#COVID19 Wanaopona Coronavirus hurudia kuumwa tena kutokana na kurudia Mswaki waliokuwa wakitumia kipindi cha kuugua

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
WATAALAMU wa afya wamebaini baadhi ya watu waliopona UVIKO-19 wanaugua tena ugonjwa huo ndani ya muda mfupi kutokana na kurudia mswaki baada ya kupona.

Kwa mujibu wa Ofisa Ufuatiliaji na Udhibiti wa Magonjwa wa Wizara ya Afya, Dk. Baraka Nzobo, ili kuepuka kuugua tena ugonjwa huo, mgonjwa anatakiwa kuuteketeza kwa moto mswaki aliokuwa anautumia.

Dk. Nzobo alikuwa akitoa elimu jana namna ya kukabiliana na maambukizi ya UVIKO-19 kwa wananchi wa Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

“Mgonjwa aliyepona UVIKO-19, hapaswi kuutumia tena mswaki aliokuwa nao kabla ya kupona, kwa sababu atajiambukiza tena ugonjwa huo kupitia vijidudu vilivyobaki.

“Mswaki uliokuwa unautumia awali na kupata maradhi ya Uviko-19 na baadaye ukapata tiba ukapona, unatakiwa kuuacha kwa kuuteketeza na kutumia mswaki mpya ili usijiambukize upya ugonjwa huo," alifafanua.

Dk. Nzobo pia alisema ni hatari kuchangia dawa moja ya meno kwa familia nzima kupitia miswaki tofauti au watu wengi kutumia dawa moja ya meno hasa kwenye kambi za wazee na shuleni.

“Mnaposhirikiana dawa ya meno kwa kupigia mswaki na kusafisha kinywa kwenye hosteli, vyuoni au mikusanyiko yoyote ni hatari kwani huchangia kueneza maambukizi ya virusi vya UVIKO-19,” alihadharisha.

Vilevile, Dk. Nzobo alisema watu wanatakiwa kuepuka kuchangia mswaki au kuhifadhi mswaki sehemu moja ili wajikinge na maambukizi ya Uviko-19.

Baadhi ya wakazi wa Mirerani akiwamo, Ally Suleiman, walisema elimu hiyo ya matumizi ya mswaki na dawa za meno kwenye mapambano ya Uviko-19, wengi wao ndiyo wameisikia kwa mara ya kwanza na wataitumia kuchukua tahadhari.

Ippmedia
 
Afadhali sasa tunaelimika kuhusu hii kitu. Ni bora kupata elimu ya kutosha ili kujikinga. Kwenye kujikinga we have no choice no matter how hard is it kuliko kudanganyana eti UVIKO-19 haipo au iliisha.
 
Nabadili mswaki halafu mikusanyiko kama kawaida.
 
kwa maana hiyo wakati unaendelea kupata tiba mpaka unaenda kupona unatakiwa kbadilisha moswaki inayo itumia,sababu mswaki inatakiwa kutumia kila siku asubui na joon,mbona la kazi ipo
 
Mtaalamu atueleze chanjon inafaa au haifai,
Sio habari za miswaki tena kwani huu nao ni ukimwi?
 
WATAALAMU wa afya wamebaini baadhi ya watu waliopona UVIKO-19 wanaugua tena ugonjwa huo ndani ya muda mfupi kutokana na kurudia mswaki baada ya kupona.

Kwa mujibu wa Ofisa Ufuatiliaji na Udhibiti wa Magonjwa wa Wizara ya Afya, Dk. Baraka Nzobo, ili kuepuka kuugua tena ugonjwa huo, mgonjwa anatakiwa kuuteketeza kwa moto mswaki aliokuwa anautumia.

Dk. Nzobo alikuwa akitoa elimu jana namna ya kukabiliana na maambukizi ya UVIKO-19 kwa wananchi wa Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

“Mgonjwa aliyepona UVIKO-19, hapaswi kuutumia tena mswaki aliokuwa nao kabla ya kupona, kwa sababu atajiambukiza tena ugonjwa huo kupitia vijidudu vilivyobaki.

“Mswaki uliokuwa unautumia awali na kupata maradhi ya Uviko-19 na baadaye ukapata tiba ukapona, unatakiwa kuuacha kwa kuuteketeza na kutumia mswaki mpya ili usijiambukize upya ugonjwa huo," alifafanua.

Dk. Nzobo pia alisema ni hatari kuchangia dawa moja ya meno kwa familia nzima kupitia miswaki tofauti au watu wengi kutumia dawa moja ya meno hasa kwenye kambi za wazee na shuleni.

“Mnaposhirikiana dawa ya meno kwa kupigia mswaki na kusafisha kinywa kwenye hosteli, vyuoni au mikusanyiko yoyote ni hatari kwani huchangia kueneza maambukizi ya virusi vya UVIKO-19,” alihadharisha.

Vilevile, Dk. Nzobo alisema watu wanatakiwa kuepuka kuchangia mswaki au kuhifadhi mswaki sehemu moja ili wajikinge na maambukizi ya Uviko-19.

Baadhi ya wakazi wa Mirerani akiwamo, Ally Suleiman, walisema elimu hiyo ya matumizi ya mswaki na dawa za meno kwenye mapambano ya Uviko-19, wengi wao ndiyo wameisikia kwa mara ya kwanza na wataitumia kuchukua tahadhari.

Ippmedia
Hawa madaktari si ndio walisema tujifukize?
 
Mnatuambia tunawe mikono kwa maji tiririka na sabuni ili kuua virus waliopo mikononi, hivi maji tiririka na dawa ya meno haiwezi kuua virus waliopo kwenye mswaki?
Au mpaka tuoshe miswaki yetu kwa maji tiririka na sabuni au miswaki tuwe tunaipaka sanitizer?
 
Miswaki muichomeshe chanjo Pia [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom