Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Status
Not open for further replies.
Tatizo ni hilo kwamba maoni yako ni bora kuliko hukumu ya mungu

Ally Kombo, don't be pathetic. Hili ni jibu jepesi sana kwa swali nililouliza. Hoja hapa si maoni ya Mungu, hoja ni Kadhi ataamuaje ikiwa Allah mwenyewe kakosea. Ikiwa Kadhi ataamua kwa maagizo ya Allah, na Allah ndio tayari keshatoa muongozo unaochanganya, je Kadhi aamue kwa muongozo gani?

Mmeomba intellectual argument na sasa unanirudisha kwenye hisia.
Mimi siongozwi na hisia bana, nimeweka hesabu hapo na wewe unaziona na hizo aya sikuzitunga mimi bali hata wewe unajua zipo kwenye Quran. Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa unaona aibu kwa makosa ya kihisabati aliyofanya Allah?

Hivi unataka kuniambia muda woote mnaotumia kujadili Biblia, Sura hizi za Quran ndio unaziona leo hapa mpk ukose majibu kiasi uanze kutumia hisia kuwa Allah anapasa kuheshimiwa hata kama kakosea hesabu? Basi kama huwezi kujibu hoja sema nimeshindwa na sio kushambulia watu. Akili za kuambiwa, changanya na zako.
 
oooh ! Kumbe Kafiri ! Ndio maana hata hiyo equation imekaa kikafiri. Sijui ujuzi wa kukokotoa na kuelewa uliupata wapi ? BTW kuna kitu unapoteza !

Bwana Ally, kama unaona kuna sehemu nimekosea kuhusu hesabu au hiyo Aya ya Quran unayo haki ya kuiweka sawa hiyo Aya na kufanya breakdown ya hesabu ili twende sawa. Kusema equation imekaa kikafiri ni ubishi wa kitoto wa mtu juha. Tueleze ukafiri wa equation na usahihi wa aya nilizozitaja na kuturekebisha, hiyo ndio itakuwa intellectual argument.

Na hii nakupa home work wewe na Topical nikitumaini mnazo Quran nyumbani mwenu. Hamna haja ya kuleteana ubishi, nawapa tu kama msaada muweze kuielewa Quran na mapungufu yake.

Sura 7:54, 10:3, 11:7, and 25:59 clearly state that God created "the heavens and the earth" in six days. But in Sura 41:9-12 the detailed description of the creation procedure adds up to eight days.

Ukiona ngumu kumeza, tema.
 
Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu..umefariki

Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam

Kwanini mali yake isigawanywe kiislam?? tunataka kadhi wawasaidie hao wanawake, watoto kuhusu mgawanyiko wa mali ya muumini huyu.. siyo voluntarily iwe sheria kabisa na hukumu itolewe na mahakama..ok

Ndio maana tunataka mahakama ya Kadhi..

NB: Naomba wale wenye hasira na uislam na waislamu watuache kwanza tuseme kwanini tunataka mahakama ya kadhi ili mtuelewe
unfortunately, akili na upeo mwingi wa waislam, hasa wanaoshabikia kuwepo kwa mahakama ya kadhi, ni wa aina hii. unajua umbumbumbu ni mzigo mkubwa sana sawa na kubeba jiwe/mwamba kwenye gunia.

kwa kukusaidia tu, wakati wa ugawaji mirathi, hatutumii sheria ya ndoa ya mwaka 1971. tunatumia sheria za kugawa mirathi, zipo wazi kabisa. sheria za ugawaji mirathi kwa watz ziko za aina kama nne, kutokana na ugawaji mirathi wa aina nne. aina hizo ni kama.
1. ugawaji kwa kutumia sheria za kimila
2. ugawaji kwa kutumia sheria za kiislam yaan quran
3. ugawaji kwa sheria ya kiserikali yaani ambayo huangukia kwa wakristo tu,7
4. ugawaji kwa kutumia sheria za kihindu.
wakristo wengi huangukia kwenye sheria ya kiserikali ambayo ni the indian succession Act, waislam huangukia kwenye ugawji mirathi kwa kufuata quran, watu wasio na dini au wafuata mila hufuata ugawaji kwa kimila na sheria yake ipo, wahindi pia hutumia ugawaji kwa sheria ya kihindu. kwasababu suala lililoongelewa ni la waislam na mahakama ya kadhi, ujue kuwa, wakati wa kugawa mirathi, ili kutambua ni sheria ipi inatakiwa kutumika kwa mtu, kuna vigezo viwili huwa vinatumika kutathmini, cha kwanza ni mwenendo wa maisha ya marehemu aliyokuwa anaishi, labda aliishi maisha ya kiislam, kikristo au kimila, na pili ni wosia au aina yaa sheria aliyotaka ije kutumiwa yeye mwenyewe aliyoisema au onyesha kabla hajafa.

