectual argument ni mbili
1. inayohusiana na gharama za kuendesha kesi katika mahakama ya kadhi!
2. Waanzishe waislamu pekee
Majibu:
1. Gharama za kuendesha kesi hizo ni vema zitoke serikalini kwakuwa kadhi courts itakuwa pia imepunguza kwa kiasi kikubwa kesi za waislamu zinazofanywa na mahakama za serikali (inabidi tufanye calculation ili tupate kiasi hasa ni kesi ngapi za waislamu kwa sasa zipo mahakamani ambazo zinatakiwa kupelekwa kadhi courts na gharam yake ni shilingi ngapi each case..tukipata tuna transfer kiasi hicho kadhi courts
2. Ni muhimu kuanzishwa kisheria ili watu walioamua kufuata sheria hiyo wakubaliane na hukumu ya kadhi, kama itakuwa haitambuliki kisheria itakuwa haina maana kwasababu itakuwa hakuna tofauti ni kutokuwa na mahakama..kutambulika ni jambo la lazima ili iweze kuitwa mahakama..lakini kuhukumiwa huko ni optional siyo lazima..lakini unapokubali mahakama hiyo lazima ukubali hukumu zake..ok
tuache jazba nataka intellectual arguments ok
J
How on hell are you going to conduct intellectual debate on non-intellectual issue? Wewe una maoni yako ambayo unataka watu waanzie hapo (kwenye calculation) wakati wengine hata concept yenyewe tu ya kuanzishwa hiyo mahakama inawatia kichefuchefu. Reading your mind, unakereka kweli kweli na ndio maana kila sentensi yako inaishia na 'OK' which means 'that is it'.
Unapowaambia wanaume unahitaji maoni halafu unachagua waseme nini ni ukosefu wa akili. Ikiwa concept yenyewe tu ni kichefu chefu, kuna haja gani ya explore second phase ambayo inainvolve calculations za hoja hewa? Wanufaikaji wa uanzishwaji wa hii mahakama ndio wanatakiwa waianzishe na kuigharamia.
Jana nilikushauri kitu, ila kwa hulka ya mtu dhaifu hukuupenda ushauri wangu na acha niurudie tena: Dini ni imani. Utekelezaji wa misingi ya imani hiyo ndio kipimo cha uhiari wa mtu kuwa wa dini hiyo au lah. Ikiwa mnachohitaji kuamuana kwa misingi ya dini yenu, basi hiyo ni sehemu ya ibada zenu na mnaweza kuyafanya hayo huko huko mnakofanyia ibada zingine. Mimi naamini Muislamu wa kweli atafanya maamuzi kwa mujibu wa sheria za kiislamu na ikiwa hataki basi huyo si muislamu, sasa kama mna mpango wa kulazimishana kuwa na imani, si mlazimishane kwa gharama zenu! Kwa mfn: Kanisa Katoliki lina mabaraza ya ndoa na ustawi wa jamii. Mambo yote yanayohusu matatizo ya ndoa na mahusiano hujadiliwa huko kwa misingi ya imani ya kikatoliki. Ikiwa mtu atapingana na maamuzi hayo ambayo yanaendana na imani ya dini, basi suala hilo litaenda mahakamani. Sasa inatuhusu nini sisi tusio waislamu kuchangia uendeshwaji wa mabaraza ya uamuzi wa ndoa za kiislamu as if ugomvi wenu unatuathiri na sisi?
Wewe umekazana kuzungumzia bajeti as if hizi hela unazozizungumzia ni za msikiti. What if Wakurya tukiamua kesi zetu wa kuwatia mkong'oto kina wife ziundiwe mahakama zake binafs kwa kuwa majaji wa mahakama za sheria hawajui mila zetu?
Intellectual gani usiyejua sheria za nchi yako? Kwanza nijuavyo mimi, Waislamu mambo yao huamuliwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za kiislamu. Ni heri ungeniambia mnaandaa mchakato wa kuboresha uelewa wa majaji juu ya sheria za dini yenu kuliko kunilazimisha nishiriki calculation za kodi yangu kuamua matatizo yako ya wewe kuwa na wake 6 na watoto 18. Mtakuwa mna yenu, wala si dini.
Leta hoja ya msingi juu ya kwa nini wasio waislamu wawajibike kuchangia mambo yenu, sio hii.