Wanaosema bandari imeuzwa wanavikosea heshima vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama

Je kuna kifungu chochote cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kinachosindikiza hili lalamiko lako?

Je kama vyombo vyetu vya Ulinzina Usalama vinatukosea sisi, hatua gani zichukuliwe?
 
Nchi imejaa watu wa hovyo hii, mwingine ni huyu...ni mikataba mingapi mibovu isiolinuafaisha taifa hili imesainiwa ktk uwepo wa vyombo hivyo hivyo unavyotaka tuviamini
, Wanaoteseka na umaskini ni watanzania sio waajiriwa wa hivyo vyombo wala waajiri wao, hilo ulijue..
 

Sheria za mikataba unazijua? Unajua watu wanasotea miaka kibao kusomea mambo hayo? Tulia usiingie mkenge na kuzungumza mambo usiyoyajua. Swali je vyombo vya ulinzi vipo chini ya nani? Mkataba huh sio wa Nchi na Nchi Bali ni wa Nchi na sehemu ya wajanja kule DUBAI think big mkuu.Karibu tena
 
Kuhusu bandari wewe una maoni gani? binafsi naona sector binafsi ihusishwe pakubwa ila kuwe na check and balance kwenye terms za uendeshaji na mafunzo kwa watu wetu.
Katika kufanya hilo unatakiwa kuwa na nguvu za hiring and firing na sio kumpa exclusive right itakayokufanya umuombe. Bandari kwa ukubwa wake upakuaji na ushushaji waweza kuwa chini ya private. Pia unaweza kuoutsource baadhi ya vitengo kwa ufanisi. Hutakiwi kutoa mamlaka kwa private kwani ataweza kukuhujumu na usimfanye chochote. Kwenye private naweza kununua hisa za mshindani ili kumuondoa kwenye Biashara. Hakunaga Ubinadamu kwenye ubepari.
 
Tena hawana adabu kabisa [emoji1787]
 

While maybe neno “bandari kuuzwa” wanakuwa wameenda mbali.

Hivyo vyombo vya usalama huwa vinakuwa wapi wkt w amikataba?

Barrick, Symbion, na mikataba ambayo baadae ilikuja julikana ni ya hasara na ufiadi? Mpaka madudu yanakuja julikana baadae?

Vyombo vya usalama vinakuwa wapi?
 
Achilia huko mbali, juzi Halmashauri kuu imesema Serikali iharakishe mchakato wa uuzwaji wa Bandari yetu, jiulize ni lini walishirikiswa? ni wapi kwenye Ilani yao ya uchaguzi kuna sehemu wamendika ubinafishishaji wa Bandari na maziwa yote Tanzania bara?

Sasa kama CCM wenyewe hawajui na wanashabikia, itakuwaje hao wana usalama wetu? Ndugu yangu jukumu la kulinda mali asili zetu ili watukuu zetu wazikute ni letu sisi wenyewe, usalama ulikuwa enzi za Mwalimu.

Usalama wa leo ni wa kunusa maandamano, kwa mfano yale maandamano ya 22 July utaambiwa wamenusa viashiria vya uvunjifu wa amani, hivyo kila mtu abakie nyumbani kwake - hapo ndipo tulipofikia kama taifa huru.
 
Nimejizuiya kutumia lugha chafu, wanaopinga mkataba huu wanachonganishwa na vyombo vya ulinzi? je vyombo vya ulinzi vinahusikaje? Ndio hao hao wanaolipeleka misikitini yaani serikali imefikia mahali wanataka kuilipua nchi kwa ajili ya Waarabu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…