wakati wa kugawa mirathi kwa kiislam, kadhi huwa anakuwepo pale mahakamani ili kuhakikisha kuwa sheria ya kiislam imefuatwa kikamilifu. ni lazima kadhi awepo, huwa anakuwepo lazima. kitu hiki kinaonyesha kuwa hakuna ulazima wa mahakama ya kipekee kuundwa kwasababu yale ambayo yangetimizwa katika mahakama hiyo bado yanatimizwa katika mahakama hizi..kadhi wanayemtaka huwa anakuwepo mahakamani na anakula ulaji vilevile, hawezi kukaa bure.

kwa kulinganisha sheria hizi zote za ugawaji mirathi, sheria inayokandamiza kuliko sheria zingine zote ni sheria ya kiislam na sheria ya kimila. sheria bora na inayofuata usawa ni sheria ya kiserikali ambayo ni ya waislam. mwanamke katika sheria ya kiislam anakandamizwa kupita maelezo, hathaminiwi si chombo cha thamani kabisa..nitaishia hapa kwasababu maandishi ningeandika mengi...
 
Sawa nani anaye implement sheria ya kiislam bila Kadhi ?
 
Bwana Ally, kama unaona kuna sehemu nimekosea kuhusu hesabu au hiyo Aya ya Quran unayo haki ya kuiweka sawa hiyo Aya na kufanya breakdown ya hesabu ili twende sawa. Kusema equation imekaa kikafiri ni ubishi wa kitoto wa mtu juha. Tueleze ukafiri wa equation na usahihi wa aya nilizozitaja na kuturekebisha, hiyo ndio itakuwa intellectual argument.

Na hii nakupa home work wewe na Topical nikitumaini mnazo Quran nyumbani mwenu. Hamna haja ya kuleteana ubishi, nawapa tu kama msaada muweze kuielewa Quran na mapungufu yake.

Sura 7:54, 10:3, 11:7, and 25:59 clearly state that God created "the heavens and the earth" in six days. But in Sura 41:9-12 the detailed description of the creation procedure adds up to eight days.

Ukiona ngumu kumeza, tema.

Mkuu acha kupotosha watu

a. Wewe unajua kuwa wakristo hawawezi kuwashinda kwa hoja waislamu kuhusu dini ipi ni ya kweli, tukianza kufanya hivyo hapa tutabadili mada; unajua wakristo wanavyolalamika kila siku kwamba dini yao inakashifiwa?? tuache hayo..

Naomba tujikite kwenye mada naomba uulize swali moja kwa wakati kuhusu mirathi maana unaonekana kuna mambo unataka kufahamu hasa haki za wanawake na kadhalika??

Nakushauri acha kejeli, majigambo na dharau maana tukianza kufanya hivyo nyinyi ni kwanza kwenda kwa Mods..kwamba wanakashifu dini..
 
Mbona umekazana kuwa ninapotosha umma ninapotosha umma lkn huelezi ninapotosha vipi?

Kwa hiyo unanitishia Mods?

Mimi sioni sehemu niliyokashifu dini yako. Haya niyasemayo nimeyatoa humo humo kwenye Quran. Shida yenu ni kwamba mnaogopa kwamba waumini wenu wakiyajua haya mtakosa majibu ya kuwapa. Mimi sina shida ukiniuliza jambo lolote toka kwenye Biblia. Sioni sababu ya kuwa mkali kwa kuwa tu nimehoji ipi ni aya sahihi kati ya mbili zinazopingana kuhusu uumbaji wa Allah.

Sawa nitaanza kuuliza swali moja at a time.

Swali la kwanza: Sura 4:11-12 inasema ikiwa mwanaume akafa, akiacha mke , binti watatu na wazazi wake, watapata urithi kwa uwiano wa Mabinti 2/3, wazazi 1/3 na mke 1/8. Nilitoa mfn jana kuwa ikiwa kiasi cha fedha alichoacha marehemu ni 100 tukiigawa kwa uwiano huo, mgawanyo utazidi kiasi cha fedha kilichopo. Je, Kadhi atatumia sheria gani kuamua kwa haki kwa mujibu wa Quran?

