Wanaotafuna Pesa za Jimbo la Kawe ni hawa hapa...


..kwa mfano, fedha za mfuko wa maendeleo jimbo la KONGWA zimekwenda wapi?

..Je, Spika Ndugai ameiba mabilioni ya fedha za mfuko wa jimbo?

..Je, Spika Ndugai hana "connection" nzuri na serikali na mawaziri?

..Je, Spika Ndugai amekuwa haungi mkono bajeti kila mwaka?
 

Wananchi hatuelewi Sheria hivo tunaingizwa Mkenge na Wanasiasa kwenye Propaganda ya Wabunge kula Pesa za Majimbo!
 
Ufafanuzi mzuri sana.[emoji123][emoji123][emoji123][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Hahaha uzuri wa maelezo ni kuwa mnalazimika kujitetea kwa kutoa maelezo...yaani mchezo umebadilika ...baadala ya kutuhumu Kama ilivyozoeleka Sasa nyie mnatuhumiwa na mnalazimika kutoa maelezo...Safi Sana..mko on defensive...
 
Kumbuka kuna vitu kama ujenzi wa zahanati na na shule, kuna miradi mingi mikubwa inaendelea.


Halafu sio kweli kwamba majimbo ya wapinzani yote yana neema.

Siasa ukizijua utakuwa na uhuru mpana sana wa kimtazamo.
 
Hahaha uzuri wa maelezo ni kuwa mnalazimika kujitetea kwa kutoa maelezo...yaani mchezo umebadilika ...baadala ya kutuhumu Kama ilivyozoeleka Sasa nyie mnatuhumiwa na mnalazimika kutoa maelezo...Safi Sana..mko on defensive...
Jimbo la kawe ni kubwa kumzidi Halima.

Linahitaji mbunge mwenye mtazamo wa kweli wa kutumikia watu.
 

Hilo la huyo mbunge wa Arumeru bora ungekaa kimya, alichokifanya kimefahamika kilikuwa na msukumo gani, na sasa majibu yako wazi.
 
Kumbuka kuna vitu kama ujenzi wa zahanati na na shule, kuna miradi mingi mikubwa inaendelea.


Halafu sio kweli kwamba majimbo ya wapinzani yote yana neema.

Siasa ukizijua utakuwa na uhuru mpana sana wa kimtazamo.

..Ndugai kamfukuza Nassari, lakini jimbo la Ndugai lina changamoto kuliko la Nassari.

..Mbunge wa CCM wa Tabora Mjini alikuwa mwenyekiti wa kamati inayofukuza wabunge wa upinzani, sasa hebu niambie hali ya kiuchumi ya jimbo lake ikoje ukilinganisha na majority ya majimbo yanayoongozwa na wapinzani?

..Jimbo anapotoka Raisi Magufuli wananchi wana changamoto kubwa sana ya maji, lakini Raisi kawajengea uwanja wa ndege wa kimataifa usiokuwa na faida kwao, na usiokuwa na matumizi kwa taifa.
 
 
Hakika umedadavua na umma umekusikia ccm ni wapotoshaji na waongo lila sehemu ndo maana miaka 59 and bado ni makini wakutupwa
 
Viwanja vya ndege ni vitu strategic huwezi kuziona faida zake leo wala kesho. Masuala ya utalii huwezi kuyapima kwa mwaka mmoja au miwili.


Kwa Tundu Lissu kuna maendeleo gani ya maana?. Yapo majimbo mengi tu ya wapinzani hayana chochote cha maana, Bunda kuna maendeleo gani?.

Na kwa awamu hii tusidanganyane. Vinajengwa vitu vingi vitakavyokuja kuinua uchumi mkuu wa taifa ndani ya miaka michache ijayo.
 
Hahaha uzuri wa maelezo ni kuwa mnalazimika kujitetea kwa kutoa maelezo...yaani mchezo umebadilika ...baadala ya kutuhumu Kama ilivyozoeleka Sasa nyie mnatuhumiwa na mnalazimika kutoa mae
Badala ya kujichekesha chekesha, unatakiwa kujadili mada, au kujibu maswali yanayotokana na mada ambayo ni:-
1. Kwa mfumo huo uliotajwa kwenye Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo, huyo Halima anaibaje ibaje?
2. Kama mkwamo wa Kawe unatokana na Halima kutafuna pesa za jimbo, je mkwamo wa majimbo mia kadhaa yanayoongozwa na CCM unatokana na wizi unaofanywa na nani?

So, jibu hayo maswali na kama huna jibu, piga kimya coz' napenda kujadili kwa hoja!
 
Yaani unataka kutuambia Chato ni more strategic kuliko Tanga, Tabora, Morogoro, Iringa, Lindi ilikogundulika trillions of cubic feet of gas, Bukoba, Musoma, and many more?!

What's so special in Chato cha kuzidi maeneo niliyotaja hapo juu?! Ile mbuga ya kutegemea kuchukua wanyama kutoka mbuga zingine?!

Sasa kama mbuga inayotegemea wanyama kutoka mbuga zingine tu mtu anaamua kuijengea International Airport, Musoma iliyo jirani na Serengeti National Park tuseme vipi?!

Hebu tupe 10 years forecast summary itakayofanya Chato International Airport kuwa economically and commercially viable ndani ya huo muda!!!
 
Kwa haya 'Madini' yaliyowekwa hapa 'Kiuweledi' na 'Kimantiki' kabisa na Chige nashauri JPM arejee tena Tanganyika Packers kuomba Radhi Wadau.
Ina maana JPM nae kafanya hizi cheap propaganda huko Kawe?!
 
Chato ni altenative airport ya Mwanza airport.

Kwenye masuala ya anga unapokuwa na Hub kwa maana ya uwanja mkubwa wa kimataifa ni lazima karibu yake uwepo uwanja wa akiba.

Dar ikiwa hub uwanja wa msaada ni Unguja.

KIA ikiwa ni hub Arusha ni alternative airport.

Mwanza unakwenda kuwa hub kwa maana ya uwanja mkubwa wa afrika mashariki hivyo Chato kiutalaam ni uwanja wa msaada kwani ni dakika kumi tu kutoka Mwanza Airport mpaka Chato Airport.

Kingine ni kwamba kule kuna mbuga za wanyama hivyo umuhimu wa uwanja ule upo kwenye utalii.

Nchi yetu imebarikiwa sana kulinganisha na tabia zetu za kulalamika hovyo mitandaoni. Miaka michache ijayo utaelewa maana ya hub ya Mwanza na Chato kuwa ni uwanja wa msaada.
 
Halima umejitahidi sana kujitetea. Lakini umechelewa.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Natakiwa na Nani kujibu mada hiyo?! Kauli yako ni ya kidikteta...hapa JF hakuna kulazimishana...naweza nikaamua kucheka tu..naweza nikajibu ok..naweza nisijibu chochote...ambacho siruhusiwi ni matusi tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…