Wanaosema Mzee Mkapa ni nguzo ya Taifa wapo sahihi

Wanaosema Mzee Mkapa ni nguzo ya Taifa wapo sahihi

Joined
Oct 7, 2019
Posts
51
Reaction score
157
Tarehe 28/12/2019 niliandika kuhusu Mzee Mkapa kichwa Cha habari kikisema Nini maana ya Legacy? Niliandika naomba Kunukuu:-

"Natamani sana kujua wasaidizi wa Rais Mkapa alioingia nao madarakani 1995. Kama kuna mtu ameacha Legacy ya kutosha kwenye nchi hii japokuwa hatuoni kwa macho ya kawaida ni Rais Mkapa.

Huyu ndiye akiyetuachia mifumo inayotusaidia kuongoza nchi hadi Leo.

NSSF
NHF
TCU
LOANS BOARD
TANROAD
TRA
MIKOPO KWA WAFANYAKAZI TOKA KWENYE MABENKI.
MKURABITA
MKUKUTA
MPANGO WA ELIMU SHULE ZA MSINGI MMEM
MPANGO WA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI
VAT
TISS

Hii ni baadhi na hii ni mifumo si Muindombinu inayoonekana lakini mshawahi kujiuliza bila hii Mifumo nchi ingejiendeshaje?

Wasaidizi wa Rais wana wakati mgumu sana kufanya kututengenezea Mifumo mingine ya kutuachia. Mifumo itakayokuwa inafanya kazi.

Ndio manaa nataka kujua wasaidizi wa Mkapa walikuwa kina Nani kwa maana ya wataalamu.

Mwenye kuwajua nisaidie kuwataja hapa. Pia Mwenye kujua Mifumo mingine aliyotuachia Mzee Ben comment hapa."

Pumzika kwa amani mzee wetu wa ukweli na uwazi.

110336297_4168297613211444_3803251169200490242_n.jpg
 
1.Balozi Ombeni Sefue.

Katibu Mkuu Kiongozi miaka 10 MFULULIZO chini ya mpendwa wetu,brilliant Hayati BWM....
Rip BWM,aaamen
 
1.Balozi Ombeni Sefue...
Katibu Mkuu Kiongozi miaka 10 MFULULIZO chini ya mpendwa wetu,brilliant Hayati BWM....
Rip BWM,aaamen
CS wa JK alikuwa nani? Kuna mpare mmoja, nimesahau jina, naye alihudumu ama kwa Ben au JK. Sijui ni Mbaga?
 
Luhanjo alikua awamu ya Kikwete au Mkapa?
Yeees, Luhanjo, kipindi cha Ben na ndio aliyempa kijiti Sefue kama sikosei. Huyo aliyesema Ombeni amehudumu kipindi cha Ben atakuwa pengine kachanganya, Ombeni si amemshikisha kijiti Kijazi?
 
Mkapa ndie mwamba wa ccm aliweza kusawazisha Mambo kwenye Jambo kwa kutumia nguvu na akili,ambayo waliobaki ni ngumu kwao kutumia akili kutatua Mambo
 
Yeees, Luhanjo, kipindi cha Ben na ndio aliyempa kijiti Sefue kama sikosei. Huyo aliyesema Ombeni amehudumu kipindi cha Ben atakuwa pengine kachanganya, Ombeni si amemshikisha kijiti Kijazi?

Ombeni kampisha Kijazi, alimpokea Luhanjo kama sijakosea.
 
Magufuli tatizo lake anaoenda sifa.. mkapa alipiga marufuku kuitwa mtukufu.

Magufuli anauwezo mkubwa wa kusimamia maamuzi hata hivyo nadhani ana nafasi ya kurekehisha ulizingatia hakuwa na uzoefu mkubwa kwenye diplomasia..

Magufuli is not creative at all
 
Basi tu wanamtamdao walimchafua sana ili JK aonekane wa maana!
Ben alikosea kuuza tu nyumba za serikali na Ubinafsishaji usiutumia akili!

Issue ya nyumba za serikali ilikuwa OVERRATED Sana...
Tujiulize...hv NHC na JKT wamejenga nyumba ngapi za WATUMISHI wa umma toka lile sakata?!!

Jibu ni..NYINGI MNO

Je fedha iliyopatikana(HATA km ni ndogo)iliingizwa katika mifuko binafsi ya walioufanya mchakato ama ziliingia HAZINA?!!

Jibu ni....HAZINA

Baada ya MIAKA kadhaa SERIKALI imehamia DODOMA...

Je huko walikohamia,hawajengi nyumba?

Jibu....WANAJENGA KWA KASI MNO

Je Wasingeziuza zile za Dar es salaam
Wangeweza kuhama nazo?

Jibu ni.....HAPANA

Fikra Nyingine...

Je SERIKALI KUWAUZIA WATUMISHI wao waliostaafu na kukaa katika zile nyumba ni KOSA?

Jibu.....SI KOSA

Je ziliuzwa kwa BEI CHEE?!!

Jibu....Wako wanaosema ziliuzwa kwa fedha isiyolingana na thamani ya ARDHI.

Je ni KOSA kubwa la kutosameheka?!!!

Jibu....Hapana kwani waliouziwa ni WATANZANIA WALIOLITUMIKIA TAIFA zaidi ya hata KIINUA mgongo walichopata mwisho wa utumishi wao.

Je Serikali ilishindwa kuzibomoa zilizochakaa na NHC kujenga maghorofa kwa AJILI ya kupangisha.

Jibu...Ingekuwa ni GHARAMA kubwa mno na hao wapangaji wakukaa masaki KICHANGA CHUI na maeneo ya mikocheni wangeweza kuAFFORD COST ZAKE KIPINDI KILE.
Lakini PIA huwenda HAWAKUAMUA kuchukua njia hiyo kwa sababu wanazozijua na SI KOSA kufanya hivyo.

Maswali ni mengi na majibu pia ni mengi juu ya kadhia iliYOVUMISHWA SANA.
Kubwa zaidi ni kuwa mzee wetu hayati Mkapa ALIONEWA Sana....alikebehiwa Sana....alizodolewa Sana....na Mara nyingi ilikuwa NI sababu watu hawakuzuiwa kuona STATUS QUO ikibadilika.
Mfano kulikuwa na kundi la watu waliojifanya KUUFIA UJAMAA na kutotaka njia mpya za SOKO HURIA ilihali kulikuwa HAKUNA jinsi ya KUTOBADILIKA......

Kulikuwa na kundi la "wanaojifanya" PAN AFRICANISTS Hawa nao walimshambulia Sana mzee wetu BWM.

Nitakuja kudadavua zaidi juu ya "AILA" za makundi hayo inshaalah.

Rip BWM,

Jumbe Brown,
Kijana Muuza Al Kasus,
Tandale Kwa Mtogole DSM.
 
Back
Top Bottom