Tazama mfano hapa:
2/3 ya 100 = 66.7
1/3 ya 100 = 33.3
1/8 ya 100 = 12.5
Ukijumlisha hapa ndio utapata 112.5 ambayo ni zaidi ya 100 iliyopo. Sasa sitegemi utasema hii ni kashfa kwa hiyo nataraji majibu ya kisomi na sio manung'uniko na vitisho kuwa na wewe utaanza kashfa.
 
Tatizo lako ni hesabu au uelewa wa dini yetu ndio maana nilikushauri uwe unauliza kabla ya kupotosha sawa mkuu..pia sikutishii mod maana naamini waislamu kwa hoja za comperative religion wako mbali sana kila siku wakristo ndio wanaolalamika tuache hayo tujikite kwenye mada ndio ushauri wangu kwako..

kuhusu hili swali nimelijibu kule kwingine narudi kwa faida ya wanaJF

a. mgawanyiko unakuwa 2/3 inaenda kwa watoto wa kike wawili wa marehemu
b. 1/6 (sudusi) ya 1/3 iliyobaki (na siyo 100) kama unavyopotosha au kwa kutojua au kujifanya shujaa katika ujinga inaenda kwa mama mzazi
c. Sehemu iliyobaki ya mali inaenda kwa mke wa marehemu umeelewa au unahitaji ubao tuiingie darasani kabisa wewe dogo
 
@shikuzan

Kwa kukurahisihia kwakuwa hesabu ngumu hizi fanya hivi; kwakuwa warithi wa mali ni watatu tu kwa mujibu wa swali lako mgawanyo utakuwa hivi:-

a. watoto wa marehemu wanawake watachukua =2/3 itakuwa imebaki 1/3 ya mali -ok

b. Mama ya mzazi atachukua sudusi 1/6 of 1/3 = 1/18 ya mali ya marehemu itabaki 5/6 ya mali -ok

c. mke wa marehemu atachukua 5/6 of 1/3 =5/18 ya mali ya marehemu

Sasa jumlisha: 2/3 +1/18 + 5/18 =18/18 =1

NB. kama kujumlisha sehemu ni tatizo nenda shule ok
 
Kweli ni kutoelewa dini yenu na kwa mtaji huu sitakuja kuielewa na sijui hata hawa wanawake waliopo huko wameenda au wamepelekwa kwa Jihad. Hebu twende wote taratibu hapa maana kama ulivyosema ubongo wangu sio mzuri:

A. 2/3 ya 100 =66.7 kwa Mabinti (Kwa hiyo kwenye 100 ukitoa 66.7 inabaki 33.3)

B. 1/6 ya 33.3 =5.55 kwa mama mzazi

C. (iliyobaki) kwa mke. (naona hukuthubutu kuiweka kihisabati kwa kuwa unajua nitauliza hiyo ?/? imeandikwa kwenye aya ipi)

Labda kuliko kushindania hesabu ambazo tayari umeshanibaini kuwa sizijui, unaonaje turudi kwenye original concept. Hii sura ni sahihi?
Sura 4:11-12
When a man dies, and is leaving behind three daughters, his two parents and his wife, they will receive the respective shares of 2/3 for the 3 daughters together, 1/3 for the parents together [both according to verse 4:11] and 1/8 for the wife .

Labda ungenielewesha hii 1/6 ya 1/3 kwa mzazi unaipata katika aya gani. Manake tukitoka nje ya Quran lolote linawezekana kihisabati. Na ndio maana ukawahi kusema iliyobaki ni ya mjane bila kusema ni ngapi ya ngapi kwa kuwa unajua hilo halipo kwenye Quran.
 
@shikuzan

Kwa kukurahisihia kwakuwa hesabu ngumu hizi fanya hivi; kwakuwa warithi wa mali ni watatu tu kwa mujibu wa swali lako mgawanyo utakuwa hivi:-

a. watoto wa marehemu wanawake watachukua =2/3 itakuwa imebaki 1/3 ya mali -ok

b. Mama ya mzazi atachukua sudusi 1/6 of 1/3 = 1/18 ya mali ya marehemu itabaki 5/6 ya mali -ok

c. mke wa marehemu atachukua 5/6 of 1/3 =5/18 ya mali ya marehemu

Sasa jumlisha: 2/3 +1/18 + 5/18 =18/18 =1

NB. kama kujumlisha sehemu ni tatizo nenda shule ok

Haya ya mimi na hesabu ni maombi yako tu kuwa niwe sijui, too late. Kitu nachosema hapa, huu ubishi utaisha pale tu utakaponiambia hii habari ya 1/6 ya 1/3 unaitoa wapi kwenye Quran. Yawezekana unanielewesha kitu ambacho siyo ndio shida yangu. Mimi si muarabu na maneno ya kiarabu nina ugeni nayo. Ni vyema tukairejea sura iliyoandikwa mambo haya ndio hapo unirekebishe kuwa "hapa wewe umechukulia hivi, wakati maana yake ni hivi" lkn ukikaa tu na kubuni namba zako ili equation zibalansi hatutaelewana.
 
