Biblia inatuambia watoto wa Nuhu ni Hamu, Yafeti na Shemu. hivyo wewe kushangaa Shemu kuwa hai baada ya gharika ni kutokusoma maandiko maana Biblia inasema Nuhu aliingia katika safina na wanawe wote na wake za wana wake. Buta Suala la Esau mjukuu wa Ibrahimu kuja kumkuta Nimrod siyo rahisi maana Ibrahimu mwenyewe amezaliwa miaka mingi sana baada ya gharika.
Mkuu tunachoshindwa kuelewana ni nini
1.Nimeweka wazi kuwa shem na Esau kwa vyanzo tofauti ndio walimuua Nimrod....
2. Hapo chini nikaelezea nadharia ya kwanini Esau anatajwa kumuua Nimrod kwenye kitabu cha yasher ndio nikaconclude kuwa hata mtoto wa Nimrod aliitwa Nimrod na ikawa cheo kwa watawala wote wa kutoka ukoo wa Nimrod
3. Kuna mchangiaji mmoja akasema kutokana na umri haiwezekani Esau kumuua Nimrod
4. Mie nimepiga hesabu kwamba kwa miaka ya Biblia kuna watu waliweza kuishi zaidi ya miaka 300 hivyo kwa hesabu nilizopiga Nimrod angekuwa na miaka takriban 200+ Esau akizaliwa
5. Ndio hapo najenga hoja kwamba gap la miaka 200 asishangae maana hata Shem naye kamzidi Nimrod miaka zaidi ya 300
6. Nimrod ni kitukuu kabisa cha Nuhu kupitia Ham na mwanaye Cush.... Shem naye anakuwa vimepita vizazi 7 ndio kazaliwa Abraham
7. Kwa mahesabu niliyoweka hapo juu niambie je which is more realistic kati ya Esau kumuua Nimrod au Shem kumuua Nimrod
Na naomba ieleweke hapa hakuna maoni yangu maana naona tunaanza kushambuliana personalities
Esau kumuua Nimrod ni kwa mujibu wa kitabu cha yasheri ambacho Biblia inakitambua
Shem kumuua Nimrod ni kwa mujibu wa mwanahistoria credible zaidi wa kiyahudi Flavius Josephus
So tujikite kwenye vyanzo sio anayewasilisha vyanzo....
Embu angalia hii family tree alafu wote mnaotetea hii objection mje hapa mseme kwanini mnashangaa Nimrod kuuawa na Esau ila Hamshangai Shem kumuua Nimrod bearing in mind kwamba kitabu cha Yasheri vinatambua Nimrod alikuwa mfalme kipindi Abraham anazaliwa!!
Kizuio kilwakivinje eden kimario Mazindu Msambule
Na mje na hoja sio mipasho tena