Wanaopinga Mkataba kati ya DP World na Serikali wanaeleweka zaidi kuliko wale wanaouunga mkono

Kwaufupi tu, wale oote waliozoea wizi, kipitisha vitu vya kishenzi , kwa njia ya bandari wakatafute kazi ya kufanya, na sio bandari tu, hata bandar bubu zitaundiwa timu maalum ya kushughulika nazo.
Watu mnaambiwa mkalime hamtaki.
Tupe ufafanuzi mkataba ni wa muda gan mkuu?
 
Naongezea hapo wanaopinga ni wengi kuliko wanaounga mkono

Pia wanaopinga wengi ni watu wanaojielewa na wengi ni wasomi wanaounga mkono wote ni la 7b na wengine hajaenda shule kabisa
Na wengi wanasukumwa zaidi na hisia pamoja na mihemko ya kidini badala ya facts
 
Habari wana JamiiForums.

Rejea kichwa cha habari chahusika.

Lengo la kuandika uzi huu ni kutoa maoni yangu juu ya wanaopinga mkataba kati ya DPW na serikali yetu ya Tanzania.

Kwa maoni yangu, naona wale wanaopinga mkataba huu wanaeleweka zaidi kuliko wale wanaouunga mkono.

Wale wanaopinga wanatoa hoja za msingi kabisa kama vile mkataba kutokuwa na ukomo, mkataba kujumisha bandari zote za Tanzania bara (zile za bahari na maziwa), mkataba kuweka chini ya usimamizi wa DPW njia zote za kimkakati wa kiuchumi, mkataba kuipendelea zaidi DPW kulinganisha na serikali, Mkataba kutoainisha kiasi gani tutapata kama nchi tukishaingia mkataba n.k.

Kwa upande wa wale wanaouunga mkono, wengi hawana hoja zaidi ya kuwapinga wale wanaoupinga na kuingiza masuala ya Uarabu na dini ya Kiislamu.

Naomba kuwasilisha.

Ni kujifanya kichwa kigumu ila kila kitu kimetolewa ufafanuzi.

01. Kuhusu ukomo wa mkataba serikal imesema HGA ndo itakuja na jibu hilo.Unataka ukomo wa utekelezaji wa mkataba kweny mkataba wa makubaliano. Be calm HGA itasema ni lini mkataba utaisha

02.Serikal imezungumza wazi DP WORLD mbali na kuwekeza port zote ila hawatopewa 100% ya maeneo ya ports,DP world watainvest kweny asilimia kadhaa za maeneo ya ports.

03.HIO HOJA YA MKATABA KUWA CHINI YA USIMAMIZI WA DP WORLD NA SIO SERIKAL UMEITOA WAPI. ARTICLE NAMBA NGAPI TUKAISOME?

ARTICLE 18 KAMA SIJAKOSEA INASEMA KODI,USHURU NA CHARGES ZINGINE ZITAFATA NA KUSIMAMIWA NA SHERIA YA JMT.HII HAITOSHI KUONESHA USIMAMIZI WA SERIKALI?

04.SAS KAMA MKATABA HAUJAWEKA WAZI NI KIASI GANI DP WORLD WATAINVEST NA KUEARN KWA MWAKA NA KIASI GANI TUTAPATA KAMA NCHI KWA MWAKA WEW UMEJUAJE MKATABA UNAIPENDELEA DP WORLD[emoji16]?

HITIMISHO

UDINI ,UZANZIBAR NA UTANGANYIKA UMELETWA NA NYIE MNAOPINGA [emoji16].

MBOWE 7 JUNE 2023 ALISIKIKA AKIHUSISHA UZANZIBAR NA UTANGANYIKA KWENYE MKATABA WA DP WORLD.

AHADI UJENZI WA MSIKIT MBEYA KWA UFADHILI WA DP WORLD KAMA AMBAVYO INASEMEKANA HII ILITOSHA KUWATOA PANGONI KUJA ND AJENDA YA UDINI.

KWAIO NIKUJUZE SWALA LA UDINI CHIMBUKO NI NYINYI WAPINGAJI NA WAPOTOSHAJI.
 
Habari wana jamii forum.

Rejea kichwa cha habari chahusika.

Lengo la kuandika uzi huu ni kutoa maoni yangu juu ya wanaopinga mkataba kati ya DPW na serikali yetu ya Tanzania.

Kwa maoni yangu, naona wale wanaopinga mkataba huu wanaeleweka zaidi kuliko wale wanaouunga mkono.

Wale wanaopinga wanatoa hoja za msingi kabisa kama vile mkataba kutokuwa na ukomo, mkataba kujumisha bandari zote za Tanzania bara (zile za bahari na maziwa), mkataba kuweka chini ya usimamizi wa DPW njia zote za kimkakati wa kiuchumi, mkataba kuipendelea zaidi DPW kulinganisha na serikali, Mkataba kutoainisha kiasi gani tutapata kama nchi tukishaingia mkataba n.k.