By the way, Topical, hii
" ..na mtasikia udhia mwingi kutoka kwa wale waliopewa kitabu kabla yenu.."
ni defensive mechanism ya mtunzi wa Quran kwa kuchelea mapungufu yake yatahojiwa na walio na ufahamu zaidi yenu. Anawaandaa kupuuza fair challenges toka kwa waliopewa kitabu kabla yenu (waliosoma kabla yenu/wenye ufahamu zaidi yenu) kwa kuwa ni dhahiri Quran ilikopiwa toka vitabu vya kale na mijumuisho ya historia zilizopo kwenye Biblia lkn bila usahihi wa kutosha.

Kwa hiyo sioni kama kuchelea huku ni suala la kujivunia. Kuna maandiko mengi kwenye Quran ambayo ukiyatilia maanani yamepandikizwa mahali ambapo sio penyewe na yanaweza kukufanya ujiulize mara mbili. Naamini unazijua kwa hatuna haja ya kuwapa mashaka wengine wasijue waelekee wapi.
 
Haya ya mimi na hesabu ni maombi yako tu kuwa niwe sijui, too late. Kitu nachosema hapa, huu ubishi utaisha pale tu utakaponiambia hii habari ya 1/6 ya 1/3 unaitoa wapi kwenye Quran. Yawezekana unanielewesha kitu ambacho siyo ndio shida yangu. Mimi si muarabu na maneno ya kiarabu nina ugeni nayo. Ni vyema tukairejea sura iliyoandikwa mambo haya ndio hapo unirekebishe kuwa "hapa wewe umechukulia hivi, wakati maana yake ni hivi" lkn ukikaa tu na kubuni namba zako ili equation zibalansi hatutaelewana.

Haya nimekupa maelezo ya Quran sura ya 4:11 na Qur 4:12

Na swali lako ni ikiwa warithi watakuwa aina tatu hayo ndio ufafanuzi wake kama huutaki ni bahati mbaya; najua hujui maana ya neno sudusi kama ilivyotumika katika Tafsiri maana yake ndio hiyo nimekupa sasa wewe si mwanazuoni wa kiislam; unahangaika bure na dini ambayo hutaka kujifunza

Huwezi kufahamu kama huna objectives ya kufahamu..
 
By the way, Topical, hii ni defensive mechanism ya mtunzi wa Quran kwa kuchelea mapungufu yake yatahojiwa na walio na ufahamu zaidi yenu. Anawaandaa kupuuza fair challenges toka kwa waliopewa kitabu kabla yenu (waliosoma kabla yenu/wenye ufahamu zaidi yenu) kwa kuwa ni dhahiri Quran ilikopiwa toka vitabu vya kale na mijumuisho ya historia zilizopo kwenye Biblia lkn bila usahihi wa kutosha.

Kwa hiyo sioni kama kuchelea huku ni suala la kujivunia. Kuna maandiko mengi kwenye Quran ambayo ukiyatilia maanani yamepandikizwa mahali ambapo sio penyewe na yanaweza kukufanya ujiulize mara mbili. Naamini unazijua kwa hatuna haja ya kuwapa mashaka wengine wasijue waelekee wapi.

Lol...
Qurani inaeleza behaviour zenu toka mwanzo zinatokana na wivu na husda kwani sisi tuko kwenye haki na tunaenda paradise na nyie mnajua mnatumikia shetani..hamtupati..

Sasa niambie katika biblia "mgawanyo wa mali ukoje kwa wakristo wote duniani" usiniambie hukumu ya state courts??? NIL
 
Ililazimu ieleze na ndio maana nikakwambia, mwandishi wa Quran (sijui ni nani) alichelea kuwa asipowaambia hivi hamtajiandaa kupinga kila mtakaloambiwa. Kwa kuambiwa kwenu hivyo, mnajiwekea ukuta wa kukataa kuelewa lolote lisemwalo na hilo ndio lengo la mwandishi, asiwapoteze kwa gharama yeyote. Na ukitaka kujua ukweli wa hili, tazama unavyokuwa mkali kuhusu internet, hupendi watu wafahamu jambo na kuhoji, nafuu yako ni wengine wasijue ili waendelee kuamini wanachoamini bila kupima.

