Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
WATAALAMU wa afya wamebaini baadhi ya watu waliopona UVIKO-19 wanaugua tena ugonjwa huo ndani ya muda mfupi kutokana na kurudia mswaki baada ya kupona.
Kwa mujibu wa Ofisa Ufuatiliaji na Udhibiti wa Magonjwa wa Wizara ya Afya, Dk. Baraka Nzobo, ili kuepuka kuugua tena ugonjwa huo, mgonjwa anatakiwa kuuteketeza kwa moto mswaki aliokuwa anautumia.
Dk. Nzobo alikuwa akitoa elimu jana namna ya kukabiliana na maambukizi ya UVIKO-19 kwa wananchi wa Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
“Mgonjwa aliyepona UVIKO-19, hapaswi kuutumia tena mswaki aliokuwa nao kabla ya kupona, kwa sababu atajiambukiza tena ugonjwa huo kupitia vijidudu vilivyobaki.
“Mswaki uliokuwa unautumia awali na kupata maradhi ya Uviko-19 na baadaye ukapata tiba ukapona, unatakiwa kuuacha kwa kuuteketeza na kutumia mswaki mpya ili usijiambukize upya ugonjwa huo," alifafanua.
Dk. Nzobo pia alisema ni hatari kuchangia dawa moja ya meno kwa familia nzima kupitia miswaki tofauti au watu wengi kutumia dawa moja ya meno hasa kwenye kambi za wazee na shuleni.
“Mnaposhirikiana dawa ya meno kwa kupigia mswaki na kusafisha kinywa kwenye hosteli, vyuoni au mikusanyiko yoyote ni hatari kwani huchangia kueneza maambukizi ya virusi vya UVIKO-19,” alihadharisha.
Vilevile, Dk. Nzobo alisema watu wanatakiwa kuepuka kuchangia mswaki au kuhifadhi mswaki sehemu moja ili wajikinge na maambukizi ya Uviko-19.
Baadhi ya wakazi wa Mirerani akiwamo, Ally Suleiman, walisema elimu hiyo ya matumizi ya mswaki na dawa za meno kwenye mapambano ya Uviko-19, wengi wao ndiyo wameisikia kwa mara ya kwanza na wataitumia kuchukua tahadhari.
Ippmedia