Ukiangalia ligi ya Tanzania kuna vituko sana na moja ya kituko ni mtu anakuambia simba ni timu bora na imeonewa na marefa ndo sababu ya kutokuchukua kombe ebu tuangalie takwimu zifuatazo
Timu iliyotoa mfungaji bora sio simba
Timu iliyotoa top assist sio simba
Timu iliyofunga magoli mengi sio simba
Timu iliyofungwa magoli machache sio simba
Timu iliyoshinda mechi nyingi sio simba
Wachezaji waliofunga kati ya magoli manane na 17 simba wako wawili tu
Ukiangalia kwenye hayo mambo 6 hakuna sehemu hata moja timu ya simba inaongoza sasa unajiuliza hiyo timu imeonewaje na marefa
Mashabiki na viongozi wa simba wanatumia mechi ya Yanga vs Simba mzunguko wa kwanza kusema wanaonewa ila kwenye hiyo mechi hiyo hiyo linesman alirule offside ya uongo ya Prince Dube na alikuwa amebaki na kipa hata kwenye hiyo mechi yanga wanamalalamiko yao