Turudi kwenye hili swali kichekesho la mgawanyo wa mali kwenye Biblia. (Ni kichekesho kwa kuwa Wakristo hawaishi kwa sheria, bali imani). Nirejee kauli yako kuhusu kwa nini mnadai mahakama ya Kadhi, ulisema ni IBADA. Sasa tofauti na ibada zenu, ibada zetu zipo mioyoni mwetu kwa imani na tumaini la kuyapata yale tuliohidiwa na Bwana wa Ulimwengu huu, pasina shuruti wala malazimishano.

Haya mambo unayoyaongea na kuyaita sheria, ni agano la Mungu na Waisraeli akiwatoa utumwani Masri. Rejea Yohana 1:16-17 "Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea neema juu ya neema. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kwelizilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo" Kama ibada yenu Waislamu ilikuja kwa Torati, basi tambua ya kuwa Neema yetu na Kweli tunaipata kwa Yesu.

Hizo sheria zenu ni zao la Agano la Kale la Mungu na Wayahudi ambalo hata hivyo walilivunja. Hata Mungu kwa kuona ugumu wa sheria, alituletea imani mioyoni mwetu na ikatuletea amani na uchaji.

Tazama Yeremia 31:31-34 "Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya Agano Jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano lile nililofanya na baba zao, katika siku zile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa Mume kwao, asema Bwana. Bali Agano hili nitakalolifanya na nyumba ya Isaraeli, baada ya siku zile asema Bwana, NITATIA SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO NITAIANDIKA; NAMI NITAKUWA MUNGU WAO, nao watakuwa WATU WANGU. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake wakisema, mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao, hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao wala dhambi yao sitaikumbuka tena".

Nachotaka uone hapa ni kuwa, sheria inayotuongoza imeandikwa ndani yetu tofauti ya ile ya Musa iliyokuwa kwenye mawe hata iliwashinda wakaivunja. Bwana aliliona hili hata akaweka agano jipya ndani yetu. (kwa hiyo elewa ni kwa imani na sio mahakama)
Amri kumi za Musa bado hazijawapa nafasi ya kuishi kwa amani kiasi mnataka na mahakama na nguvu ya kisheria ya kutekeleza hukumu za mahakama hiyo, lkn Yesu alitupa amri moja kwa kila anayeamini:
Yohana 13:34 "amri mpya nawapeni, Mpendane. Kama mimi nilivyowapenda ninyi, mpendane hivyo hivyo"
Bwana Topical, ukimpenda mke wako hutamdhulumu mali yake na kumpa kaka yako. Ukimpenda mke wako, hutamfanya sex toy yako wala hutambadilishana kama bidhaa au kumtoa kwa wanaume wengine kama mnavyofanya.

Kuomba mahakama ni dalili ya kushindikana kwa imani. Shuruti haiji ilipotawala hiyari. Nikiwa muislamu nitayafuata ya Allah kwa imani na wala sitasubiri kadhi atume polisi kuja kunidhalimisha nitimize vifungu vya ibada. Kinachowafanya mlidai la enforcement ya hukumu ni upungufu wa imani.

Yesu ndio baba wa logic, na haya unayajua pia. Maswali yote ya sheria aliyajibu kwa hekima hata sheria ikakosa maana kwa waiaminio. Kama unabisha hili niulize nikufafanulie kwa nini naamini Yesu ni wa imani na sio sheria.

Hatuitumainii sheria kwa namna ile unavyoihitaji wewe. Shida yenu ni kwamba, muumini aliyeacha wosia kuwa sehemu ya mali yake ipelekwe msikitini waliobaki huwa hawafanyi hivyo. Kwa kuwa hawafanyi hivyo basi ndio mnataka namna ya kumaliza tatizo kwa sheria na hukumu, lkn mmeshajiuliza kwa nini hawatekelezi?

TIA SHERIA KTK MIOYO YA WAISLAMU HALAFU UTAONA KAMA ITAHITAJI MAHAKAMA KUWAFANYISHA WATU IBADA. FUNDISHENI MISIKITINI JUU YA UMUHIMU WA KUMTIII ALLAH NA SIO KUWALAZIMISHA WATU KWA NGUVU KANA KWAMBA ALLAH HAKUSEMA KUWA ATAWAHUKUMU YEYE MWENYEWE WASIOMTII.

