Wanaotafuna Pesa za Jimbo la Kawe ni hawa hapa...

Mkuu Chige ,kongole sana kwa ufafanuzi wa kiwango cha Ph.D ya ukweli ya M.I.T.
Kama kwa ufafanuzi huu bado kuna watu hawataelewa,basi huko Tanzania kutakuwa kuna watu wenye matatizo makubwa ya kiakili.
Mungu akubariki sana mkuu Chige
Mkuu residentura,

Taifa kama taifa lina viumbe wa ajabu kuliko maelezo!

Kuhusu kutoelewa, YES, wapo wengi tu ambao hawataelewa!! Wapo ambao hawataelewa kwa sababu wameshajitoa ufahamu na hivyo kuwa katika wakati mgumu kuelewa jambo lolote lakini wapo ambao pia hawataelewa kwa sababu tu uwezo wa kuelewa umeishia njiani!
 
Mkuu Chige ,sijapata kuona awamu ambayo wapiga propanda wa CCM ni hovyo kama hii. Si wa mitandaoni, vyombo vya habari wala viongozi wenyewe,ni hovyo hovyo hovyo balaa.
 
Hatakasiki Sauti ya zege mkuu, hata uzikili uchi
 
Ume elimisha sana lakini ukweli unabaki, Wabunge wote waliokaa majimboni kwao kwa zaidi ya miaka 10 au vipindi viwili wanatengenezewa sana mizengwe.

Watu wa Kawe wamemchoka Halima na sio vinginevyo.
Sio kweli
Halima ni bora 💯x💯💯💯💯💯💯kuliko tapeli movie actor mchungaji fake so usituchagulie tafadhali
 
..Na Ndugai anapofungia wabunge wa upinzani kuhudhuria vikao vya bunge hajui kwamba kuna maslahi ya wananchi yatakuwa yanajadiliwa? Na majimbo yanayoongozwa na ccm maeneo mbalimbali lakini yamekithiri kwa umasikini mna utetezi gani?
Hafunguwi mbunge pasipo kuwepo sababu zenye kueleweka.

Yule wa Arumeru alivuliwa kabisa ubunge kwa utoro wake, ukiwa mjeuri lazima ukutane na spika mwenye kiburi.

Ukiwa unaelewa uzito wa nafasi yako huwezi kuwa na viburi vya kitoto vyenye kuwaumiza wapiga kura wako.

Kusema majimbo ya CCM yamekithiri umaskini ni kukariri maisha, siku hazibaki vile vile kama miaka ya nyuma.
 

..umasikini wa jimbo la Ndugai unaweza kulinganisha na jimbo lolote linaloongozwa na wapinzani?

..je, ina maana Ndugai alikuwa akiiba fedha za mfuko wa jimbo, au alikuwa akitoka nje wakati wa mijadala ya bajeti?

..katika kampeni hizi pia tumesikia kwamba wananchi wa Chato wana shida kubwa ya maji, lakini wamejengewa uwanja wa ndege wa kimataifa.
 
Huu ndio upuuzi uliotukuka-yaani mbunge hawezi kufanya lolote hadi akaongee na raisi. Sasa namuelewa Lissu.
Mbunge kazi yake kuwa kuungo kati ya wananchi na serikali .Sasa alienda kufanya nini bungeni kama hiyo kazi haiwezi na hana ushawishi kwa serikali? So bora jimbo la kawe lingekaa bila mbunge lisubiri tu huruma za serikali

Halima Mdee safari lazima afungashwe virago kazi ya kuwa kiungo kati ya wana Kawe na serikali hawezi
 
..Na Ndugai anapofungia wabunge wa upinzani kuhudhuria vikao vya bunge hajui kwamba kuna maslahi ya wananchi yatakuwa yanajadiliwa? Na majimbo yanayoongozwa na ccm maeneo mbalimbali lakini yamekithiri kwa umasikini mna utetezi gani?
Angalia hoja zao zote za kufungiwa ukishaona wanafungiwa kwa kuleta hoja za majimbo yao?

Hoja zote za wao kutolewa haxihusiana hata Siku moja na majimbo yao

Wakikaa mle bungeni wala hawahangaiki na mambo ya majimboni kwao
 
Mfano jimbo hoi la Kongwa!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mbunge kama mwenyekiti wa kamati ana uwezo mkubwa wa kuhoji matumizi ya pesa! Kukaa kimya ndio kutokuwajibika
 
Angalia hoja zao zote za kufungiwa ukishaona wanafungiwa kwa kuleta hoja za majimbo yao?

Hoja zote za wao kutolewa haxihusiana hata Siku moja na majimbo yao

Wakikaa mle bungeni wala hawahangaiki na mambo ya majimboni kwao

..kama umewafungia utajuaje walichotaka kujadili wakati wamefungiwa?

..mimi nimeona mara nyingi wanafungiwa kwa fitina za Spika Ndugai.

..pia Spika Ndugai amekuwa akizuia bajeti mbadala kusomwa, na humo ndimo kuna mapendekezo ya kambi ya upinzani kuhusu maendeleo ya Tanzania.
 
NI KWELI KABISA. Kilangila.
 

..majimbo mengi hapa nchini, na zaidi yanayoongozwa na wabunge wa ccm, yanedorora kimaendeleo.

..je, majority ya wabunge wa ccm wameshindwa kuwa kiungo kati yao na serikali ya chama chao?
 
Unavyoongea utadhani kuna jimbo mwaka 1961 lilishakuwa tajiri tangu siku ile ya uhuru!!.

Maendeleo ni mchakato wa miaka na miaka sio sawa na upishi wa chapati na chai.

Marekani kule California kuna watu wanalala nje lakini kuna mabilionea wanaocheza sinema na viwanja vya ndege.

Tajiri na maskini walikuwepo kabla hatujazaliwa na tutakufa tukiwaacha.
 
Huyo anayejiita Mtumishi wa Mungu kondoo kawaacha na nani? Sipati picha siku akiukosa ubunge atakavyorudi kwa kasi kwenda kukusanya sadaka [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…