Kwa upande wa wale wanaouunga mkono, wengi hawana hoja zaidi ya kuwapinga wale wanaoupinga na kuingiza masuala ya Uarabu na dini ya Kiislamu!

Naomba kuwasilisha.
Sawa kabisa. Wanaopinga mkataba wanaorodhesha hoja. Wanaounga mkono, wanawapinga wanaoupinga mkataba bila hata ya kugusia mkataba wenyewe. Ingekuwa busara kama wangezijibu hoja zinazotolewa.
Zaidi ya hayo, wanaoupinga mkataba wamesema wazi kasoro za mkataba, na si kumkataa mwekezaji aliyetambuliwa kwenye mkataba. Wanasingiziwa kuingiza mambo ya udini ambayo wala hawakuyagusia kwenye hoja zao. Kama ingekuwa masuala ya dini, kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Uturuki, nchi ya Kiislamu, kujenga SGR? Au kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Stieglers Gorge kujengwa na Misri, nchi ya Kiarabu na Kiislamu? Bila shaka hakuna udini katika kupinga mradi.
Kwa mambo yalipofikia hivi sasa, suluhisho ni kuitisha kura ya maoni (referendum) ili maoni ya wengi ndiyo yachukuliwe. Kuna Mkatoliki mwenzangu anayeupinga waraka wa TEC kwa hoja kwamba hakuulizwa atoe maoni yake na kwamba inabidi tuukubali mkataba kwa kuwa Bunge limeridhia. Hoja hii si sahihi. Kuhusiu TEC kutomhusisha na kwamba Bunge limeridhia, jee Mbunge wake alikwenda kumuuliza maoni yake kabla ya Bunge kuridhia? Kwa nini adai kuulizwa na TEC tu na siyo Mbunge wake? Hoja hii haina mshiko. Aidha, TEC haijasema iwe wanavyotaka wao. Wanachosema ni kwamba Serikali isikilize wananchi. Hao wananchi waelezwe kiuwazi mkataba ulivyo na wao ndio waamue. Serikali haitaki kuweka mambo wazi, na ndiyo maana Waziri Nnauye akakataza vyombo vya habari kuutangaza waraka wa TEC. Ni siri ipi hiyo inayolindwa hivyo na Serikali?
Katika miaka michache iliyopita kumekuwa na kesi si chini ya kumi kati ya DP World na inchi mbalimbali ulimwenguni ambazo DP World ilishindwa. Hii ni sababu tosha kwamba tuwe makini kwenye mikataba tunayoingia. Aidha Tanzania imefikishwa mahakamani mara kadhaa sasa na kutozwa faini kwa sababu ya kuvunja mkataba ambao tumekuja kugundua baadaye kwamba mkataba tulioingia una kasoro. Nashindwa kuelewa kwa nini mtu apinge kuchunguzwa kwa mkataba huu ili kuondoa uwezekano wa kuishia mahakamani kama ilivyotokea hivi sasa, maadam tumegutuka kwamba kuna kasoro. Hivi Serikali ilikuwa 'serious' kweli kupeleka Dubai wasanii kama Steve Nyerere kwenye majadiliano ya mkataba? Aidha, Bunge lilitoa saa 24 tu kwa watu kutoa maoni na watu 72 wakafikisha maoni ndani ya muda huo. Kuna namna mbili za kuangalia idadi hiyo. Moja, hao watu 72 ni wachache mno kati ya milioni zaidi ya 60 ya Watanzania kusema kwamba tulipata mawazo ya wananchi. Pili, hao watu 72 ni wengi mno kuweza kujitokeza kwa kushtukizwa tu ndani ya saa 24. Ina maana kwamba kama muda ungekuwa mrefu zaidi, bila shaka watu lukuki wangejitokeza. Hivi ndivyo TEC wanavyoomba: wananchi wasikilwe: Mkataba uchunguzwe upya; kasoro zitakazobainishwa zirekebishwe; Mwekezaji huyo huyo apewe tenda kama amekubali kurekebisha dosari; na mambo yaendelee.
 
Waliojenga hoja ya kupinga ndio waliongoza hoja ya udini,Uarabu, Utanganyika na Uzanzibari Kwa ajili ya upuuzi wao. Na wakabeba na maaskofu, wachungaji na mapadri kwenye majukwaa yao

Na mnaendelea
makuwadi ya warabu dpworld mapumbavu yote yamehongwa na hizo hela yatazitolea popote penye matundu mwilini.
 