Mazinge uliyemzungumzia jana ni yupi Topical?
 
Msaada zaidi kwako Topical unayetaka kujua kwa nini tupo tulivyo:
1. Kwanza elewa kuwa Mkristo ni lazima uwe logical. Kuwa logical ni lazima upate uweza wa roho ili uwe na hekima. Hapa namaanisha uwe mcha Mungu. Yesu hakuwa mtumwa wa Sheria, badala yake alikuwa mtu logical. Mfano: Nyingi za ibada zenu ni kwa ajili ya dunia na si kwa ajili ya Mungu. Mnajitafutia utukufu kwa wanadamu wanaowazunguka na kudhani mnampendeza Mungu. Yesu anasema

"Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana, maana hujiumbua nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wamefunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini, na Baba yako aonaye sirini atakujaza"
Mathayo 6:16-18

Wengi wa wazitumainiayo sheria hawazijui, badala yake wanakuwa watumwa wa sheria bila kujua lengo na nia yake: Yesu ambaye ni Baba wa LOGIC anafanya hivi: "ya Kaisari mpeni Kaisari na yake Mungu mpeni Mungu" Marko 12:17

Hata zile sheria mnazoziamini na kuzifuata kwa akili zenu, utekelezaji wake haupo. Ni mapokeo bila kutimiza lengo, kwa kuwa hamumjui Bwana. Nikukumbushe siku ile Yesu alipomponya mkoma siku ya sabato, tazama Wafarisayo walivyomzonga ya kuwa amevunja sheria ya sabato kwa kufanya kazi siku ile. Sasa Bw. Topical na wenzio msiojua kwa nini ni vyema kuijua maana badala ya kuwa mtumwa wa maandishi: Sabato maana yake pumziko. Mkoma yule siku zote alikuwa akisumbuka na kutaabika na ugonjwa, angefanya nini Yesu zaidi ya kumpumzisha ili naye yule mkoma apate pumziko(sabato). Kumbe wale walidhani Yesu amekosea ndio waliopotoka, kwani Yesu hakuvunja sheria, bali aliitimiza. Tazama Marko 2:27-28 "akawaambia Sabato ilifanyika kwa ajili ya wanadamu na si wanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye bwana wa Sabato"
Wote walikaa naye miaka yote ya upamoja nae, lkn hawakuweza kumpa pumziko la matatizo yake, lkn tazama Bw.Topical, Bwana wa Sabato alimpa Sabato yake naye kwa mara ya kwanza akapumzika.

Na pengine Topical hujaelewa siri ya Ufalme wa Yesu. Si wa duniani kiasi ayarejee magomvi yetu na kuanza kujadili namna tutakavyogawana mali kama ilivyo ktk kitabu chenu. Marko 10:21 "Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, umepungukiwa na neno moja. Nenda ukauze ulivyo navyo vyote, ukawape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate" Hapa utaona namna Yesu anavyoichukulia mali tuliyonayo hapa duniani, sidhani kama atakaa chini kuanza kutuelekeza namna ya kuigawa kwa wake zetu sita.

Ama kuhusu talaka
Mathayo 19:3-9
"Basi mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu kwa kumwambia, Je, ni halali kwa mtu kumuacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliumba mtu mume na mtu mke, kwa sababu hiyo mtu atamuacha babaye na mamaye na ataambatana na mkewe, na hao wawili hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwuliza, jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka na kumwacha? Akawaambia, Musa kwa kutambua ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa ya kuwaacha wake zenu; lkn tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine; azini, naye amuoaye yule aliyeachwa; azini."

Jibu ni hilo: Kama si kwa kosa la uasherati, si sahihi. Na muumba aliumba mtu mke na mtu mume, na si mtu mume na watu wake.

Basi eleweni ya kuwa yale tuyapayo nafasi kubwa ktk maisha yetu si yale ambayo Yesu aliyatazamia tuyatende. Mwanzo wa migongano ndio chimbuko la sheria na kama upendo ukitawala na yale aliyoyaagiza Yesu yakafanyika kwa imani, basi hatuna haja ya shuruti, hatuna haja ya kuamuliwa na binadamu na hatuna haja ya kumtumainia Kadhi, ila Mungu. Mungu alipoona Agano lake na wana wa Israeli likivunjika, hakuleta mahakama bali alituletea Roho Mtakatifu ndani ya Agano Jipya nasi, akaandika sheria yake mioyoni mwetu nayo ituongoze.

