Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Ofukozi pipo used to die in ze ze ze reki.
Ni tatizo la lafudhi tu hilo.

Ni sawa na WANAIJERIA wengi wao wanajua kuzungumza lugha ya Kiingereza ila wameathiriwa na lafudhi ya lugha mama (mother tongue)

Hata lafudhi ya UINGEREZA, AUSTRALIA na MAREKANI huwa hazifanani japokuwa wote hao wanazungumza Kiingereza kama lugha yao ya Taifa katika Mataifa yao.
 
Ila mnasahau mzee lugha ya Kiingereza ni ligha yake ya kufundishiwa toka akiwa sekondari. Biden hajafundishiwa kwa Kiswahili au Kifaransa.
Kama Magufuli angekuwa haelewi masomo kwa sababu ya lugha inayofundishiwa hapo sawa ila suala la kuimudu vizuri lugha ni zaidi ya darasani kufundishwa kwa hiyo lugha tu.
 
Elimu ya Tz, kuanzia form one mpaka PhD iko kwa kiingeereza. Na PhD za Tz lazima zifanywe kwa Kiingeereza except PhD ya kiswahili.

Hivyo ni kitu abnormal kwa kwa mtu kumaliza PhD hajui Kiingeereza cha kuongea au anaongea hovyo.

Hata kama ni PhD ya kemia, bado hiyo kemia Katika usomaji na kufanya utafiti inakua addressed kwa Kiingeereza.
Una maana Magufuli hajui Kingereza cha kuandika na kuongea. Hivi alipokuwa anafundisha alikuwa akitumia lugha gani. Kila mtu anaweza kuamua kutumia lugha yoyote ile bora wale anaongea nao wanaijuwa hiyo lugha. Lugha yetu TZ ni Kiswahili, kwa hiyo Magu anayo haki kutumia Kiswahili anapoongea na Watanzania.
 
Back
Top Bottom