Wanaopinga Mkataba kati ya DP World na Serikali wanaeleweka zaidi kuliko wale wanaouunga mkono

Wanaopinga Mkataba kati ya DP World na Serikali wanaeleweka zaidi kuliko wale wanaouunga mkono

Sawa kabisa. Wanaopinga mkataba wanaorodhesha hoja. Wanaounga mkono, wanawapinga wanaoupinga mkataba bila hata ya kugusia mkataba wenyewe. Ingekuwa busara kama wangezijibu hoja zinazotolewa.
Zaidi ya hayo, wanaoupinga mkataba wamesema wazi kasoro za mkataba, na si kumkataa mwekezaji aliyetambuliwa kwenye mkataba. Wanasingiziwa kuingiza mambo ya udini ambayo wala hawakuyagusia kwenye hoja zao. Kama ingekuwa masuala ya dini, kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Uturuki, nchi ya Kiislamu, kujenga SGR? Au kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Stieglers Gorge kujengwa na Misri, nchi ya Kiarabu na Kiislamu? Bila shaka hakuna udini katika kupinga mradi.
Kwa mambo yalipofikia hivi sasa, suluhisho ni kuitisha kura ya maoni (referendum) ili maoni ya wengi ndiyo yachukuliwe. Kuna Mkatoliki mwenzangu anayeupinga waraka wa TEC kwa hoja kwamba hakuulizwa atoe maoni yake na kwamba inabidi tuukubali mkataba kwa kuwa Bunge limeridhia. Hoja hii si sahihi. Kuhusiu TEC kutomhusisha na kwamba Bunge limeridhia, jee Mbunge wake alikwenda kumuuliza maoni yake kabla ya Bunge kuridhia? Kwa nini adai kuulizwa na TEC tu na siyo Mbunge wake? Hoja hii haina mshiko. Aidha, TEC haijasema iwe wanavyotaka wao. Wanachosema ni kwamba Serikali isikilize wananchi. Hao wananchi waelezwe kiuwazi mkataba ulivyo na wao ndio waamue. Serikali haitaki kuweka mambo wazi, na ndiyo maana Waziri Nnauye akakataza vyombo vya habari kuutangaza waraka wa TEC. Ni siri ipi hiyo inayolindwa hivyo na Serikali?
Katika miaka michache iliyopita kumekuwa na kesi si chini ya kumi kati ya DP World na inchi mbalimbali ulimwenguni ambazo DP World ilishindwa. Hii ni sababu tosha kwamba tuwe makini kwenye mikataba tunayoingia. Aidha Tanzania imefikishwa mahakamani mara kadhaa sasa na kutozwa faini kwa sababu ya kuvunja mkataba ambao tumekuja kugundua baadaye kwamba mkataba tulioingia una kasoro. Nashindwa kuelewa kwa nini mtu apinge kuchunguzwa kwa mkataba huu ili kuondoa uwezekano wa kuishia mahakamani kama ilivyotokea hivi sasa, maadam tumegutuka kwamba kuna kasoro. Hivi Serikali ilikuwa 'serious' kweli kupeleka Dubai wasanii kama Steve Nyerere kwenye majadiliano ya mkataba? Aidha, Bunge lilitoa saa 24 tu kwa watu kutoa maoni na watu 72 wakafikisha maoni ndani ya muda huo. Kuna namna mbili za kuangalia idadi hiyo. Moja, hao watu 72 ni wachache mno kati ya milioni zaidi ya 60 ya Watanzania kusema kwamba tulipata mawazo ya wananchi. Pili, hao watu 72 ni wengi mno kuweza kujitokeza kwa kushtukizwa tu ndani ya saa 24. Ina maana kwamba kama muda ungekuwa mrefu zaidi, bila shaka watu lukuki wangejitokeza. Hivi ndivyo TEC wanavyoomba: wananchi wasikilwe: Mkataba uchunguzwe upya; kasoro zitakazobainishwa zirekebishwe; Mwekezaji huyo huyo apewe tenda kama amekubali kurekebisha dosari; na mambo yaendelee.
Tunahitaji hivyo vipengele vyenye dosari binafsi nimeusoma mkataba sijaona shida.

Watanzania wengi ni wavivu kusoma na wepesi kuamini.Huwezi taka wananchi wapige kura kwenye jambo linalohitaji taaluma bahat mbaya wenye taaluma hawakai kweny nafasi zao.

Wananchi wengi wanapinga/wanaunga mkono sabab ya imani yao kwa wanaowaamin.Wapo wapenda chadema wao huamin kile chadema inasema hatakam taarifa sio sahih.

Kweny hili jambo kinachohitajika ni uzalendo. Nyeusi iwe nyeusi nyeupe iwe nyeupo. Ajenda iwe maslah ya TAIFA na sio ajenga shirikishi.

BINAFSI NAUNGA MKONO IGA KAMA KUNA UWEZEKANO IGA IKABORESHWA ZAID KWENYE 1 IKAWA 2 BASI NAUNGA MKONO MABORESHO HAYO.
 
Habari wana JamiiForums.

Rejea kichwa cha habari chahusika.

Lengo la kuandika uzi huu ni kutoa maoni yangu juu ya wanaopinga mkataba kati ya DPW na serikali yetu ya Tanzania.

Kwa maoni yangu, naona wale wanaopinga mkataba huu wanaeleweka zaidi kuliko wale wanaouunga mkono.

Wale wanaopinga wanatoa hoja za msingi kabisa kama vile mkataba kutokuwa na ukomo, mkataba kujumisha bandari zote za Tanzania bara (zile za bahari na maziwa), mkataba kuweka chini ya usimamizi wa DPW njia zote za kimkakati wa kiuchumi, mkataba kuipendelea zaidi DPW kulinganisha na serikali, Mkataba kutoainisha kiasi gani tutapata kama nchi tukishaingia mkataba n.k.

Kwa upande wa wale wanaouunga mkono, wengi hawana hoja zaidi ya kuwapinga wale wanaoupinga na kuingiza masuala ya Uarabu na dini ya Kiislamu.

Naomba kuwasilisha.
Aponisawa na kujitekenya nakucheka mwenyewe pigeni kelele nyinyi wachache sisi tuliowengi tumeukubali mkataba ndiomaana mkiitisha mkutano wanatoka watukiduchu lakini tungekuwa hatuupendi sisi wengi barabara zingejaa
 
Back
Top Bottom