Kwa mfano wa Yesu tutatumia LOGIC zaidi kuamua mambo yetu kuepusha makwazo kwa wenzetu. Ndio maana siamini kuwa nina haki ya kuchukua sehemu ya mali ya kaka yangu, au dada yangu ikiwa ana watoto ambao kwa imani yangu, wanaitegemea hiyo mali iwasaidie. Kizuri cha kufanya ni kuwasaidia zaidi wao na mama yao ktk kuboresha maisha yao. Na ni imani yangu kuwa kwa kuwa na LOGIC tutaendelea kama Jamii na kama Taifa kwani tukiishi kwa mapokeo ya tamaduni za watu wengine ambao mazingira yetu hayafanani na yao, tutakwama.

Itanisaidia nini kuvaa Kanzu kama Yesu ikiwa kwetu Tanzania hamna joto kama kwao? Ukitumia akili, utavaa suruali na kufuata matendo yake, sio mavazi. Hatutamuiga Yesu kukohoa ili kuudhihirishia ulimwengu ya kuwa tu wafuasi wake.
 
@shizukan

Mkuu umeanza kuhubiri without any practical solution to the problem??

Pamoja na kwamba wakristo wanaamini kuwa hakuna na talaka lakini wakristo wengi wanaachana kila siku na wanaenda mahakamani na kugawanya mali zao kwa mujibu wa sheria za wabunge (state) kwasababu Biblia haina majibu ..NONE

Nikufahamishe tu kwamba mirathi katika uislam na sheria za Allah (Mwenyezi Mungu) zinatoa haki sawa kabisa; kwani mwanamke anapata sehemu yake, watoto wako wana sehemu yao na wazazi wako wana sehemy yao; kumbuka mwanamke anapofanya kazi na kupata mapato hatakiwi kuhudumia familia kwa mujibu wa sheria..

Unajua essence ya hiyo hukumu ni very simple; kwasababu hivi wewe ukifa wewe leo (assume huna watoto) kwanini mke apate sehemu yote mali yako??? na wazazi wako wasipate hata shilingi?? wakati wao kwa namna moja au nyingine ndio wanahusika wewe kupata fedha ulizo nazo

Mkuu imani bila practical solution ni "Illusion" ...

Swala lingine biblia inasemaje ikiwa utakufa wewe bila watoto lakini ukawa na wazazi wako hawastahili chochote katika mali yako???
 
@Topical

Sihubiri, nakueleza. Ilinipasa nikuweke sawa juu ya kwa nini hatuhitaji muongozo wa namna ya Kadhi kwa kuwa imani inatosha. Vile vile ilinipasa kukuamsha upate kujua kuwa talaka nyingi mnazopeana kwa mujibu wa Yesu (Mungu) ni tamaa tu ya kufanya uasherati.

Kama unaona wakristo wanaachana basi jua kuwa wanaachana kwa matatizo yao, na dhamira zao mbaya na si kwa maelekezo ya Mungu. Mungu hakutaka kuachana. Kwa kuwa suala la kuachana ni tamaa na hitilafu za dunia, basi hata yanayoambatana na kuachana yapaswa kuamuliwa na mamlaka za dunia.

Haki sawa kabisa ni nadharia ya kufikirika kwani hata kwenye Quran haipo. Huko imeandikwa mwanamume atapata mara mbili ya mwanamke. Na nilichojaribu kukuelimisha mwanzo ni juu ya kukopi tamaduni za watu wengine na kuzi-implement juu ya maisha ya watu wa hali tofauti. Hainiingii akilini kuniambia kuwa mwanamke wa kiislamu anatakiwa afanye kazi lkn mapato yake ni ya kwake binafsi halafu uniambie hayo unayoyasema yanawezekanika hapa Tanzania.

Hebu fikiria tu, wewe unalima shamba kwa minajili ya kutunza familia, mkeo anaenda kazini na kurudi usiku kila siku halafu fedha anazopata huko anakenga nyumba ambayo wewe unaniambia hapa kuwa kwa mujibu wa dini yenu, haikuhusu. Kwa kweli sijui.

Kuhusu mimi nikifa leo na kuacha mke bila mtoto, sio shida kwa mke wangu kupata mali zetu zote. Hivi, unapomuoa mke huwa unakaa nae kwenu? Mimi hapa ndio sielewi dini yenu. Navyofahamu, mwanaume huachana na ndugu na wazazi wake na kuambatana na mkewe, nao huwa mwili mmoja tangu kuoana kwao. Sasa sioni wazazi na kaka na dada zangu wanaingiaje kwenye mali inayonihusu mimi na mke wangu. Ukioa manake tangu hapo, wewe na mkeo ni familia mpya inayojitegemea.

