Wanaotaka kuanza kusoma CPA karibuni tushauriane

swali fikirishi..hivi ukiachana na waliosoma accounts....wengine wote waliosoma degree za courses tofauti na accounting..wanaweza soma CPA, na je inawasaidia kitu gani?
 
kivip mkuu
Course ngumu lakini return yake kwa Tanzania ni hovyo tu. Yaani unachokiwekeza, muda unaotumia kusoma na shida zote za kuhangaika kuipata hazilingani ni return yake.

Kwa gharama utakazotumia na muda utakaopoteza kuhangaika na cpa ukiuwekeza kwenye mambo mengine unakuwa mbali.

Kwa sasa unaweza kuipata cpa na ukaendelea kukaa mtaani bila ajira. Nchi zingine ukiwa na cpa wewe ni tajiri ila sio kwa bongo.
 
Bongo roho mbaya na wivu imetawala, mtu anaona bora akupige chini, kuliko akupe kitengo na CPA yako, alafu umpite mshahara, privileges nyingine.

Asilimia kubwa upoteze mda wako, kuongeza skills za mikono, unajua huwez kulala njaa mtaani.

Tusome kwa kuangalia demands ya soko, sio usome tu kwa kuiga mtu au uonekane unasoma vitu vigumu.
 
Nchi hii huwa inafuata mkumbo tu lakini haijawa tayari kabisa kuendana na hadhi ya kile inachokiiga. South Africa ukiwa na CPA umaskini unauaga.

Kule CPA wanalipwa hela ndefu sana, na kila mtu anatamani kuwa CPA ila mziki wa kuipata ndio kikwazo ila kwa wale wanaoweza kukomaa na kuipata huwa wanakula mema ya nchi.
 
South wanoko kuliko Waingereza.ACCA
 
Dah hizo sio mbinu ya kukamua watu pesa kweli?
 
Dah mbona mnatuchanganya sasa
Ili kufikia level ya kuwa Certified Public Accountant (CPA) kuna ngazi tano.

1.ATEC One (4 subjects)
2. ATEC Two (4 subjects)
3.Foundation (6 subjects)
4.Intermediate (6 subjects)
5.Final (4 subjects)

*Waliochukua degree za Accountacy wanaanzia Intermediate

*Non-Accountancy degree anaanzia Foundation. Masomo sita.

Form 6 leaver's
1. Waliochukua ECA wanaanza ATEC two
2. Waliochukua combi nyingine wa naanza ATEC one.

*Seatings za mitihani ni Mara mbili kwa mwaka. May na November
 
Duh aisee ule mziki wa cpa sijawahi ona, ulinipeleka mchaka mchaka mno hata nikiunganisha msuli wa form 6 na degree bado haifiki hata nusu.

Sitiing ya Kwanza - May

Sitting ya kwanza nilifanya May huku nimelipia tuition centre / review classes, nikitoka kazini naenda centre huku nimechoka balaa, kwa misifa nilichukua masomo 6, aisee nlikula za ovyoo ovyo usoni nikafaulu somo moja tu la B6 (hili somo jepesi kuzidi yote ni kama civics), nilitamani kulia!!, hata hivyo matokeo hayakunishangaza maana nilikuwa nikifika centre nimechoka sana kufatilia kwa umakini kipindi, nkirudi home nina majukumu ya kifamilia, n.k

Sitiing ya Pili - November

Sitting ya pili nikaona wacha nijisomee kivyangu tu nikaona centre inanibana nikawa private candidate nikachagua masomo yangu manne tu, ikawa ni mwendo wa kusolve past papers za bodi yetu na nchi nyingine ((acca, cima, cpa ireland, cpa ghana, cpa nigeria, ca india)), maswali ya vitabu, kula pindi youtube videos, google, n.k yani msuli wa notes asilimia 30 na msuli wa kusolve pepa asilimia 70, nilipiga pepa 4 nikachomoa zote B5 baba lao, B1 mama mwenye nyumba, b3 na b2. hiki kipindi nlikuwa naamka saa 10 nasukuma kalamu hadi saa 12 na nusu, computer ya kazini niliijaza pdf za maswali ya kutosha, saa 11 na nusu jioni nafika home nakaa hadi saa 12 na robo ivi naenda kasehemu karibu na home napiga piga msuli hadi saa 3 narudi home, weekends jumamosi na j2 saa 7 mchana hadi saa 10 then misele ya hapa na pale, jamani hiki kipindi sitasahau, hadi hapa nilipo nakumbuka formula za variance analysis topic ya b5.

Sitting ya tatu - May

sitting ya tatu ya may mwaka ujao nikafanya masomo manne ...ya final level matatu c1, c2, c4 na kiporo kimoja cha intermidiate b4, nilifaulu yote!! c4 na b4 masomo ya tax nilianza kusoma mapema mno kufikia July mambo kibao nisha cover hasa ukizingatia c4 ndio somo jepesi zaidi kwa inal level na kitabu chake ndio kidogo kuzidi vyote kwa intermidiate na final, kwa hio nikawa nimepunguza mzigo, ikawa na deal sana na c1 na c2 ambayo nayo hayakua mapya sana maana hilo c1 ni kaka mkubwa wa b2, c2 ni kaka mkubwa wa b3.

Sitting ya nne - November

sitting ya nne na ya mwisho Novemba hapo sasa nikawa nimebakiza somo moja tu la C3, mfalme wa wafalme, huyu mjinga ukienda kichwa kichwa anakupa kichapo heavy na hana undugu na masomo mengine ya intermediate kama wenzake kina c1, c2 na c4, ikawa kila siku jioni masaa mawili nampapasa yeye tu 🤠 tena nilianza mapema, siku ya mtihani ikafika nikafanya pepa na nikaimaliza nikiwa nina uhakika napata B lakini nilipotoka kwenye mtihani niliona kuna swali moja nimechanganya mafaili, matokeo yalivyotoka kinyonge ila si mbaya nilipata C.

graduation sikwenda, ratiba zilinibana

niliacha kazi private baada ya jambo kutiki serikalini

nilimaliza cpa ila moto ilionipelekea siji sahau

CONCLUSION:

-Wahi kuanza kusoma cpa kabla ya majukumu mengi, ukimaliza tu chuo we unganisha kama uwezo upo.

-Kama umeamua kusoma cpa uwe umemaanisha, Cpa haisomwi kilelemama, cpa inahitaji jitihada kubwa mno, watu wengi hukatisha safari zao za cpa kwa kukata tamaa baada ya kufeli mara kwa mara ama sheria za bodi kuwalazimu kuacha, hivyo usitegemee kusoma cpa kama unavyosoma chuoni, huku mtu kufaulu somo inabidi upate alama ya C inayoanzia maksi 40 lakini shughuli ya kupata hilo karai si mchezo, kuhusu kupata B ukiachana na somo la B6 ambalo wengi wanajipigia ni nadra sana maana wanaozipata ni takribani asilimia moja tu, kuhusu alama A ni kama muujiza maana binafsi nimewahi kuiona mara moja tu.

-Solve sana maswali kuliko kusoma notes, solve maswali ya pastpapers ya Tz, ireland, india, nigeria, cima, acca, n.k

-fanya walau masomo manne manne au matatu ili kupata timetable nzuri na concetration kubwa. kupiga masomo sita kwa mpigo si shughuli ya kitoto ile.

-usifatilie matokeo ya wenzako unaweza kukata tamaa na kuwa jealous, binafsi sitting yangu ya kwanza nlipofanya masomo 6 na kufaulu 1 tu kuna wenzangu walifaulu manne, ila hadi navyohitimu walikuwa hawajamaliza maana kuna masomo yalikuwa yamewabana wanarudia hadi mara 3 ngoma inadunda, kiufupi kuwahi kuanza ku clear masomo mengi usimcheke yule ambae kafaulu moja au kafeli yote


-Mitihani ya may inakazwa sana kuliko novemba, tumia nafasi za novemba vizuri
 
Hongera kiongoz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…