Sawa kabisa. Wanaopinga mkataba wanaorodhesha hoja. Wanaounga mkono, wanawapinga wanaoupinga mkataba bila hata ya kugusia mkataba wenyewe. Ingekuwa busara kama wangezijibu hoja zinazotolewa.
Zaidi ya hayo, wanaoupinga mkataba wamesema wazi kasoro za mkataba, na si kumkataa mwekezaji aliyetambuliwa kwenye mkataba. Wanasingiziwa kuingiza mambo ya udini ambayo wala hawakuyagusia kwenye hoja zao. Kama ingekuwa masuala ya dini, kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Uturuki, nchi ya Kiislamu, kujenga SGR? Au kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Stieglers Gorge kujengwa na Misri, nchi ya Kiarabu na Kiislamu? Bila shaka hakuna udini katika kupinga mradi.
Kwa mambo yalipofikia hivi sasa, suluhisho ni kuitisha kura ya maoni (referendum) ili maoni ya wengi ndiyo yachukuliwe. Kuna Mkatoliki mwenzangu anayeupinga waraka wa TEC kwa hoja kwamba hakuulizwa atoe maoni yake na kwamba inabidi tuukubali mkataba kwa kuwa Bunge limeridhia. Hoja hii si sahihi. Kuhusiu TEC kutomhusisha na kwamba Bunge limeridhia, jee Mbunge wake alikwenda kumuuliza maoni yake kabla ya Bunge kuridhia? Kwa nini adai kuulizwa na TEC tu na siyo Mbunge wake? Hoja hii haina mshiko. Aidha, TEC haijasema iwe wanavyotaka wao. Wanachosema ni kwamba Serikali isikilize wananchi. Hao wananchi waelezwe kiuwazi mkataba ulivyo na wao ndio waamue. Serikali haitaki kuweka mambo wazi, na ndiyo maana Waziri Nnauye akakataza vyombo vya habari kuutangaza waraka wa TEC. Ni siri ipi hiyo inayolindwa hivyo na Serikali?
Katika miaka michache iliyopita kumekuwa na kesi si chini ya kumi kati ya DP World na inchi mbalimbali ulimwenguni ambazo DP World ilishindwa. Hii ni sababu tosha kwamba tuwe makini kwenye mikataba tunayoingia. Aidha Tanzania imefikishwa mahakamani mara kadhaa sasa na kutozwa faini kwa sababu ya kuvunja mkataba ambao tumekuja kugundua baadaye kwamba mkataba tulioingia una kasoro. Nashindwa kuelewa kwa nini mtu apinge kuchunguzwa kwa mkataba huu ili kuondoa uwezekano wa kuishia mahakamani kama ilivyotokea hivi sasa, maadam tumegutuka kwamba kuna kasoro. Hivi Serikali ilikuwa 'serious' kweli kupeleka Dubai wasanii kama Steve Nyerere kwenye majadiliano ya mkataba? Aidha, Bunge lilitoa saa 24 tu kwa watu kutoa maoni na watu 72 wakafikisha maoni ndani ya muda huo. Kuna namna mbili za kuangalia idadi hiyo. Moja, hao watu 72 ni wachache mno kati ya milioni zaidi ya 60 ya Watanzania kusema kwamba tulipata mawazo ya wananchi. Pili, hao watu 72 ni wengi mno kuweza kujitokeza kwa kushtukizwa tu ndani ya saa 24. Ina maana kwamba kama muda ungekuwa mrefu zaidi, bila shaka watu lukuki wangejitokeza. Hivi ndivyo TEC wanavyoomba: wananchi wasikilwe: Mkataba uchunguzwe upya; kasoro zitakazobainishwa zirekebishwe; Mwekezaji huyo huyo apewe tenda kama amekubali kurekebisha dosari; na mambo yaendelee.
Ahsante sana kwa mchango murua Mkuu.
 
Kwaufupi tu, wale oote waliozoea wizi, kipitisha vitu vya kishenzi , kwa njia ya bandari wakatafute kazi ya kufanya, na sio bandari tu, hata bandar bubu zitaundiwa timu maalum ya kushughulika nazo.
Watu mnaambiwa mkalime hamtaki.
Yani watu wapitishe vitu vya wiz na kishenz huku ccm na wapumbavu wao wako bandarini? nyie wapumbavu na washenz tulishawambia nchi ilishawashinda ndio maana mmebaki kuwa wapumbavu tu na matumbo makubwa kama mifuko ya mpunga akili hamna miaka 60 toka uhuru kwa upumbavu wenu na kukosa akili kwenu mnauza bandari ccm yote ni mabwabwa na wafuas wao.
 
Na wengi wanasukumwa zaidi na hisia pamoja na mihemko ya kidini badala ya facts
Shida ndio iko hapo unakuta mtu anapinga kwa hoja ya msingi mwingine anadakia mbona kuna mikataba mibovu iliingiwa wakapewa wazungu huu wamepewa waarabu ndio mnawaka sasa imagine argument kama hizo na ndio mana hili dubwasha limeleta kelele nyingi kwa sababu wote kama Taifa tumeshindwa kusimama na kusema mapungufu yako hapa na pale ili serikali irekebishe sasa imegeuka wanaounga mkono wanawapinga wanaopinga,Mpira umehamishwa golini😁😁😁 inahuzunisha sana
 
Hako ni kakikwazo tu kanatengenezwa kwa lengo la tahaluki kwa watanzania..wanajua wakitengeneza kataharuki watanzania wengi hawana uelewa wa kutosha watawafuata.

Wewe unafikiri kwanini kwenye hiko kikwazo kinachowafanya wapinge kwa nguvu zote, kwa nini kwa makusudi wanawaaminisha watanzania hawa wasioelewa kua bandari inauzwa?
Wanajua watanzania hawana uelewa wa kutosha ndio wanaingiza maneno ya taharu ya aina hii kumbe sio kweli.

"ingeni kwa mfumo wa kutoa elimu kwa watanzania na sio kupinga kwa njia ya kuwapa tahatuki watanzania".
Kama wewe ni mtanzania na unaelewa kwanini uwasemehe wengine kua hawaelewi.Sidhani kama tuna ujinga mwingi kiasi chakushindwa kujua kipi ni sahihi na kipi si sahii hasa kwenye hili la bandari.Kwa jinsi tu ambavyo huyu mwekezaji alivyokuja kwakupitia mlango wa nyuma inatosha tu kujua hili jambo haliko sawa,ndo maana watetezi wake ni wengi inaonekana dhahiri ni dili ya high table.
 
Wabunge wetu tulio wachagua walichambua kwa kina makubaliano yaliyo ingiwa Kati ya nchi yetu na Dubai latika uwekezaji maeneo mbalimbali kwa kuanzia Bandarini ambapo mkataba utaingiwa siku zijazo.

Ufafanuzi wa kina umetolewa, Mahakama pia kupitia maamuzi yake huko Mbeya imetamka waziwazi faidi zitakazo patikana kutokana na uwekezaji wa DPW.

Leo hii TEC wanajitokeza bila hata aibu wala kuheshimu vyombo vingine kama Bunge letu na Mahakama na kupinga uwekezaji wa DPW, kwahiyo wao ndio wanaelewa zaidi ya Bunge letu?
tuache unafiki kwenye jambo hili, tuwe wakweli, tuiache serikali ifanye kazi zake za kuletea maendeleo wananchi.
 
Habari wana JamiiForums.

Rejea kichwa cha habari chahusika.

Lengo la kuandika uzi huu ni kutoa maoni yangu juu ya wanaopinga mkataba kati ya DPW na serikali yetu ya Tanzania.

Kwa maoni yangu, naona wale wanaopinga mkataba huu wanaeleweka zaidi kuliko wale wanaouunga mkono.

Wale wanaopinga wanatoa hoja za msingi kabisa kama vile mkataba kutokuwa na ukomo, mkataba kujumisha bandari zote za Tanzania bara (zile za bahari na maziwa), mkataba kuweka chini ya usimamizi wa DPW njia zote za kimkakati wa kiuchumi, mkataba kuipendelea zaidi DPW kulinganisha na serikali, Mkataba kutoainisha kiasi gani tutapata kama nchi tukishaingia mkataba n.k.

Kwa upande wa wale wanaouunga mkono, wengi hawana hoja zaidi ya kuwapinga wale wanaoupinga na kuingiza masuala ya Uarabu na dini ya Kiislamu.

Naomba kuwasilisha.
Hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyokua !
Kwa sababu nyumba nzuri huanza kwa kujengwa msingi mzuri !
Ukikosea kujenga msingi nyumba haitakuwa imara !
Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu !
Watu wakishaanza dharau na kejeli dhidi ya wengine hapo utangamano na umoja huwa vinatoweka haraka sana !
Matokeo yake hao watu hawatakuwa na sauti moja kuhusu suala lililopo mbele yao !
Matokeo yake yatabaki malumbano tu yasiyokuwa na faida yeyote !!
Na ndivyo ilivyo kwa wakati huu.
 
Naongezea hapo wanaopinga ni wengi kuliko wanaounga mkono

Pia wanaopinga wengi ni watu wanaojielewa na wengi ni wasomi wanaounga mkono wote ni la 7b na wengine hajaenda shule kabisa
Sawa kwahiyo mpaka wabunge ni kundi hilo?
 
Kwa maana hiyo mpaka wabunge pia ni kundi hilo?
Kwanza tuweke kumbukumbu sawa! Karibia wote hawana hiyo sifa ya kuitwa wabunge! Iwapo tu vigezo na masharti vitazingatiwa.

Hivyo siwezi kuongelea chochote kuhusu hao viumbe.
 
Back
Top Bottom