Labda niuulize swali, na naomba ulijibu kwa uaminifu. Kama ukifa leo, ukamuacha mke na watoto 4 bila mali yoyote, mgawanyo wa majukumu ya kuwalea watoto wako uko vipi kwa mujibu wa Quran?
(namaanisha, wazazi wako watachukua watoto wangapi kuwasomesha, dada yako atachukua wangapi na mkeo atabaki na wangapi?)

Au kwa namna nyingine, kama umekufa leo ukiwa huna mali sana sana una madeni, mama yako atalipa hayo madeni ngapi ya ngapi, mkeo atalipa ngapi ya ngapi na kaka/dada zako watalipa ngapi ya ngapi kwa mujibu wa Koran?

La mwisho kuhusu Biblia inasemaje nikifa bila mtoto kuhusu mali yangu vs wazazi, nafikiri hukunielewa jana. Dini yetu haijaangaza kwenye mali wala mabishano ya magawanyo. Kama nimekufa na kuacha mke, bila mtoto, nitakuwa nimekufa mimi. Mimi na mke wangu ni kitu kimoja, kwa hiyo kufa kwangu hakuhitaji mrithi kwani mke bado yu hai. Ikiwa nimekufa bila mke wala mtoto, basi familia yangu itarithi kilichopo.

Usisahau maswali yangu mawili kujibu
 
@shizukan

Ndugu imani bila practical solution ni illusion; ndio maana dini yetu inataka watu wawe na imani kubwa sana; ikiwa ni pamoja na ulivyosema kuwa talaka lakini inatakiwa iwe last resort na ndio maana katika maisha ya mtume wetu Muhammad (S.A.W) hajawai kutoa talaka katika maisha yake; hii ina maana Allah hapendi waislam waachane na mahakama ya kadhi ina deal na reconcilation kwanza kabla ya talaka; na talaka inachukuliwa kama ruhusu ikiwa kila hatua imeshindikana..kwa wenye imani jambo hili ni adhimu lakini kifo (mirathi) ni lazima maana kila mtu atakufa..

Unauliza haki katika dini yetu ni kufikirika siyo kweli kwasababu haki imeainishwa vizuri; na kwa muislamu mwanaume na mwanamke muumini hakuna tatizo kwenye hukumu za Allah kwakuwa yeye alituumba anatufahamu tulivyo..kwahiyo sisi waumini hatuoni tatizo kwenye hukumu zilizopo kwenye Quran kama nilivyokuelekeza kwenye hii thread tangu mwanzo; of course kwako wewe ambaye huamini uislam (hujaonja raha ya imani hii) utakuwa na reservations kama hizo..

Unauliza nikifa mimi bila mali majukumu ya kulea watoto wangu yanakuwa sawa sawa kama ilivyoanishwa katika katika kurithi; maana yake ni kwamba ndugu zangu, wazazi wangu na mke wangu kwa uwiono uliopo kwenye mirathi ikiwa wanatakiwa kupata kama ningekuwa na mali.. anaweza kuwa mkeo, ndugu zako etc kutegemeana na uwezo wao kiakili, ki-umri, etc hapo ndio utaona umuhimu wa wanazuoni kutoa fatwa kwa mujibu wa sharia na sunna.

Kuhusu madeni ni kwamba waislamu hawaruhusiwi kuzikwa wakiwa na madeni hadi ijulikane nani atalipa madeni yake; sheria inaruhusu ndugu zako (kike na kiume; wazazi wako; mke wako; waislamu wenzako) kukulipia madeni au kuahidi kulipa kwa mujibu wa sharia..utaona kuwa majukumu yanakuwa ya kifamilia ..kwa ufupi uislam unaamini katika misingi ya familia kubwa na si nuclear family kama mnavyoamini nyinyi wakristo..

Mkuu uislam unatoa practical solution in all spheres of life; kwahiyo uislamu siyo utamaduni wa watu bali ni way of life na inaweza kufuatwa na mtu yeyote, siyo mila za watu kama unavyosema na hapa Tanzania kuna watu wengi wanaishi kiislam ndio maana wanaomba wahukumiwe kiislam pia hasa kwenye mirathi etc..

Mkuu nasisitiza imani bila practical solution kama hii iliyopo kwenye uislam ni illusion tu ndio wakristo hawajui wafuate nin zaidi ya logic ambayo logic differs from person to person, from country to country, from one situation to another..i??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom